24 Ocak 2011 Pazartesi

Kutoka Katika Mkusanyiko

Kutoka Katika Mkusanyiko

wa Risala za Nuru

NENO LA ISHIRINI NA TATU

Kilichotungwa na

SAID NURSI

Kutoka Katika Mkusanyiko

wa Risala za Nuru

YİRMİÜÇÜNCÜ SÖZ

Suwahili Lisanına Tercümesi

Mafao ya Imani na Maelezo Kuhusu Furaha na Hudhuni ya Mwanadamu

Kwa Jina la Allah Mwingi wa Rehema na Huruma

95:4 Bila shaka Tumemuumba mwanadamu kwa umbo lililo bora kabisa

5: Halafu Tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini,

6: Ila wale wenye kuamini na kutenda mema, watakuwa na ujira usiokwisha (unaoendelea maisha) .”


MLANGO WA KWANZA

Katika Hoja Tano zifuatazo, tutaeleza faida tano tu miongoni mwa maelfu ya faida za imani

Hoja ya Kwanza

Kutokana na nuru ya imani, mwanadamu hupanda hadi akafikia daraja la ukamilifu la juu kuliko yote, na hupata thamani inayostahili kuingia Peponi. Na kutoka na na giza la kutokuwa na imani, hushuka hadi daraja la chini kuliko zote na huanguka hadi kufikia daraja linalostahili kuingia Motoni. Kwani imani ni uhusiano ambao humuunganisha mwanadamu na Mtengenezaji Mwenye Enzi.

Thamani ya mwanadamu hutokana na kuonyesha kwake sanaa ya Kiungu na udhihirisho wa Majina ya Uungu kwa njia ya imani yake. Kutoamini au kutokuwa na imani huukata uhusiano huo, na kutokana na kukatika huko kwa uhusiano, sanaa ya Kiungu hufichika, na thamani ya mwanadamu hupunguka hadi kuwa thamani ya kuweko kwake kimwili tu. Mwili wa mwanadamutakribani hauna thamani yeyote, kwani ni wa kuharibika na una mnyama wa kupita tu. Tunaelezea ukweli huu kwa njia ya hadithi yenye mafunzo:

Katika kazi ya sanaa, thamani ya nyenzo zinazotengezea hiyo sanaa hutofautiana na thamani ya ile sanaa inayoundwa.Wakati mwingine thamani hizi mbili zaweza kuwa sawa, na wakati mwingine hutokezea kuwa thamani ya dola tano ya sanaa hupatikana katika nyenzo kama chuma yenye thamani ya senti tano tu. Wakati mwingine hata sanaa ya kale huweza kugharimu dola milioni moja, wakati nyenzo iliyotengenezewa haigharimu hata senti kidogo tu. Iwapo sanaa hiyo ya kale itapelekwakwenye soko la vitu vya kale, huenda ikauzika kwa bei yake halisi kwa sababu ya sanaa iliyo nayo na jina la msanii stadi aliyeitengeneza. Ambapo, kazi hii ya sanaa inaweza kuuzwa kwa bei ya chuma chake kwenye soko la mhunzi.

Kwa mantiki hiyo hiyo, mwanadamu ni sanaa ya pekee yenye thamani kubwa mno ya Allah, Mwenye Enzi zote, na nimuujiza mororo na mzuri sana wa Uweza Wake, ambaye Alimuumba kudhihirisha Majina Yake yote na maandiko yake, kwa umbo la mfano mdogo wa ulimwengu. Kwa hiyo endapo mwanadamu atang'arishwa kwa maisha ya imani, basi maandiko yote yenye maana sana yataonekana. Mwenye imani huzidhihirishakupitia uhusiano wake na Mtengenezaji wake, yaani, sanaa ya Uungu iliyo ndani yake hudhihirishwa kwa njia ya matamshi kama haya:

“Mimi ni kazi ya MtengenezajiMwenye Enzi, ni kiumbe Chake, na ni lengo la Rehema Yake na Upaji Wake.”

Kwa hiyo, imani inadhihirisha dalili zote za sanaa katika umbo la mwanadamu, ambaye huzidisha thamani kwa muujibu wa uwiano wa udhihirisho wa sanaa hii, na kwa kuwa kiumbe kisicho maana, na hivyo hupata daraja ambayo ni juu ya viumbe vyote vingine, anakuwa mlengwa wa Nenola Allah na mgeni Wake humu duniani, na ambaye anastahili kuingia Peponi.

Lakini ikiwa kutoamini, ambako hutokana na kukatika kwa uhusiano huu, kutamwingia mwanadamu, tena kote kule kudhihirishwa kwenye maana sana kwa Majina ya Uungu hugubikwa na giza na huwa hayasomeki.Kwani, ikiwa msanii hatambuliki, sifa zinazodhihirisha thamani ya sanaa yake pia haziwezi kutambulika. Mingi ya mifano halisi ya zile sanaa bingwa na maandiko yaliyonyanyuliwa hufichika. muhimu na maandishi yaliyoinuliwa yatafichika.Kuhusu sifa za kuwepo kwake, mwanadamu asiye kuwa na imani husingizia vyanzo vya kipuuzi, husingizia asili nabahati, na hivyo huzirahisisha na kuwa kama kiyoo kitupu ingawa zenyewe,kwa yakini, ni kama almasi zinazog'aa.Yeye hawi tena wa maana kuliko kitu chochote cha kidunia, anakuwa kajihukumu mwenyewe aishimaisha ya mpito, na ya kusonga roho, ambaye sio mbora kuliko mnyama asiweza kujisaidia lolote, mhitaji na aliyedhurika. Hatimae huozelea mbali na kuwa udongo. Kutokuwa na imani, basi, huharibu asili ya mwanadamu na hugeuza almasi yake kuwa mkaa wa mawe.

Hoja ya Pili

Kama ambavyo imani ni nuru inayomuangaza mwanadamu na inadhihirisha jumbe zilizoandikwa ndani yake na Anayetegemewa Milele, hivyo ndivyo inavyoangaza ulimwengu na kuondoa giza kutoka kwenye mambo ya zamani na yajayo. Tutaeleza ukweli huu kwa njia ya tukio la kubuni nililo na uzoefu nalo kuhusu maana ya aya ifuatayo ya Qur’an tukufu:

2:257 Allah ni Mlinzi wa wale wanaoamini. Huwaongoza kutoka katika tabaka za giza kwenda katika nuru [Allwaahu waliyyul-ladhiyna aamanuw, yukhrijuhum-minadh-dhulumaati ilan-nuwr].”

Ilikuwa hivi:

Katika maono ya kubuni, nilikuwa nasimama katika daraja la kutisha lililojengwa juu ya bonde lenye kina kirefu kati ya milima miwili. Dunia nzima iligubikwa na wingu zito la giza kila sehemu. Nilivyotokea kutazama kulia kwangu, nilikuwa na ono la kaburi kubwa. Nilipotazama kushotoni kwangi nilihisi kama nilikuwa naona dhoruba kali na maafa yakiandaliwa kati kati ya mawimbi makubwa sana ya giza.

Kisha, nikatazama chini juu ya ukingo wa daraja hilo, na nilidhani nilikuwa naona genge lenye kina kirefu sana.

Katika giza lile la kutisha, nilikuwa na tochi yangu. Kwa kutumia mwanga wake dhaifu, mandhari ya kutisha sana ilionyeshwa kwangu. Daraja lote lilijaa majijoka mabaya sana, simba na mijidude ilinitokea hata nikajuta kwa nini nilikuwa na tochi. Kila nilikoielekeza niliona vitisho vivyo hivyo.

‘Tochi hii inaniletea matatizo tu’, nililia, na nikaitupa chini na ikavunjika. Halafu, ghafla tu, giza likatoweka na kila pahala pakaangazwa; ilkuwa kama nimewasha swichi ya taa kubwa kwa kule kuivunja tochi yangu,na nikaona kila kitu katika asili yake halisi.

Niligundua kwamba lile daraja, kwa hakika, lilikuwa ni njia kuu iliyopita juu ya ardhi tambarare nyoofu.

Lile kaburi kubwa lilokuwa kuumeni kwangu lilikuwa bustani zuri la kijani ambamo mikusanyiko ya kuabudu, sala, kutukuza na maongezi ilikuwa ikifanywa chini ya uongozi wa watu maarufu. Mandhari ya upande wa kushoto ambayo hapo mwanzoni nilifikiri ina dhoruba, ina magenge ya kutisha, sasa ilionekana kuwa ni ukumbi wa karamu, kibaraza chenye kivuli, mahala pazuri sana pa kupumzikia nyuma ya milima mizuri. Nilitambua kwamba yale niliyoyadhani kuwa ni majidude na majijoka yalikuwa, kwa kweli, ni wanyama waliowahi kufugwa kama ngamia, kondoo, na mbuzi. Nikasema:

“Sifa na shukrani zimwendee Allah kwa nuru ya imani,” kisha nikazindukana huku nikiisoma aya ifuatayo ya Qur’an:

“2:257 Allah ni Mlinzi wa wale wanaoamini. Huwaongoza kutoka katika tabaka za giza kwenda katika nuru [Allwaahu waliyyul-ladhiyna aamanuw, yukhrijuhum-minadh-dhulumaati ilan-nuwr].”

Ile milima miwili niliyoiona kwenye maono yangu ya kudhania ni, kwa hakika, mwanzo na mwisho wa maisha haya na maisha kati ya kifo na Ufufuko.

Daraja ni urefu wa maisha ya mtu, baina ya awamu mbili ya zamani (upande wa kulia) na ya baadae (upande wa kushoto). Tochi ni kibri yake yeye mwanadamu ambayo, kwa kutegemea fanaka zake yenyewe, haijali Ufunuo wa Kiungu. Kile nilichokiona mie mwanzo kama majidude ni matukio ya dunia na viumbe vya kiajabu ndani yake.

