24 Ocak 2011 Pazartesi

MANENOMAFUPI

Kutoka Katika Mkusanyiko

wa Risala za Nuru

MANENOMAFUPI

Kilichotungwa na

SAID NURSI

Kutoka Katika Mkusanyiko

wa Risala za Nuru

KÜÇÜK SÖZLER

Suwahili Lisanına Tercümesi

KWA JINA LAALLAHMWINGI WA REHEMA NA HURUMA

Na sie huomba msaada kutoka Kwak. Shukrani zote Anastahiki Allah, Mola wa limwengu zote; na sala na amani ziwe juuya Bwana wetu Muhammad, na kwa watu wote wa familia yake na maswahaba wake. [Wa bihiy nasta'iyn, Al-hamdu lil-Laahi Rabbil-l'aalamiyn, wasw-swalaatu was-salaamu 'alaaSayyidinaa Muhammadin wa 'alaa aalihiy wa swahbihiy ajma'iyn.]

Ndugu! Ulitaka kusikia maneno machache ya nasaha kutoka kwangu. Kwa hivyo, pamoja na kuiusia roho yangu, sikiliza ewe ndugu maneno machache ya ukweliyaliyomo kwenye mafumbo ambayo, kwa kuwa wewe ni askari, yataelezwa kwa lugha ya kijeshi. Nafikiria kwamba roho yangu inahitaji nasaha kuliko yeyote, na wakati mmoja niliinasihi roho yangu mwenyewe kwa Maneno Manane yaliyofunuliwa kwa aya nane za Qur'an.Hivi sasa nitainasihi roho yangu kwa Maneno haya haya, lakini kwa kifupi, na katika lugha ya watu wa kawaida. Kila anayetaka kusikiliza asikilize pamojana mie.


NENO LA KWANZA

Thamani ya Bismil-Laahi

Bismil-Laahi, yaani kwa Jina la Allah, ni mwanzo wa vitu vyote vizuri. Kwa hivyo na sisi pia tutaanza na hiyo. Jua, ewe roho yangu, maneno haya mabarikiwa ni alama ya Uislamu, na husomwa daima na kila kiumbe kwa kutumia ndimi zao za silika. Iwapo unataka kutambua jinsi Bismil-Laahi ilivyokuwa ni chanzo kisichomalizika cha nguvu na baraka, basi sikiliza fumbo lifuatalo:

Kwa mgeni anayesafiri katika majangwa ya Arabuni, ni lazima kuchukua jina la kiongozi wa kabila na awe chini ya ulinzi wake. Njia hiyo tu ndio inaweza kumwokoa na uovu wa wanyang'anyi na ataweza kutimiza mahitaji ya safari yake.Vinginevyo, akisafiri peke yake, dhamiri yake ya kufanya hivyo itapotea, kwa sababu ya maadui na mahitaji ambayo ni lazima ayakabili.

Hapo zamani watu wawili walifunga safari ya jangwani ya aina hii. Mmoja alikuwa na hulka ya kidhalili, mwingine alikuwa mwenye kiburi. Msafiri dhalili alichukua jina la kiongozi wa kabila, na huyu mwenye kiburi hakuchukua.Yule wa kwanza alisafiri salama usalmini kila pahala.Kila alipokutana na mnyang'anyi, alikuwa akisema:” Mimi nasafiri kwa jina la kiongozi fulani”, na mnyang'anyi huenda zake bila kumdhuru yule msafiri. Alikuwa akipewa heshima katika kila hema aliloingia kwa sababu ya hilo jina.

Kinyume cha hivi, huyu mwenye kiburi alikumbwa na maafa yasio kifani katika safari yake yote. Alikuwa akitetemeka kwa sababu ya woga na akalazimika afanye kazi ngumu na aombeombe kwa kila hitajio lake. Akawa mtu wa chini na wa kuaibisha.

Ewe roho mwenye kiburi! Wewe ndiwe huyu msafiri, na dunia hii ndio jangwa. Udhaifu wako na ufukara hauna mipaka. Maadui na madhila hayana hesabu. Ikiwa hivyo ndivyo, basi liite Jina la Mmilikaji wa Milele na Mtawala wa Kudumu Daima wa dunia yote hii, yaani jangwa. Ni kwa njia hiyo tu ndio utaweza kuepuka kulazimika kuombaomba kwa kila mtu, na kutetemeka kwa wogawa kila tukio.

Haya maneno Bismil-Laah ni hazina iliyobarikiwa mno kiasi kwamba, kwa kukufungamanisha wewe na Uweza usio upeo na Rehema isiyo kifani ya Mwenye Enzi Zote na Mwenye Rehema, huugeuza udhaifu wako wa kupindukia na ufukara wako, uwe muwakilishi asikizwaye kuliko wote mbele ya Mahkama Yake iliyotukuka. Kila anayetamka Bismil-Laah kisha akatenda jambo kwa Jina la Allah, ni sawa na mtu anayejiunga na jeshi kisha akatenda jambo kwa jina la nchi, asimuogope yeyote, hufanya vitu vyote kwa jina la sharia na la nchi, na huku akikazana dhidi ya kila tatizo Hapo mwanzo tuliona kuwa kila kiumbe husoma Bismil-Laah kwa njia yake ya maumbile yake. Hii huwaje?