Kwa hivyo mtu ambaye kaangukia kwenye giza la upotofu na kutojali kwa sababu ya kuiamini kibri au kujiona kwake, anafanana na mimi katika hali ile ya mwanzo - katika mwanga dhaifu wa tochi. Kwa ujuzi wake usiotosha na unaopotosha, huyaona yaliyopita kama kaburi kubwa katika giza la kuzimika, na huyaona yajayo kama mandhari yenye dhoruba ya kutisha yanayotawaliwa na bahati. Hiyo tochi humuonyesha yeye matukio na viumbe ambavyo, kwa kweli, vimeamuriwa na Mwenye Hekima na Rehema zote na, katika kuitii Amri Yake, vinatimiza kazi maalumu na zinatekeleza madhumuni maalumu, kama majidude. Kwa hivyo yeye ndiye anayelengwa katika aya ifuatayo ya Qur’an:

“2:257 … Lakini wanaokufuru, walinzi wao ni mashetani. Huwatoa katika mwangaza na kuwaingiza katika kina cha giza. [.. Wal-ladhiyna kafaruw awliyaauhumut - twaaghuwt, yukhriju wnahum minan-nuwri iladh-ghulumaat]”

Lakini iwapo mwanadamu huyo atabahatika kupata mwongozo wa Uungu, na imani imwingie moyoni mwake, na ile kibri yake ya aina kama ya Firauni ivunjike, akikisikiliza Kitabu cha Allah, hapo atafanana na mimi kwenye hali ile ya baadae: ghafla ulimwengu wote utajazwa Nuru ya Kiungu, ukithibitisha maana ya aya ifuatayo ya Qur’an:

“24:35Allah ni nuru ya mbingu na ardhi. [Allwaahu nuwrus-samaawaati wal ardhw]”

Kisha ataona kwa macho ya moyo wake, kuwa yaliyopita sio kaburi kubwa, bali kila karne iliyopita na milki ya nabii au mtakatifu, ambapo roho zilizotakaswa, baada ya kukamilisha wajibu wa maisha yao (yaani wajibu wa kuabudu), kwa maneno haya:

“Allah ni Mkuu kuliko wote” kwenye ndimi zao, waliruka kwenda kwenye makazi ya juu zaidi, upande wa baadae. Hutazama kushotoni kwake, na kwa kutumia nuru ya imani, anaona, nyuma ya mageuziyale yaliyo kama mlima ya Dunia ya Katikati, na maisha yajayo, pahala pa karamu palipoandaliwa na Mwenye Huruma zote kwenye muhala mwa raha katika mabustani ya Peponi. Anaamini kuwa dhoruba zile, mitetemeko ya ardhi, magonjwa ya mlipuko, na mengineyo, yanafanya kazi fulani maalumu, kama vile anavyoelewa mvua ya vuli na upepo, kwa mfano, juu ya ukali wao, kuwa zina madhumunimengi mazuri.

Hoja ya Tatu

Imani ni nuru na ni nguvu.Naam, yeyote anayeipata imani ya kweli huweza kuukabili ulimwengu mzima, na kwa kadri ya nguvu ya imani yake, na akaepushiwa mashinikizo ya matukio. Huku akimtegemea Allah, husafiri katika mawimbi ya milima ya matukio katika meli ya maisha katika usalama kamili. Husafiri humo dunianikwa raha msitarehe mpaka siku ya mwisho, kwa kuwa keshapunguziwa mzigo wake kwa kuukabidhi kwa Nguvu za Mwenye Enzi zote. Kaburi litakuwa pahala pa kupumzikia kwake, na baadae aruke kwenda Peponi kuipata raha ya milele.

Kinyume cha hivyo, ikiwa hamtegemei Allah, achilia mbali kuruka, huo uzito wa maisha ya dunia utamteremsha awe wa chini kuliko wa chini wote. Kwa hivyo, imani hupatikana kwa kuthibitisha Umoja wa Kiungu, ambayo inahitaji kujisalimisha kwa Allah, na kujisalimisha kunahitaji kumtegemea Allah, na kutegemea kunaleta furaha katika dunia zote mbili.

Huku kumtegemea Allah kusieleweke vibaya:haimaanishi kupuuza ‘chanzo na athari’ moja kwa moja. Bali ina maana kwamba mtu ufikirie chanzo kama pazia la mkono wa Nguvu:katika kuzingatia hayo mtu huhitaji kukidhi Matakwa ya Kiungu, ambayo ni aina ya ibada kwa matendo. Kwamba kutaka na kutafuta ni matendo ambayo hayatoshi kuleta athari maalum. Mafanikio, sharti tuelewe, kwa muujibu wa imani sahihi, hukutazamiwi kutoka kwa yeyote ila Allah, Mwenye Enzi zote: tunamuamini Yeye kwamba Ndiye pekee Anayeleta athari, kwa hivyo daima tumshukuru Yeye.

Mfano wa yule anayemwamini Allah na wa yule asiyemwamini Allah ni kwa namna hii:

Wakati mmoja watu wawili walipanda meli wakiwa wamebeba mizigo mizito juu ya vicha na migongo yao.Mara walipopanda melini, moja wao aliutua mzigo wake juu ya meli akaukalia ili kuulinda.Lakini yule mwingine, kwa kuwa alikuwa mjinga na mwenye kujiona, hakuutua mzigo wake.Alivyoambiwa autue, ili ajipunguzie uzito wa mzigo, lakini akjibu: Hapana, sintoutua chini, usije ukapotea. Hata hivyo, mimi nina nguvu za kutosha za kuubeba”.Akaambiwa tena: “Lakini hii meli ya kifalme na ya kutegemewa inayotuchukua wewe na sie, ina nguvu zaidi, na inaweza kuilinda mali yako vizuri kuliko wewe. Bila shaka unaweza kuchoka, kupata kizunguzungu na ukaangukia baharini pamoja na mizigo yako. Nguvu zako zitashindwa. Kisha, ukiwa mgongo wako wenye kupinda pamoja na kichwa chako kisichokuwa na ubongo, hutoweza tena kuihimili mzigo ule ambao unazidi kuwa mzito kila wakati. Isitoshe, nahodha akikuona katika hali hiyo, ama atasema wewe umechanganyikiwa na akufukuze katika meli yake, au atafikiri: “Huyu mtu hana shukrani au ni msaliti, haiamini meli yetu au anaitilia shaka, na anatudhihaki.”, na akaamuru utiwe jela. Pia utatiwa alama na utataniwa na kila mtu. Kwa watazamaji, kujiona kwako kunadhihirisha udhaifu wako, majivuno yako yanadhirisha kutojiweza kwako lolote, na kujifanya kwako kunadhihirisha kudharaulika kwako: kwa ajili hiyo umekuwa kichekesho - tazama jinsi watu wote wanavyokucheka!

Maneno haya yalikuwa onyo la kumtosha huyo mtu maskini. Akautua mzigo wake juu ya meli na akaukalia, na akamwambia mwenziwe: “Allah Apendezwe nawe! Nimepata afuweni! Na zaidi, nimeepuka kufungwa jela, na kuchekwa.”

Sasa, ewe mtu, usiyeiweka imani yako kwa Allah! Zindukana , kama alivyofanya huyu mtu kwenye hadithi hii ya mafunzo, na uiweke imani yako kwa Allah, ili uepushwe na kuombaomba kwa viumbe vyote, na kutetemeka kwa woga katika kila tukio. Pia uepushwe na kujidanganya mwenyewe, na kuwa wa kuchekwa, na uepushwe na shinikizo za maisha haya na maisha Baada ya Kifo.

Hoja ya Nne

Imani humuwezesha mtu kupata utu wa kweli, na kupata daraja la juu kuliko viumbe vingine vyote.Kwa hiyo kuamini na kuabudu ndio wajibu wa msingi na wa maana sana kwa mwanadamu kuliko lolote jingine.Kinyume cha hivyo, kutoamini humshusha mwanadamu hadi awe nyama mwitu katili lisiloweza kujifanyia lolote lenyewe.

Miongoni mwa maelfu na maelfu ya ushahidi wa jambo hili, tofauti zilizopo kuhusu njia za kuzaliwa wanyama na watu ni ushahidi au alama tosha. Kwani wanyama wanapozaliwa, huelekea wameletwa duniani baada ya kufunzwa huko kwenye dunia nyingine na wakakamilishiwa vipaji vyao vyote. Baada ya saa saa au siku au miezi michache tu, hufikia hali ya kuwa na uwezo kamili wa kiasli wa kuishi maisha yake kwa muujibu wa kanuni zake na masharti yake maalumu.

Kwa muda usiozidi mwezi mmoja, ndege kama jurawaau nyuki, kwa mfano, hupata au tuseme hufunuliwa ustadi na uwezo wa kumudu kuishi katika mazingira yake mnamo muda wa siku ishirini, wakati mwanadamu atahitaji miaka ishirini. Hii maana yake ni kuwa, wajibu wa msingi wa wanyama, kazi yao muhimu sio kujikamilisha kwa kujifunza, au kujiendeleza kwa njia ya elimu ya kisayansi; wala sio kwa kusali na kuomba msaada kwa kuonyesha kutokujiweza kwao. Wajibu wao au kazi yao katika uumbaji ni kutenda mambo ndani ya mipaka ya vipaji vyao walivyozaliwa navyo, ambayo ndio aina ya ibada waliopangiwa nao.

Kinyumme cha hivyo, mwanadamu huzaliwa na ujuzi wa maisha na mazingira

Yake na haja ya kujifunza kila kitu. Akiwa hawezi kujua kikamilifu hali ya maisha hata baada ya miaka ishirini, anahitaji kuendelea kujifunza kwake mpaka mwisho wa maisha yake. Anaelekea kaletwa duniani na udhaifu mwingi na kutoweza kiasi kwamba inaweza kumchukua miaka hata miwili kujifunza jinsi ya kutembea tu.

Hawezi kubainisha kati ya uzuri na ubaya.hadi baada ya miaka kumi na tano; Na kwa muujibu wa kuishi katika jamii, afikie pahala pa kuweza kuchagua jambo Lipi lina faida na lipi halina faida kwake.

Kwa hivyo, wajibu muhimu wa mwanadamu, yaani ule unaohusu maisha yake, ni kupata ukamilifu kwa njia ya kujifunza, na kutangaza kumuabudu kwake Allah na kumtumikia Yeye kwa njia ya sala na dua. Sharti atafute majibu ya maswali kama haya yafuatayo:

“Kwa huruma ya nani maisha yangu yanaendeshwa kwa hekima namna hii?Kwa Ukarimu wa nani mimi ninafundishwa kwa upendo hivi?Kwa upendeleo na upaji wa nani mimi ninalishwa taratibu hivi? - na kisha sharti asali na aombe kwa “Mpaji wa Mahitaji” huku akitambua kinyenyekevu kuhusu mahitaji yake ambayo yeye mwenyewe hawezi kuyakidhi hata moja ya elfu moja yake. Kisha kuuelewa na kukiri kwake kwa kutojiweza kwa lolote na ufukara kutakuwa ndio mabawa mawili ambayo atayatumia kuruka kwenda katika daraja za juu kuliko zote, akiwa mtumwa wa Allah.

Hii maana yake ni kuwa mwanadamu alikuja katika maisha haya kutaka ukamilifu kwa njia ya elimu na sala. Kila kitu, kwa asli yake, ni lazima kinategemea elimu. Na msingi,chanzo, mwanga, roho ya elimu yote ya kweli ni elimu ya Allah, na imani ndio msingi wenyewe hasa wa elimu. Baada ya imani,sala hubakia kuwa ndio wajibu muhimu wa mwanadamu na ndio msingi hasa wa ibada. Kwani mwanadamu, juu ya kule kutojiweza kabisa kufanya lolote, anakabiliwa na mabalaa yasiyokwisha na ni mlengwa wa maadui wengi, na ana ugonjwa wa kuwa na mahitaji na matakwa mengi yasiyo kifani juu ya ufukara wake wa kupindukia.

Hebu fikiria jinsi mtoto anavyodhihirisha kutaka kwake kitu fulani ambacho hawezi kukifikia. Ama husema kuwa anakitaka kitukile, au hulia tu. Alichofanya katika njia zote hizi mbili ni aina ya ombi au sala, kwa njia ya maneno au matendo, kwa ulimi wa udhaifu wake,na hatimae hufikia lengo lake. Halikadhalika, mwanadamu ni kama mtoto anayependwa sana miongoni mwa viumbe hai. Ama hulia, kwa sababu ya udhaifu wake na kutojiweza kwake, mbele ya Milki ya Mwingi wa Rehema na Huruma, au atasali kwa sababu ya ufukara wake na mahitaji yake, ili akidhiwe mahitaji yake, na yeye sharti alipe kwa kutekeleza wajibu wake wakutoa shukurani kwa kukidhiwa hizo haja. Vinginevyo, kule kutoshukuru kwa yule anayedai kuwa na akili na uwezo mwingi sana kupita vyote, kulenga mahitaji yake yote kwenye uwezo wake yeye mwenyewe kuyakidhi, kutakujafanana na mtoto mtukutu ambaye analia kwa ajili ya inzi wanaombughudhi yeye. Aina hii ya kutokushukuru, inakwenda kinyume na asili muhimu ya mwanadamu na humfanya astahili adhabu kali.

Hoja ya Tano

Imani huhitaji sala iwe ndio njia ya uhakika ya kufaulu na ukamilifu; hulka ya mwanadamu anahitaji sana sala; na Allah huamuru hivi:

“25:77 Sema (Ewe Muhammad, kwa wanaokataa): 'Mola wangu asingekujalini kama si kule kusali kwenu. [Qul maa ya'abau bikum Rabbiy lawlaa du'aukum].”

“40:60 Na Mola wenu Anasema:, 'Niombeni, Nitakujibuni.[Wa qaala Rabbukumu- d'uwniy Astajib lakum.]”

Iwapo yeyote atashupaa aseme: 'Tunasali na kuomba mara nyingi, lakini hatupewi tunachoomba, ingawa aya iliyonukuliwa hapo juu inasema kuwa kila sala hukubaliwa pamoja”; jawabu litakuwa kama ifuatavyo:

Sala inayojibiwa haimaanishi kuwa “imekubalika” kwa kila hali. Kuna jibu kwa kila sala; lakini kuikubali sala na kutoa kitu kilichoombwa hutegemea Hekima ya Mwenye Nguvu. Kwa mfano, endapo mtoto mgonjwa atamwomba daktari ampe aina fulani ya dawa. Daktari yule ama atampa aina ile ya dawa, au atampa dawa bora zaidi kwa manufaa ya mtoto huyo; au hatompa dawa yeyote kabisa, iwapo ataamua kuwa aina yeyote ya dawa huenda ikawa mbaya kwa afya yake.

Halikadhalika, Mwenye Nguvu zote, Ambaye ni Msikivu na Anayeona vyote, bila shaka hujibu sala ya mtumwa Wake, na hugeuza hudhuni ya upweke wake ikawa furaha ya kuwa na Yeye. Lakini jibu lake halitegemei matakwa ya mwanadamu yeyote, bali hutegemea Hekima ya Kiungu. Kufuatana na Hekima Yake, Atatoa kinachoombwa au kilicho bora zaidi au hatotoa chochote kabisa.

Kwa hivyo, kwa vile Mwenyezi Mungu yupo kila pahala kila wakati na huona kila kitu kila wakati, Yeye huwa anajibu au anashughulikia sala za waja wake. Kwa njia ya kuwepo kwake na kujibu kwake, Yeye hugeuza athari za upweke kuwauzoefu.

Lakini hufanya hivyo, sio kwa muujibu wa matakwa yasiyofaa au yasiyo msingi ya huyo mtu, bali kwa muujibu wa matakwa ya hekima ya Kimungu. Mungu ama hutoa kile kilichoombwa, au kile ambacho ni bora zaidi, au hampi chochote kabisa.

Tena, sala ni aina ya ibada na zawadi ya ibada aghlabu hutolewa katika Maisha Baa ya Kifo. Kwa yakini, sala haisimamishwi kwa madhumuni ya kidunia.

Bali madhumuni ya kidunia ndio huwa sababu ya kusimamisha sala.Kwa mfano, sala au maombi kwa ajili ya mvua ni aina ya ibada; na ukosefu wa mvua ndio sababu ya sala hiyo sio madhumuni yake. Ikiwa mvua itafanywa ndio lengo pekee la sala, basi sala hiyo haitakubaliwa kwa kuwa haitokuwa sala ya kweli, haitodhamiria kuipata radhi ya Allah.

Machweo ya juapia huashiria wakati wa sala ya jioni; na kupatwa kwa jua au mwezini nyakati za ibada mbili maalum ziitwazo salat-al-kusuf na salat-al-khusuf. Kwa kuwa kufunikwa kwa alama mbili hizo zinazong'ara, jua na mwezi, ni aina bili za udhihirisho wa ilki ya Uungu, Mwenye Nguvu zotehuwaamuru watumwa Wake kufanya aina ya ibada ambayo ni makhsusi kwa matukio yale. Lakini sala kama hiyo haisaliwi ili kusababisha kufunikwa huko kuishe - kwani kudumu na mwisho wa matukio hayo kumeshajulikana kwa njia ya mahesabu ya kinajimu. Mantiki hiyo hiyo inahusu ukame na hata maafa au mabaa mengine. Yote hufuatiwa na aina fulani za sala.

Katika nyakati kama hizo, mwanadamu ndipo hutambua kule kutojiweza kwake kwa lolote na hivyo huhisi haja ya kutaka ukimbizi mbele ya ukuu wa Mwenye Enzi zote kwa njia ya sala na dua.

Sasa, ikiwa afa hilo halitositishwa hata baada ya kusimamisha sala nyingi, mtu usiseme:

“Sala yangu haikukubaliwa”, lakini useme: “Wakati wa sala bado haujaisha”. Iwapo Allah Atasitishia afa hilo, basi hii itatokana na Huruma Zake na Upaji Wake, na wakati ule huwa ndio alama ya kumalizika kwa sababu maalum ya sala ile.

Mwanadamu sharti atake radhi ya Allah kwa njia ya kumuabudu Yeye.

Lazima akiri ufukara na udhaifu wake katika sala yake, na aombe ukimbizi Kwake katika sala; na asiingilie katika shughuli za Umola Wake. Lazima aache uchukuaji hatua Kwake Yeye Nwenyewe, na ategemee Hekima Zake. Asishitaki Rehema Zake.

Kila kiumbe, kama ilivyosemwa kwenye aya maalumu za Qur'an, humpa Allah aina yake fulani ya kumtukuza na aina yake maalumu ya ibada, na ambacho kinaifikia Milki ya Allah kutoka ulimwengu wote ni aina ya sala. Viumbe vingine kama mimea na wanyama husali kwa njia ya ndimi za uwezo wao wa kutimiza umbo kamili na kuonyesha Majina fulani ya Kiungu. [Kwa mfano mbegu za mimea na manii ya wanyama fulani huzaa kiasili mimea na wanyama.Zina uwezo huo, kwa hiyo muelekeo wake wa kukomaa, kwa hakika, ndio sala ; katika kufanya hivyo hukiri na kudhihirisha Majina fulani ya Kiungu.

Kama Mwenye Kuendeleza, Mwenye Kuunda, nk.]

Aina nyingine ya sala huonyeshwa katika ulimi wa matakwa asilia. Viumbe vyote hai husali kwa Mwenye Huruma sana ili awape ridhaa ya matakwa yao muhimu ambayo waowenyewe wanashindwa kuyakidhi.Aina nyingine tena ya sala ni ile inayofanywa katika ulimi wa kutojiweza kabisa . Kiumbe hai kikiwa katika shida huchukua ukimbizi kwa Mlinzi Asiyeonekana kwa njia ya maombi ya dhati kabisa, na hugeukia kwa Mola wake Mwingi wa Huruma. Hizi aina tatu za sala hukubalika kila mara, isipokuwa zikiwa na vikwazo fulani.

Aina ya nne ya sala, ambayo inafahamika kwa kila mtu,ni ile tunayoifanya.

Hii pia imegawanyika katika aina mbili: moja ni ile ifanyayo kazi na ni ya matendo; na nyingine ni ya maneno na ya moyoni. Kwa mfano kutenda jambo kwa muujibu wa sababu ni sala ya utendaji. Kwa kule kukidhi sababu, mwanadamu hujaribu kupata ridhaa ya Allah kwa ombi lake, kwani sababu peke yake hazitoshi kuleta matokeo, na ni Allah peke Yake Ndiye hutoa matokeo. Kwa mfano, kulima ardhi, ni aina nyingine ya sala ya utendaji, ambayo kwa kweli ni njia ya kugonga kwenye mlango wa hazina ya Huruma ya Allah. Aina hii ya sala mara nyingi hukubalika, kwa vile ni maombi kwa Jina la Kiungu, Mwingi wa Ukarimu.