Kwa mfano: mgeni mpweke akifika jijini anaweza kuiamuru halaiki ya watu kwa pamoja pahala fulani kufanya kazi fulani. Endapo amri hiyo wataitii, unaweza kuwa na hakika kuwa mtu huyo hayafanyi yale kwa matakwa yake mwenyewe au kwa kutumia nguvu zake mwenyewe, bali kwa madaraka ya mtawala wa jimbo lile.

Kwa njia hiyo hiyo, kila kiumbe kilichoko hufanya mambo kwa Jina la Allah, Mwenye Nguvu zote. Mbegu na punje za nafaka.ingawa ni ndogondogo sana, zinabeba miti mikubwa sana vichwani mwao, na hunyanyua mizigo mizito kama milima. Kila mti husema Bismil-Laah na huijaza mikono yake kwa matunda kutoka kwenye hazina ya Rehema, na hutupa sie kwenye sahani. Kila bustani pia husema Bismil-Laah.

Chungu cha kupikia kutoka katika jiko la Uweza wa Allah, ndimo ambamo huandaliwa vyakula vingi tofauti vizuri. Wanyama wote waliobarikiwa kama ng'ombe, ngamia, kondoo, na mbuzi husema Bismil-Laah, na huwa chemchemi za maziwakutoka kwenye uwingi wa Rehema, na hutupa sisi kwa Jina la Mtoaji, mlo mwororo na msafi kama maji ya uhai. Kila mmea, kila tawi la majani, kila mzizi na shina, vyote pia husema Bismil-Laah. Mizizi na nyuzi, zilizo nyororo kama hariri, za mimea yote, miti, na majani, husema “Kwa Jina la Allah”, na kutoboa na kupenya kwa kupita ndani ya mawe magumu na ardhi, huku ikitaja Jina la Allah, Jina la Mwenye Rehema, na ndipo kila kitu kinamilikishwa kwao au kinakuwa chini yao.

Kutanda kwa matawi ya mti angani, kupenya kusikozuilika kwa mizizi yake kati kati ya mawe magumu na ardhi, kuota na kuchipuka kwake chini ya ardhi, majani yake laini ya kijani kibichiyakiwa yamehodhi unyevunyevu juu ya kuweko joto kali - mambo haya yote yanaunda ukweli ambao ni kama pigo alilopigiwa mtu mwenye imani asilia. Yanadukua kidole ndani ya jicho lake lisiloona na kusema: “Ule ukali na lile joto ambao uwezo wake wewe uliutegemea sana, unalazimika kufanya kazi kwa muujibu wa Amri za Allah.” Ndio maana kila uzi laini wa mzizi wa mmea, kama ilivyokuwa ile fimbo ya Musa, unatii amri iliyomo katika aya ifuatayo:

2:60Na Musa alipoomba maji kwa ajili ya watu wake, nasi Tukasema: 'Ewe Musa, lipige jiwe kwa fimbo yako;' Mara zikabubujika humo chemchem kumi na mbili..

ndipo inapenyeza ndani ya jiwe hilo. Kila jani jembamba kama karatasi, kama moja ya viungo vya Ibrahim, amani iwe juu yake, husoma aya hii:

21:69 Tukasema: 'Ewe moto! Kuwa baridi na salamajuu ya Ibrahim.

ili kulishinda lile joto kali.

Sasa kwa kuwa vitu vyote husema kindanindani bismil-Laah na huwasilisha kwetu neema za Mungu kwa Jina Lake Mungu, nasi pia hatuna budi tuseme Bismil-Laah na tutoe kwa Jina la Mungu na tuchukue kwa Jina Lake. Tusipokee chochote kutoka kwa wale watu wasiojali na wasiotoa kwa Jina la Mungu.

Suali

Huwa tunawalipa watu kwa kile wanachotuletea, ingawa wao ni 'wachukuzi' tu 'wa sahani'.Sasa je, Allah, Ambaye ndiye Mmiliki halisi wa mali zote. Anatudai nini?

Jibu: Yule Mpaji wa neema adimu na bidhaa tunazozifaidi, hututaka tumlipe mambo matatu tu:tumkumbuke, tumshukuru, natutafakari.