Kuhusu hiyo aina ya pili ya sala ya wanadamu, ambayo hufanywa kwa ulimi na moyo, hii ndio ya kweli hasa; ni ya kumuomba Allah kutoka moyoni kitu ambacho mikono yetu sisi haiwezi kukifikia. Sehemumuhimu kuliko zote za aina hii ya sala, na matunda yake mazuri na matamu kuliko yote ni, muombaji hujua kuwa yupo Yeye Anayemsikia, Anayejua kila kinachotokea moyoni mwake, Ambaye Uweza Wake unasambaa kila pahali, Ambaye Anaweza kukidhi kila Takwa lake, na Ambaye huja kumsaidia kwa sababu ya rehema na huruma kwa ajili ya udhaifu na kutojitosheleza kwake.

Na hivyo, Ewe mwanadamu masikini usiweza kujisaidia! Kamwe usiiwache sala ambayo ndio ufunguo wa Hazina ya Huruma na njia ya kuifikia Pawa Isiyo Kifani. Ing'ang'anie; panda hadi kwenye daraja kubwa kuliko yote la utu, na ukiwa kiumbe uliyependelewa na wa juu kuliko vyote, ongeza katika sala yako sala ya ulimwengu mzima. Sema kwa niaba ya viumbe vyote:

“1:5.. Wewe tu Ndiye tunayekuomba msaada.”, na uwe mfano mzuri kwa viumbe vyote!


MLANGO WA PILI

Mlango huu una Maelezo Matano kuhusu furaha na hudhuni ya mwanadamu.

[Mwanadamu aliumbwa kwa umbile zuri kuliko yote, kwa mtindo mzuri kuliko mingine ya uumbaji na akapewa uwezo wa kufahamu mengi. Kwa hiyo amepelekwa katika uwanja wa majaribio ambako ama atapanda hadi daraja la juu kuliko yote, au atashuka hadi daraja ya chini kuliko yote. Daima mwanadamu ana njia mbili zilizo wazi kwake, ya kupanda bila kikomo au kushuka bila kikomo. Mwanadamu yupo hapa duniani kama muujiza wa uwezana kilele cha uumbaji. Sasa tutaelezea siri ya huku kupanda na kushuka kwa mwanadamu katika maelezo matano.]

Elezo la Kwanza

Mwanadamu ana uhusiano na , na anazihitaji takribani aina zote za viumbe.

Mahitaji yake yanakwenda mbali katika sehemu zote za ulimwengu, na matamanio yake yanafika mpaka milele. Kama anavyotamani ua moja, ndivyo anavyoyatamani majira yote ya vuli. Anapenda bustani na pia Pepo ya milele. Kama anavyotaka kumwona rafiki yake, ndivyo anavyotaka kumwona Yeye Mwenye Enzi, Mwenye Uzuri wote. Kama anavtotarajia sana kupiga hodi kwa rafiki yake mpenzi amzuru ndivyo pia anataka kuomba ukimbizi mbele ya hadhikuuya Mwenye Enzi zote, Ambaye ataufunga mlango wa dunia hii na aufungue mlango waMaisha Baada ya Kifo, dunia ya maajabu, Ambaye ataibadilisha dunia hii na kuleta ijayo ili aepeke na mtenganona asilimia 99 yarafiki zake ambao wameondoka kwenda katika Dunia ya Katikati. Kwa hivyo, kwa mtu aliye katika hali hii, lengo la kweli la ibada kwake linaweza kuwa tu ni Mwenye Enzi zote Mtukufu, Mwingi wa Rehema zote Mwenye Uzuri usio kifani, Mwenye Hekima zote za Ukamilifu, Ambaye mikononi Mwake Ndimo mlimo hatamu za kila kitu, Ambaye ndiye anayemiliki mafao ya kila kiishicho, Anayeona kila kitu na yupo kila pahala, Asiyezuilika na mipaka yeyote, Aliye huru bila vikwazo vyovyote, Asiyekuwa na dosari yeyote au kosa lolote au upungufu wowote. Kwani Yeye Ambaye Anaweza kukidhi mahitaji yasiyo kikomo ya mwanadamu sharti Awe ni Mwenye Uweza Mwingi Usio Kipimo na Ujuzi wa aina zote. Kwa hiyo Yeye Ndiye peke Anayestahili kuabudiwa.

Sasa, Ewe mwanadamu! Iwapo unamuabudu Yeye peke Yake, utalifikia daraja la juu ya viumbe vyote vingine. Ukikataa kumwabudu Yeye, utakuwa mtumwa aliyedhalilishwa wa viumbe visivyowezakujisaidia. Ukiwacha sala na imani kwa Allah, ubakie kutegemea ubinafsi na uwezo wako mwenyewe, na udai ukuu wa kujiona, utashushwa katika daraja la chini kuliko nyuki au mchwa, na dhaifu kuliko inzi au buibui, kuhusu matendo chanya na ugunduzi wa kujenga. Lakini,katika kutenda maovu na uharibifu, utakuwa na uzani mzito kuliko mlima na utakuwa mharibifu kuliko gonjwa la kuua sana Sababu yahe ni hii: unazo namna mbili za kuwa - moja ni chanya na tendaji, na inahusu ugunduzi wa kujenga, kuishi, na wema; nyingine ni hasi na tendewaji na inahusu uharibifu, kutoishi na uovu.

Kuhusu namna ya kwanza ya kuwa: huwezi kushindana na nyuki au jurawa, na u dhaifu kuliko inzi au buibui; huwezi kufanya ambao wao wanaweza kuyafanya. Lakini kuhusu namna ya pili ya uharibifu,unaweza kuishinda milima, na hata ardhi na mbingu, kwani wewe unaweza kuhimili mzigo ambao vyenyewe haviwezi kuuhimili. Kwa hivyo, matendo yako yanaonyesha athari kwa njia pana zaidi kuliko yao.

Ukitenda jambo jema, au ukiunda kitu fulani,hii haikiuki uwezo wa mkono wako na nguvu zako. Lakini kinyume cha hivyo, matendo yako maovu na maharibifu, ni ya kuchokoza na ya kupanuka. Kwa mfano, kutokuwa na imani ni uovu, na uharibifu, na nikutokukiri. Dhambi moja, yaweza kuwa ni tusi kwa viumbe vyote, udhalilishaji wa Majina yote ya Kiungu na udhalilishaji wa wanadamu wote. Kwani viumbe vyote vina daraja kuu na kazi muhimu, kila moja ikiwa ni ujumbe wa Mola, kiyoo cha Utukufu Wake, na mtumishi wa Uungu Wake. Kutoamini huwanyang’anya daraja walizopewa na kazi hizi, na huwashusha wakawa vitu vya kuchezea vinavyotegemea bahati, hadi kwenye daraja ya kutokuwa na maana, vitu ambavyo havina kazi wala havina thamani, ambavyo huishia kuoza na kuharibika.

Na pia, kwa kunyang’anywa huko, huyatukana Majina ya Uungu, ambayo maandishi yake na udhihirisho wake mzuri, huonekana katika viyoo vya kila kilichoumbwa ulimwenguni kote. Kutoaminipia humuangusha chini mwanadamu ambaye ni kazi ya ushairi wa Hemima inayoonyesha udhihirisho wote wa Majina yote ya Kiungu, muujiza mkuu wa Uweza amba o, kama ilivyo mbegu, una mti mzima wa uumbaji, na khalifa wa Allah duniani, mkubwa kuliko malaika na na wa juu kuliko milima, ardhi na mbingu kwa muujibu wa imani aliyoichukua, kwenye daraja ambalo ni baya na dhaifu zaidi, asiye na usaidizi na mpweke zaidi kuliko mnyama wa chini kuliko wote. na humshusha hado awe katika daraja la bango la kawaida, ambalo huharibika na likose maana yeyote, akiwa kachanganyikiwana anaharibika haraka.

Kwa ujumla: Kuhusu uovu na uharibifu, roho ya kibinadamu, nafsi inayoamuru uovu inaweza kutenda makosa ya jinai yasiyohesabika na isababishe uharibifu usio kifani, wakati uwezo wake wa kutenda mema ni mdogo sana. Kwa mfano, inaweza kuharibu nyumba kwa muda siku moja, lakini haiwezi kuijenga nyumba hiyo hiyo kwa siku mia moja. Lakini endapo roho ile itaacha kujitegemea yenyewe, kujivuna kwake, na itegemee msaada wa Kiungu katika kufanya mema na uvumbuzi wa kujenga; ikiwa itaacha kutenda uovu na uharibifu, na iombe msamaha wa Kiungu na hivyo iwe mtumishi mkamilifu wa Allah, basi huwa ndio mkusudiwa wa aya ifuatayo ya Qur’an:

“25:70 Ila yule atakayetubia na kuamini na kutenda mema, basi hao ndio Allah Atawabadilishiamaovu yao kuwa mema. [Illaa man taaba wa aamana wa ‘amila ‘amalan swaalihan fa ulaaika yubaddilul-Lwaahu sayyiaatihimhasanaati].”

Uwezo usio kifani wa mwanadamukutenda maovu hugeuzwa kuwa uwezo usio kifani wa kutenda mema. Mwanadamu huifikia thamani ya “Umbo zuri kuliko yote ya uumbaji (creation)”, na hupanda hadi kufikia “wa juu kuliko wote walio juu”.

Ewe mwanadamu usiyejali, fikiria basi Hisani ya na Upaji wa Mwenye Enzi zote (All-Mighty). Wakati ambavyo, kwa hakika, ni haki kamili kuandika dhambi moja tu kama ilivyo kuandika dhambi elfu moja kwa muujibu wa kipimo chake cha matokeo na na athari zake,na tendo jema kama moja tu, Allah hufanya kinyume cha hivyo.Huandika tendo moja la dhambi kama moja, lakini huliandika tendo moja la wema kama kumi, au sabini, au mia saba, au mara zingine mara elfu saba. Pia sharti uelewe katika elezo hili kwamba kuingia Motoni ni malipo ya matendo ya mtu na haki safi, ambapo kuingia Peponi ni matokeo ya Hisani Yake tupu.

Elezo la Pili

Mwanadamu ana nyuso mbili: mmoja unatazama maisha haya ya dunia kwa sababu ya ubinafsi wake, na mwingine unatazama maisha ya milele kwa sababu ya asili yake kama mtumwa wa Allah. Kuhusu hiyo ya kwanza, yeye ni kiumbe masikini kweli - Uchaguo wake ni dhaifu kama unywele mmoja, uwezo wake umezingatiwa kwenye ufundi mmoja tu uliowekewa mpaka imara, maisha yake ni mafupi kama mmuliko wa mwangakulinganisha na maisha ya dunia, na kuishi kwake kimwili ni kama kwa kitu kidogo sana kinachoishia kuoza tu. Katika hali hii, yeye ni mjumbe wa aina moja tu kati ya aina nyingi sana za vinavyoishi, vilivyosambazwa kote kwenye kila ngazi ya ulimwengu.

Kuhusu huo uso wa pili, kwa muujibu wa kuona kutojiweza na kutotosheleza kwakekama mtumwa wa Allah, ni kimbe muhimu. Kwani Muumba Mwenye Hekima zote Ameweka katika aslili ya mwanadamu hali ya juu kabisa ya kutojiweza na ufukara ili awe kiyoo kionyeshi kinachorudisha udhihirisho mkubwa sana wa Huruma na Uweza wa Allah, na wa Utajiri na Ukarimu Wake. Kwa hivyo kwa muujibu wa imani na ibada, mwanadamu hupata uwezo na utajiri usio na mipaka.

Mwanadamu anafanana na mbegu kwa kuwa na uwezo wa kukua na kupata ukamilifu. Mbegu imepewa na Uweza uwezo mkubwa na hujaaliwa kuutekeleza kwa muujibu wa programu ya Kudura kuwa itachipua chini ya udongo na ikue hadi iwe mti “mkamilifu”kwa njia ya kuabudu kwake, kufuatana na lugha ya uwezo wake. Iwapo mbegu ile itatumia vibaya uwezo wake na ivivutie vitu viharibifu kwa sababu ya muelekeo, basi itaishia kuoza papo hapo pafinyu ilipo. Kinyume cha hivyo, ikiwa itatumia uwezo wake vizuri, kwa muujibu wa sheria Yake, kama isemavyo aya ifuatayo ya Qur’an:

“6:95 Allah Ndiye Mpasuaji (Muoteshaji) wa mbegu na kokwa zikawa miti...

[Innal-Lwaaha faaliqul habbi wan-nawaa...].”

kisha itachomoza kutoka katika pahala pake pafinyu, na ikuwe kuwa mti wa kutisha uliojaa matunda, na hulkayake ya udogo itakuja kuwakilisha ukweli mkubwa na wa dunia nzima.

Hulka ya mwanadamu pia imepewa na Uweza uwezomkubwa na imeandikwa programu muhimu na Kudura. Sasa iwapo mwanadamu atatumia uwezo wake na vipaji katika dunia ile finyu, chini ya udongo wa maisha ya kidunia, ili kukidhi matamanio yake ya kimwili na nafsi yake inayoamrisha uovu, ataharibika kama mbegu iliyooza, kwa ajili ya utamu usio maana katika maisha mafupi, na hivyo, ataiacha dunia hii huku akiwa na mzigo mkubwa wa kiroho katika roho yake isyo na bahati. Lakini,kwa upande mwingine akiiotesha ile mbegu ya uwezo wake chini ya “udongo wa ibada”kwa kutumia “maji ya Uislamu” na “nuru ya imani”, kwa muujibu wa sharia za Qur’an, na ikiwa atatumia vipaji vyake vya kiroho kwa madhumuni yake ya kweli, basi bila shaka atakua awe mti wa milele na mtukufu, ambao matawi yake yanafika mpaka kwenye Dunia ya Katikati na dunia ambamo mahitaji ya mwanadamu huchukua maumbo ya Maisha Baada ya Kifo tu, na huo utazaa matunda yasio hisabu makamilifu katika dunia ijayo. Kwa hakika atakuwa ni tunda lamti wa uumbaji ambalo litapendelewa sana huko Peponi na ukamilifu mwingi sana na baraka zisizo hesabu.

Maendeleo ya kweli ya mwanadamuyanawezekana kwa kugeuzavipaji vyake vyote, kama akili, moyo, roho, na dhana,kuelekea maisha ya milele, ili kila moja itashugulika na aina yake yenyewe ya ibada. Kwa kile ambacho watu waliopotea wanadhania kuwa ndio maendeleo, yaani, mtu kutumia vipaji vyake vyote, pamoja na moyo na akili, kwenye ubinafsi wa kimwili na wenye kuamrisha maovu ilikuonja raha zote za kidunia hadi ile raha ya chini kuliko zote, sio maendeleo, bali ni mpunguo na ufisadi. Niliwahi mara moja kuona ukweli huu katikamaono ya dhana ambayo ni kama ifuatavyo:

Niliwasili katika jiji kubwa lililojaa majumba ya kifalme. Nje ya baadhi ya majumba haya ya kifalme kuliendelezwa maonyesho ya kufurahisha watu.

Nilipokaribia moja ya majumba hayo, niliona kuwa mmiliki wa hilo jumba alikuwa yupo mlangoni, akicheza na mbwa. Wanawake walikuwa wakiongeaongea na vijana wageni, na wasichana walikuwa wakiandaa michezo ya watoto. Mlinda mlango alielekea kama anawadhibiti. Kisha nikatambua kuwa jumba lile ndani lilikuwa tupu, na kazi zote muhimu zikaachwa bila uangalizi wowote - ishara ya kuwa wakazi wa jumba hilo walikuwa mafisadi sana kiasi cha kufanya kazi hizo.

Kisha nikaja kwenye jumba la kifalme jingine kubwa. Safari hili mbwa mtii alikuwa kalala mlangoni, na jirani yake alisimama mlinda mlango mwenye uso wa ukali, uzito usiocheka. Jumba hilo lilikuwa kimya mno kwamba niliingia kwa mshangao.

Ndani yake kulikuwako shuguli nyingi, ghorofa juu ya ghorofa, wakazi walikuwa wakishughulika na kazi mbalimbali muhimu. Wanamume katika ghorofa ya kwanza walikuwa wakishughulika na utawala. Ghorofa ya pili wasichana na wavulana walikuwa wakisoma. Katika ghorofa ya tatu walikuwepo wanawake wanajishughulisha na sanaa nzuri na nakshi za kistadi. Mmiliki wa jumba hilo la kifalme alikuwa ghorofa ya juu akiwasiliana sasa zote na mfalme ili apate usalama wa watu wa nyumbani kwake, na kufanya kazi za daraja la juu kwa ajili ya maendeleo yake mwenyewe na kujikamilisha. Kwa kuwa hawakuniona, hakuna ambaye alinisimamisha,kwa hivyo niliweza kutembetembea kisha nikatoka zangu. Nje nikaona kuwa jiji limejaa majumba ya kifalme ya aina hizi mbili. Nilipouliza nikaambiwa kuwa yale majumba ambayo ndani ni matupu, na yaliyoelekea kuwa mazuri sana, yalikuwa ni ya watu wasioamini wa msitari wa mbele kabisa na waliopotea; na wa majumba mengine ni Waislamu waadilifu wenye daraja za juu. Kisha pembezoni nikaliona jumba la kifalme ambalo lilikuwa limeandikwa jina langu “SAID”.Nilipolitaza kwa makini nilihisi kama vile naiona picha yangu mle. Nikalia, nikazindukana na kuamka.

Sasa nitafafanua maono haya, na naomba Allah Ajaaliye yatokee vyema Lile jiji ni maisha ya kijamii ya wanadamu na ardhiya ustaarabu wa wanadamu. Kila jumba la kifalme ni mwanadamu, na wakazi wa majumba ya kifalme ni hisia na vipaji vya mwanadamu kama macho, masikio, akili, moyo na roho, na uwezo wa hasira na tamaa mbaya. Kila hisia na kipaji cha mwanadamu kina wajibu mahususi wa kuabudu, na pia raha mahususi na machungu mahususi. Ubinafsi na matamanio, na uwezo wa hasira na tamaa mbaya vinawasilisha mbwa na mlinda mlango wa jumba la kifalme. Kwa hivyo, ili kuzishinda hisia kuu na vipaji vya juu sanavya matamanio na fikra za kimwili, na kuvisababisha visahau wajibu wake muhimu, bila shaka ni mshusho na ufisadi, sio maendeleo. Unaweza kufafanuamaelezo mengine ya ono hili wewe mwenyewe.

Elezo la Tatu

Kwa mintaarafu ya matendo na jitahada zake za kimwili, mwanadamu sio zaidi ya mnyama dhaifu, kiumbe asiweza kujisaidia. Hata mduara wa milki yake ni mdogo kiasi ambacho vidole vyake vinaweza kugusa mzingo wake, na huo ndio udhaifu na kutojiweza mwenyewe na ulegevu wa mwanadamu kiasi kwamba hata wanyama wanaofugwa wameathiriwa navyo. Iwapo kwa mfano mbuzi na ng’ombe waliofugwa wakilinganishwa na wenzao wa mwituni, tofauti kubwa zitabainika kati yao.

Lakini akiwa kama kiumbe mtendewaji na mpokeaji anayetakiwa asali na kuomba, mwanadamu ni msafirimzuri anayeruhusiwa kukaa kidogo kwenye nyumba ya wageni ya dunia hii. Anakuwa ni mgeni waYeye Aliye Mkarimu Ambaye kampaa mwanadamu hazina za Huruma Yake isiyo kifani, na Amevisalimisha kwake kazi zake nyingi zisizo kifani za uweza wa uumbaji na hata watumishi Wake mahususi. Na pia Ameandaa kwa matumizi na furaha ya mgeni Wake eneo kubwa sana la kuonakiasi kwamba kipenyo chake ni mbali kadri ya upeo wa macho au upeo wa dhana.

Sasa basi, ikiwa mwanadamu , kwa kutegemea uwezo wake wa kimwili na wa kuzaliwa nao, analifanya lengo lake ni kuishi maisha ya kidunia na akazanie kula raha za maisha haya, atashindwa kupumua ndani ya duara finyu. Tena basi, sehemu za mwli wakena hisia na vipaji vyakevitamshitaki na kutoa ushahidi huko katika Maisha Baada ya Kifo. Lakini akijijua yeye mwenyewe kuwa ni mgeni, na atumie muda wake ndani ya mipaka iliyoidhinishwa na Mwenyeji wake Mkarimu, ataishi maisha ya furaha na na amani, na aifikie daraja ya juu kuliko zote miongoni mwa viumbe. Katika Maisha Baada ya Kifo atazawadiwa kwa maisha ya raha ya milele, na sehemu za viungo vyake na vipaji vyake vyote vitatoa ushahidi kumtetea yeye.

Vipaji vyote vizuri kabisa vya mwanadamu hakupewa ili avitumie katika Maisha haya ya kipuuzi ya kidunia, bali kapewa kwa ajili ya maisha muhimu sana ya milele. Akilinganishwa na wanyama, mwanadamu ana hisisa na vipaji vingi zaidi, ambapo raha anayoweza kupata kutoka kwenye maisha ya kimwili tu ni kidogo sana kuliko ile ya wanyama. Kila raha ya maisha ya kidunia huambatana na maelfu ya sehemu ndogo za machungu, na huharibiwa na hudhuni yaliyoachwa kutoka mambo ya zamani, woga wa yajayo, na kutoweka kwa raha yenyewe. Lakini hivi sivyo alivyo mnyama. Raha zake hazina machungu na starehe zake hazina wasiwasi. Wala haziathiriwi na hudhuni zayaliyopita, na wala wasiwasi wa yajayo hauwezi kumzuia katika starehe za maisha yake. Huishi maisha yaraha na humtukuza Muumbaji wake.

Kwa kumalizia, ikiwa mwanadamu, ambaye kaumbwa kwa umbo bora kuliko yote, anasisitiza maisha ya kidunia tu, hushushwa hadi kuifikia daraja mara mia chini kuliko ya jurawa, ingawa ana vipaji mara mia zaidi na vilivyokomaa zaidi kuliko vya mnyama. Katika kitabu kingine, nilieleza ukweli huu kwa njia ya hadithi ya kufunza. Sasa nitairudia tena, kama inahusu maudhui haya.

Mtu ampa mmoja wa watumishi wake vipande kumi vya dhahabu na anamuamuru akajishoneshee suti moja kwa kitambaa maalumu. Anampa mtumishi wake mwingine vipande elfu moja vya dhahabu na anampa orodha ya vitu akanunue sokoni. Wa kwanza ananunua suti nzuri ya kitambaa kizuri kuliko vyote kwa vile vipande kumi vya dhahabu. Huyu wa pili anafanya ujinga. Hatambui ni kiasi gani cha fedha amepewa, wala haisomi ile orodha ya vitu vya kununua, bali anafikiri anamuiga rafiki yake. Kwa hivyo anakwenda katika duka moja na anaagiza suti.

Muuza dukaasiyekuwa muadilifu anampa suti, kwa bei ya vipande elfu moja vya dhahabu, ya kitambaa kibaya kuliko vyote. Huyu masikini mtumishi anarejea kwa bwana wake ambako anakemewa sana na anapewa adhabu.

Yeyote mwenye akili anaona kwamba vipande elfu moja vya dhahabu Hakupewa huyu mtumishi ili anunue suti, lakini kwa ajili ya kazi muhimu.

Kwa njia hiyo hiyo, vipaji vya kiroho, na hisia ambazo mwanadamu kapewa, zimeendelezwa zaidi kuliko zile za wanyama. Kwa mfano jicho linaweza kutambua daraja zote za uzuri; hisia zake za kuonja, ulimi wake,vyaweza kutofautisha aina zote za ladha za vyakula, akili zake zinaweza kupenyahadi kwenye taarifa nyingi za ukweli; moyo wake unapendelea daraja zote za ukamilifu, na kadhalika.

Ambapo vipaji vya wanyama (isipokuwa kipaji kimoja ambacho huendelea sana katika kila mnyama kwa muujibu wa wajibu wake maalumu), huendelea kidogo sana au haviendelei kabisa.

Sababu ya mwanadamu kuwa na vipaji vingi ni kuwa, hisia za mwanadamu zimeendelea mbali sana kwa sababu ya akili yake. Aina nyingi za mahitaji yake zimemfanya afunue na kuendeleza aina mbalimbali za hisia, na kuwa mwepesi wa kuhisi vitu mbalimbali. Pia kwa sababu ya asili yake inayoweza kueleweka, mwanadamu kapewa matamanio ambayo huweza kugeuzwa kwa nia na malengo mengi. Kwa sababu ya utofautiwa kazi zake muhimu, hisia zake na vipaji vyake vimetanuliwa sana.

Isitoshe, kwa kuwa ana uwezo wa kufanya kila aina ya ibada, basi ana uwezo wa kutimiza kilaaina ya ukamilifu.

Bila shaka, utajiri huu wa vipaji na uwingi huu wa uwezo hauwezi kuwa alipewa kwa ajili ya maisha ya kidunia ya kipuuzi na kimuda tu. Vimo kwa mwanadamu kwa sababu wajibu wake muhimu ni kutambua kazi zinazolenga katika nia zisizo mwisho, za kuthibitisha kutokujiweza kwake mwenyewe, ufukara na kutojiosheleza katika aina ya ibada, kuchunguza kwa uwezo wake wa kuona mbali na uelewaji wa kupenya sana, na kuushuhudia kutukuzwa kwa Allah na viumbe wote, kutambua na kushukuru kwa misaada ya Yeye Aliye Mwingi wa Rehema iliyoletwa kwa njia ya mafao, na kutazama nakutafakari, kuzingatia maonyo kutoka ka tika miujiza ya Uweza wa Mola unaodhihirishwa katika kazi Zake za Uumbaji.

Ewe mwanadamu unayeabudu dunia, ambaye unavutiwa na maisha ya Dunia na ambaye hujuwi maana ya asili yako kama umbo bora kuliko maumbo ya viumbe vyote! Siku moja niliona asili ya kweli ya maisha ya dunia hii katika ono la kudhania kama ifuatavyo:

Nilitokezea kuwa katika safari ndefu. Mola wangu alinijaaliya nigunge safari hii. Akanipa polepole baadhi ya fedha kutoka kwenye vipande sitini vya dhahabu alivyonigawia mimi. Hii iliendelea kwa muda fulani, na baada ya muda nikawasili katika hoteli ambako kulikuweko starehe. Nilichezea kamali vipande kumi vya dhahabu pale kwa usiku mmoja wa starehe na ufuska. Kulipokucha, nikakosa fedha za kununulia vyakula ambavyo Nitahitaji huko niendako. Kilichobakia katika fedha nilizopewa ni machungu na hudhuni na majuto tu yaliyoachwa na dhambi na raha haramu.

Nilikuwa katika hali hiyo ya kuhudhunisha alipokuja mtu Na akaniambia hivi:

“Umepoteza kila ulichokuwa nacho na hivyo unastahili adhabu. Tena utaendelea hadi mwisho wa safari yako bila fedha. Lakini mlango wa toba haujafungwa, ukitumia akili yako. Ukipokea vipande vilivyobaki vya posho yako, weka nusu yake akiba, na ununulie vyakula muhimu utakavyohitaji mwisho wasafari yako.”

Ubinafsi wangu haukuridhika kuweka akiba ya nusu, kwa hivyo mtu yule Akasema:”Basi hifadhi theluthi moja yake.”

Lakini ubinafsi wangu haukuridhika na hii pia.Yule mtu akasisitiza: “Basi robo.”

Nilitambua kuwa ubinafsi wangu hauwezi kuacha pumbazi zake, hivyo Yule mtu aligeuka akaenda zake kwa hasira.

Katika wakati huo huo nilijikuta ninasafiri kwa treni ndani ya tundu ardhini La kupita treni kwa haraka mno kama vile nakwenda chini kiwima. Nilishikwa na hofu, lakini hapakuwepo popote pa kukimbilia.. Kwa mshangao mkuu nikayaona maua mazurina matunda matamu pembezoni mwa reli, yakining'inia kutoka pembezoni mwa hilo tundu la kupita treni. Nikafanya ujinga wa kujaribu kuyachuma baadhi yao. Lakini yalikuwa yamezungukwa na miiba ambayo kwa sababu ya kasi ya mwendo wa treni, ilinichana mikono nilipoyagusa, na kuifanya itoke damu. Nilichojaribu kukishikakiliniponyoka. Ghafla mtumishi akaja karibu yangu akasema:

“Nipe senti tano, nami nikulipe maua na matunda kiasi chochote unachotaka.

Vinginevyo, mikono yako hiyo iliyochanika, utapoteza mia badala ya tano.

Isitoshe, kuna adhabu ya kuyachuma bila ruhusa.”

Huku nikiwa nimefadhaishwa na hali hii, nilitazama nje dirishani kuona Wakati hili tundu la kupitia treni linakwisha. Lakini sikuuona mwisho. Niliiona Milango mingi katika kuta za hilo tundu la kupita treni ambamo abiria kutoka kwenye treni walikuwa wakirushiwa. Ghafla nikauona mlango mkabala na mie, ukiwa na jiwe la kaburi kila upande. Nilipochungulia nje nikaona jina langu, SAID, limeandikwa kwa herufi kubwa kwenye mawe hayo ya makaburi. Nikatoa kilio cha mshangao na toba. Bila kutazamia, nikasikia sauti ya yule mtu aliyenipa ushauri pale kwenye mlango wa hoteli, akaniambia:

“Je, umepata akili?” Nikamjibu: “Ndio. Lakini sasanimekata tamaa na hakuna niwezacho kufanya.”Akaniambia: “Tubia, na muamini Allah.” Nikajibu:

“Nafanya hivyo.”

Kisha nikaamka, na nikajikuta nimegeuka kuwa Said mpya, yule Said wa zamani alitoweka.

Sasa nitafafanua baadhi ya sura za ono hili la kudhania:

Safari ni maisha ya mwanadamu, ambayo, kwa hakika, ni safari kutoka katikadunia iso ya kweli ya milele, yakipitia awamu za tumbo la uzazi la mama, ujana, uzee, kaburini, Dunia ya Katikati, Ufufuo, na Daraja. Vipande sitini vya dhahabu ni miaka sitini yaani wastani wa umri wa mwanadamu. Nilipoona hilo ono nilikuwa nina umri wa miaka arubaini na tano. Allah peke Yake Ndiye Anayefahamu lini mie nitakufa. Mwanafunzi mwaminifu wa Qur'an Takatifu alinionyesha njia ya kweli ili nipate kuitumia mika kumi na mitano iliyobaki kwa ajili ya MaISHA Baada ya Kifo. Iuyo hoteli, kama nilivyokuja kuielewa, ni Istanbul (mji mkuu wa Turkey, nchi ya mwandishi wa kitabu hiki), kwangu mimi. Treni inawakilisha wakati, na kila behewa ni mwaka mmoja. Lile tundu la kupitia treni ni maisha ya kidunia, yale maua na matunda yenye miiba ni raha haramu na starehe zilizokatazwa zinazoufanya moyo utoke damu kwa mawazo ya kutengana mara ninapoyagusa.Kutoweka kwa raha huongeza hudhuni, na baki ya kuwa haramu, humfanya mtu apate adhabu.

Mtumishi katika treni alisema:

“Nipe senti tano, nami nikulipe kiasi cha maua na matunda utakayotaka.”

Hii maana yake ni raha na ladha halali au zilizoruhusiwa, zipatikanazo kwa njia za sheria, zinatosheleza mtu kuridhika nazo, haziachi sababu yeyote ya kutumia njia haramu.

Wewe mwenyewe waweza kufafanua taarifa-kamili zilizobakia za ono hili.

Elezo la Nne

Mwanadamu, miongoni mwa viumbe, ni sawa na mtoto dhaifu.

Nguvu zake hutokana na udhaifu wake, na pawa yake hutokana na kutofaa kwa lolote. Ni kwa sababu ya haya matarajio ya nguvu na pawa viumbe vyote vimesalimishwa kwake. Iwapo basi mwanadamu anakiri udhaifu wake na anakuwa mtumishi dhalili kwa Allah kwa njia ya sala yake, ya maneno na tendaji, iwapo anatambua kutofaa kwake kwa lolote na akaomba msaada wa Allah, hapo atakuwa katimiza wajibu wa kushukuru kwa kusalimishiwa vitu vyote kwake. Isitoshe, Allah Atamuwezesha afikie lengo lake na apate nia zake kwa njia ambayo angeachiwa ategemee uwezo wake yeye mwenyewe asingefaulu kupata hata moja ya mia yake. Mara nyingine hukosea na kuisifia nguvu bna uwezo wake yeye mwenyewe kwa kufanikisha kulipata takwa fulani ambalo amepatiwa kwa njia ya sala iliyosaliwa kwa ulimi wa silika yake.

Hebu fikiria jinsi udhaifu wa kifaranga wa kuku ulivyokuwa ni chanzo kikubwa cha pawa yake, inayomfanya mama kuku amshambulie hata simba mzima.

Au jinsi udhaifu wa ndama wa simba unamsalimisha kwake mnyama mkubwa sana kama mama simba ambaye mwenyewe aona njaa kumlisha ndama wake. Ni ajabu jinsi nguvu ya kuomba iliyomo kwenye udhaifu ilivyo kubwa, na jinsi udhihirisho wa Huruma wanayopewa viumbe wasio bahati ilivyokuwa ya ajabu! Kwa njia hiyo hiyo ambayo mtoto anayependwa hulipata lengo lake kwa kulia, au kwa kusema anachotaka, au kwa kununa, na akaweza kuwasababisha watu wakubwa wenye nguvu kumhudumia yeye. Kwa sababu ya udhaifu wake na kutokuwa na usaidizi wowote, kwa kweli, hisia za upendo na ulinzi huwaingia watu kwa ajili yake kiasi kwamba hata ishara ndogo tu ya mkono wa huyo mtoto inatosha kuwateka watu wenye pawa waje upanda wake.

Sasa, ikiwa mtoto kama huyu atakujakuwa na majivuno ya kuukana upendo na ulinzi anaoonyeshwa na aseme, kwa tuhuma za ulinzi juu yake, kuwa: “Nafanya yote haya kwa nguvu zangu mie mwenyewe”, basi atastahili kuchapwa kofi kidogo.

Halikadhalika, mtu mzima naye bila shaka atastahili adhabu iwapo ataikana Rehema ya Muumba wake imfikiayo yeye, na kuituhumu Hekima ya Allahkwa kutokuwa na shukrani kwa yale ambayo Rehema ya Kiungu imempa, asingizie mafanikio yake yoteyametokana na uwezo na akili yake mwenyewe, kama inavusema Qur'an hivi:

“28:78 Akasema: ‘Hakika nimepewa haya kwaababu ya ilimu niliyo nayo…

[Qaala innamaa uwtiytuhuu 'alaa 'ilmin 'indiy].”

Hii inaonyesha kwamba, umilikaji anaouonyesha mwanadamu humu Ulimwenguni, maendeleo yake katiika ustaarabu na teknolojia, vyote Hajavifanikisha kwa uwezo wake, juhudi, na fanaka zake mwenyewe tu. Haya yote yanatokana na udhaifu wake na kutojiweza kwake ambako huvutia msaada wa Kiungu; ufukara wake ni chanzo cha kulishwa kwake Kiungu, kutojua kwake kunafidiwa na ufunuo au kuvuviwa kwa Kiungu; mahitaji yake yanavutia upendeleo wa Kiungu. Pia ni Rehema na Upendo wa Kiungu, na Hekima ya Kiungu, lakini kamwe sio uwezo wake na ujuzi wake yeye mwenyewe, ambavyo vimempa umilikaji wa viumbe vingine vyote, na vimemwekea vitu vyote wazi avitumie. Vile vile ni Amri na Huruma ya Kiungu, ambayo peke yake ndio humfanya mwanadamu, awe mdhaifu mno hata nge asiyeona au nyoka asiyekuwa na miguu amshinde; kutuwezesha kuvaa hariri kwa kupitia kwa kiwavi na kula asali ya mdudu mwenye sumu.

Kwa kuwa hii ni kweli, Ewe mwanadmu, achilia mbali majivuno na usiiweke imani kwako mwenyewe! Bali, kiri kutofaa kwako kwa lolote na ukiri udhaifu wako Mbele ya utukufu wa Allah kwa kuomba msaada Wake, na kwa kusali na kuomba na kumbembeleza Yeye. Tangaza ufukara wako na na kutojitosheleza kwako, na onyesha kuwa wewe u mtumishi Wake wa kweli. Kisha useme hivi:

“3:173.. Lakini maneno hayo yakawazidishia imani Waislamu, wakasema:

Allah Anatutosha.Naye ni Mlinzi Mbora kabisa. [… Fakhshawhum fazaada Hum iymaan; wa qaaluw hasbunal-Lwaahu wa ni'imal-wakiyl.]”

Na kwa kusema hivyo, upande juu madarajamengi.

Kamwe usiseme hivi:

“Mie sio chochote; nina thamani gani hata Muumbaji Mwenye Hekima zote aniwekee viumbe vyote viwe chini yangu na Anitake shukurani za kilimwengu?”

Ni kweli wewe sio chochote kwa mintaarafu ya mwili wako, lakini kuhusu wajibu wako au cheo chako, wewe ni mtazamaji mwangalifu wa ulimwengu huu mzuri, ni ulimi msemaji mzuri wa viumbe unaotangaza Hekima ya Kiungu, ni mwanafunzi mwangalifu wa kitabu cha uumbaji, msimamizi mtamanifu wa viumbe ambavyo hutukuza sifa za Allah, na ni bwana mheshimiwa wa viumbe vinavyoabudu.

Wewe ndiwe, Ewe mwanadamu, hakika ni kipunje kidogo kisicho maana; kiumbe fukara na mnyama dhaifu kwa muujibu wa hulka yako ya kimwili na roho iliyozaliwa kimwili, unahesabiwa, na kwa hiyo unasombwa na mawimbi makubwaya uumbaji. Lakini ukikamilishwa kwa njia ya nuru ya imani, ambayo ina mn'garo wa upendo wa Kiungu, kwa kwa njia ya mafunzo ya Kiislamu, utauona ufalmefalme katika kuwa kwako mtumwa, uelewekaji katika umaalumu wako, dunia nzima katika upweke wako mdogo, na cheo kikubwa sana katika kuwa kwako sio chochote. Pia ile milki ya usimamizi wako wa viumbe vingine vyote itakuwapana sana kiasi kwamba wewe unaweza kusema hivi:

“Mola wangu Mwenye Huruma kanitengezea dunia hii iwe makazi yangu.

Amenipa jua na mwezi kama taa, majira ya vuli kama shada la mawaridi, majira ya kiangazi kama karamu ya upendeleo, na wanyama kama watumishi watiifu. Ameiweka mimea pia chini yangu, kama mapambo na vyakula kwa nyumba yangu.”

Kwa kumalizia, iendapo utaitii nafsi yako inayoamrisha maovu na Shetani, utaanguka hadi uwe chini kuliko wote walio chini. Lakini endapo utaufuataukweli na Qur'an, utapanda hadi ufike juu kuliko wote wlio juu na uwe mfano mzuri kuliko yote wa uumbaji.

Elezo la Tano

Mwanadamu kaletwa humu duniani kama mgeni mwenye wajibu maalumu, na aliyejaaliwa uwezo muhimu. Amepewa kazi mahsusi kufuatana na huu uwezo, na amehimizwa sanaazitekeleze kazi zote hizo na akaonywa sana asiache kuzifanya kazi hizo. Ili kuifanya hiyo siri ya kuwa “mfano mzuri kuliko yote ya uumbaji” ieleweke, hapa chini tutatoa muhutasari wa ibada na kazi anazotakiwa mwanadamu kuzifanya, ambazo tulishazieleza katika kitabu kingine.

Ibada za mwanadamu zimegawanyika aina mbili. Moja ni ile ambayo inaonyeshwa bila kutajwa na inayohusu kutafakari. Nyingine ni ile ya kusali wazi wazi inayofanywa kwa kuomba moja kwa moja mbele ya Allah.

Aina ya kwanza: ni kwamba, mwanadamu hushahidilia kitiifu Ufalme wa Umola Wake juu ya viumbe, na hutazama kwa mshangao kazi za Uzuri na Ukamilifu Wake.

Kisha huwaonyesha viumbe wenziwe kazi za sanaa za mapambo na fumbo ambazo zinadhihirisha Majina matakatifu ya Kiungu. Pia hupima kwa vipimo vya uonajivito vya Majina na Mola, ambayo kila moja ni hazina ya kiroho iliyofichika, na huvitathmini kwautambuzi wa shukurani wa moyoni.Kisha hufanya uchunguzi wa karibu wa kurasa za uumbaji, karatasi za mbingu ardhi, ambazo kila moja ni barua ya Pawa ya Kiungu, na huzitafakarikwa matamanio makubwa.

Baadae, kadiri anavyotazama kwa mshangao na matamanio hizo nakshi na stadi za uumbaji, hutamani sana kumjua Muumbaji wao Mzuri na anatamani sana ahudhurie mbele Yake, ambako anataraji atapokewa katika ridhaa Yake.

Aina ya pili: ni kwamba mwanadamu hugeuka kuelekea kwa Muumbaji wake Mtukufu, Ambaye Anataka Ajulikane kwa njia ya miujiza ya sanaa Zake.

Mwanadamu huyo hujitua mzigo Kwake kwa imanithabiti na hujaribu kupata Ujuzi kutoka Kwake.

Kisha hutambua kwamba Mola Mwenye Huruma hutaka Yeye Apendwe kupitia kwenye matunda mazuri ya Huruma Zake. Kisha na yeye hujifanywa apendwe naYeye kwa kukithirisha upendo wake Kwake.

Pia huona kwmbaMpaji Mkarimu humlisha yeye kwa mafao ya upendeleo ya kimwili na kiroho yaliyokuwa mazuri kuliko yote. Humlipa Yeye kwa kumshukuru na kumsifu, kwa njia ya kazi zake zote, matendo, mfumo wa maisha, na ikiwezekana kwa hisia zake zote na vipaji vyote.

Kisha huona kuwa Mola wa Uzuri na utukufu Anajidhihirisha Mwenyewe Katika viyoo vya viumbe, na hutangaza Utukufu, na Ufalme Wake na Uzuri Wake.

Kwa hiyo hujibu kwa kusema : “Allah ni Mkuu kuliko wote, Utukufu uwe kwa Allah”, Na husujudu mbele Yake kwa mshangao na upendo.

Tena hutambua kuwa moja ya Utajiri wa Kipekee unaonyesha mali na hazina Zake zisizokuwa na kikomo kwa ukarimu mkubwa sana.Kujibu hayo basi,humtukuzana kumsifu Yeye, na kwa kudhihirisha mahitaji yake, humuomba Yeye ampe mapendeleo Yake.

Ndipo huona kwamba Muumbaji Mtukufu Aliipanga ardhi kama maonyesho ambamo anaonyesha kazi Zake zote zisizo mfano. Kwa hivyo hata yeye huzithamini, na husema hivi:”Maajabu yaliyoje haya Ambayo Allah Aliyapendana Akayaumba!”, huthibitisha uzuri wake na kusema: “Allah Azibariki!”, huonyesha mshangao wake na kusema: “Utukufu uwe kwa Allah!”, na huonyesha upenzi wake kwa kusema:”Allaha ni Mkuu kuliko wote!”.

Pia huona kwamba Yeye Aliye wa Pekee hudhihirisha Upweke Wake katika Uumbaji Wake wote kwa njia ya ishara Zake maalum na sharia Zake maalum, na pia mihuri na lakiri Zake zisizoigika ambayo Yeye kaiweka kwenye viumbe vyake vyote. Huandika juu ya kila kitu ishara za Upweke Wake, na hupandisha duniani kote bendera Yake ya Umoja. Hivyo huwa akitangaza UmolaWake. Kwa hili, mwanadamu hulijibu kwa kuamini, kukubali, kukirikwa, na kushuhudia kwa, Umoja Wake, kumpenda, na kumwabudu kiaminifu.

Kwa aina zote hizo za kumwabudu na kutakari mwanadamu huweza akapata uanadamu wa kweli.Anaweza kuonyesha kuwa yeye ni mfano mzuri kuliko yote ya uumbaji, na kupitia rehema ya imani, aweze kuwa khalifa mwaminifu wa Allah humu duniani.

Sasa basi ewe mwanadamu usiyejali, unayedidimia chini sana kuliko walivyo walioko chini kwa kutumia vibaya radhi yake, ingaw ameumbwakama mfano mzuri kuliko yote ya uumbaji, nisikilize mimi!Ili uweze kuonekana ubaya wa sura ya ardhi ambayo hugeukia matamanio na uchu, na kinyume cha hivyo, uzuri wa ajabu wa sura nyingine inayogeukia Maisha ya Akhera, tazama “Jedwali” zifuatazo hapa chini:

Jedwali ya Kwanza inaonyesha hali halisi ya dunia ya wasiojali:

Usinialike mimi nije duniani,

Nimekuja huko, na nikakuta mambo ya uovu na ya kupita tu.

Kutojalia ni pazia linaloficha Nuru ya Ukweli.

Vitu vyote, Vilivyoumbwa vyote, ni vya kufa (mortal), na vimejaa madhara.

Kuishi, hakika huwa ninakuvaa' lakini hugeuka kukawa kutokuishi, kulikojaa mikosi.

Ama kuhusu maisha, nimepata uzoefu wake, lakini nimeonja mateso mengi mno.

Akili ni njia ya malipo yanayostahilika; umilele ni chanzo cha maumivu.

Maisha yamepitia kwenye fikra zisizo maana, wazo la ukamilifu halikuwahi kuwa.

Matendo ni ya kuonyesha tu, na matarajio huishia kwenye ukatishaji tamaa.

Daima kukutanishwa huishia katika kutenganishwa, tiba ni sawa na maradhi.

Kila pahala pako gizani, marafiki wameachwa peke yao bila ulinzi.

Sauti za wanadamu ni vilio vya vifo; viumbe hai vyaishia kuteketezwa.

Sayansi zinageuzwa kuwa nadharia, falsafa inatumiwa vibaya na imejaa dosari.

Raha, kwa hakika, ni majonzi; kuishi kumeambatana na kutokuishi.

Jedwali ya Pili inaonyesha hali halisi ya watu wa mwongozo:

Nimempata Mpendwa wa Kweli, na Kutojali kumetoweka, na nuru ya Ukweli imechomoza tena, Kuishi ni ushahidi wa Uungu na maisha ni kiyoo kimrudishacho Allah Akili ni ufunguo wa hazina nyingi; mpito ni mlangowa umilele.

Cheche ya kujifanikisha imekufa; lakini jua la uzuri daima linang'aa.

Kufa hupelekea kukutana tena; majonzi, kwa yakini, ni furaha.

Maisha ni matendo safi; Umilele ni maisha safi.

Giza ni utando mwembamba unaoigubika nuru; kifo ni mwanzo wa maisha ya kweli; Vitu vyote ni marafiki waaminifu; sauti zote ni utukuzo wa Allah.

Kila punje katika uumbaji inamtukuza na kumsifu Allah.

Mahitaji ni hazina ya utajiri; na katika kutowezakujisaidiaiko pawa kamilifu.

Iwapo umemgundua Allah; ujuwe kuwa vitu vyote vinesalimishwa kwako.

Ikiwa wewe u mtumwa wa Mmiliki wa viumbe vyote; basi mali Yake yote ni yako.

Endapo wewe unajiona na unadaiumiliki wako binafsi; Ujuwe hiyo ni majaribio yasiyo na mwisho na madhila.

Na pia ni mateso yasiyo kifani, ambayo haiwezekani kuyahimili.

Ukiwa wewe ni mtumwa wa Allah kweli; utapata furaha isiyo kifani.

Katika kuwa hivyo utapata zawadi zisizo mwisho; na huleta raha isiyo kifani.

Utukufu uwe Kwako! Hatuna Ujuzi ila uliotufundisha Wewe. Bila shaka Wewe ni Mwingi wa Ujuzi wa Vyote, na Rehema zote.

Ewe Mola wangu! Ipumzishe akili yangu, na ilegeze kazi yangu, na fungua fundo Kutoka ulimini kwangu, ili waelewe hotuba yangu.

Ewe Allah! Mpe Amani na Baraka Muhammad, asili yake nadhifu na ya kipekee, ambaye ni nuru inayoumbua siri zote, udhihirisho wa nuru, nukta ya kati ambako udhihirisho wa Utukufu wa Allah umeanzia, nukta ambapo mzunguko wa dunia ya Mwenye Hisani (Grace) na Mwenye Uzuri (Beauty) huanzia. Ewe Allah, kwa siri ya yeye katikakuhusiana na Wewe, na kwa kule kusafiri kukuelekea Wewe, niepushie woga wangu, nilinde nisianguke, punguza huzuni zangu na nitakase nitokane na matamanio. Uwe nami, uniondoshe kutoka kwangu mie mwenyewe nije Kwako, nipendelee nisijifikirie mimi mwenyewe, usiniache nikiwa ninajijali mno mimi mwenyewe, nimegubikwa na hisia zangu, nifungulie kila siri. Ewe Mwenye kuishi Milele na Unayejiendeleza Wewe Mwenyewe! Nirehemu mimi na warehemu wenzi wangu na warehemu waumini wote na watu wote wa Qur'an.

Aamin. Ewe Mwenye Huruma kuliko wote wenye huruma, Ewe Mwenye Ukarimu kuliko wakarimu wote!

Hatima (conclusion) ya wito wao itakuwa hivi:

“Sifa zote Anastahili Allah, Mola wa limwengu zote.”


Hiç yorum yok:

Yorum Gönder