Basi kusema Bismil-Laah mwanzo wa kila jambo ni namna ya kumshukuru; na kusema Alhamdu lil-Laah (Utukufu na shukrani zimwendee Allah) mwisho wa kila jambo ni namna ya kumshukuru. Amma kutafakari: hii ni kuwa daima tunajali na kufikiri juu ya neema adimu na za ajabu ambazo sisi huzipokea kama miujiza ya Uweza wa Yeye Anayestahiki Kutegemewa Milele na wote na kama zawadi kutoka kwa Yeye Mwenye Rehema Zake. Ungediriki kuubusu mkono wa mtu aliyekuletea zawadi adimu kutoka kwa mfalme, bila kutambua kabisa nani hasa aliyekuletea hiyo zawadi, utakuwa ujinga ulioje huo! Kuwasifu na kuwaenzi wale wanaoelekea kuwa ndio wapaji, wakati unasahau yule Mpaji Halisi wa neema, ni ujinga mbaya maraelfu na zaidi.

Ewe roho! Endapo unataka kuepuka ujinga kama huo, toa kwa Jina la Allah na pokea kwa Jina la Allah. Hadi mwisho kabisa, tenda jambo kwa Jina la Allah. Hii itakutosheleza.


ONDÖRDÜNCÜ LEMANIN İKINCİ MAKAMI

MAKAZI YA PILI YA MMULIKO WA KUMI NA NNE

Linachofuatia sasa ni muhimu hapa. Linaelezea siri sita kati ya siri nyingi sana za hiyo Bismil-Laah, yaani Kwa Jina la Allah, Mwingi wa Rehema na Upole.

ANGALIA: Nuru kali kutoka katika Bismil-Laah kuhusu Urehemevu wa Allah ilinigusa Akili yangu iliyokuwa na giza, kutoka mbali. Nilitaka niihifadhi kwa ajili yangu mie mwenyewekwa njia ya maandishi, na kuufuatilia na kukusanya nuru yake katika sehemu ishirini mpaka thalathini za “Siri”. Hamadi, sikuweza kufanya hivi kwa sasa; na hizo ishirini hadi thalathini zimepunguzwa hadi kufikia sita.

Niandikapo “Ewe mwanadamu” ninajikusudia mimi mwenyewe. Hata hivyo, ingawa mafunzo haya yananilenga mahususi mimi mwenyewe, ninayaita “Makazi ya Pili ya Mmuliko wa Kumi naNne, kwa masahihisho ya ndugu zangu waangalifu.Natarajia yatawanufaishawale ambao nina mahusiano nao ya kiroho na ambao mioyo yao ni mierevu kuliko wangu. Hoja hapa inaugusa moyo (heart) hasa kuliko akili, inataka kuuhoji moyo kuliko kuutazamaushahidi wa wazi.

KWA JINA LAALLAHMWINGI WA REHEMA NA HURUMA

“27:29 (Yule Malkia akawakusanya mawairi wake) akasema: 'Enyi wakuu (wa Baraza)! Akika nimeletewa barua tukufu: 30: 'Imetoka kwa Suleimani, nayo ni:Kwa Jina la Allah, Mwingi wa Rehema na Huruma.':

Katika Makazi haya zitaelezwa “Siri” sita.

Siri ya kwanza

Mtazamo mmoja wa “Kwa Jina la Allah, Mwingi wa Rehema na Huruma” niliuona kwa njia ifuatayo:

Juu ya uso wa ulimwengu, na wa ardhi, na wa mwanadamu, imepigwa mihuri mitatu ya Umola, mmoja ndani ya mwingine, na kila mmoja unachukua muundo (pattern) wa mingine.

Kwanza: Mhuri mkuu wa Uungu, unaodhihirika katika kujisaidia wenyewe kwa wenyewe, kushirikiana, kwa vitu vyote ulimwenguni, kuungamanana kurejezeana kwao.Na rejea ya huu ni “Kwa Jina la Allah”.

Pili:Mhuri mkuu wa Urehemevu wa Kiungu unaodhihirika katika kufana kwa umbile, mpangilio wa kinidhamu na wa kuowana, wema na hurumakatika kuondoka, kuzalisha na kudhibiti mimea na na wanyama juu ya uso wa ardhi. Na rejea ya huu ni “Kwa Jina la Allah Mwingi wa Rehema”.

Tatu:Mhuri adhimu wa Uhuruma wa Kiungu Unaodhihirika katika undani wa uzuri wa Kimungu, marekebisho ya taratibu ya upole wa Uungu, kusambaa kwa nuru ya Uhuruma wa Kiungu kwenye uso wa nafsi ya kuelewa kwa mwanadamu.Na rejea ya huu ni “Kwa Jina la Allah, Mwingi wa Rehema na Huruma.

Kwa hivyo Bismil-Laah ni maelezo ya mihuri hiyo mitatu ya Umoja au Upweke wa Umungu, ambao unachora msitari unaoangaa katika ukurasa wa ulimwengu, mkao imara, na uzi wa dhahabu.Inayodhihirishwa kutoka kwenye mtu wa hapo juu, ncha ya “Kwa Jina la Allah, Mwingi wa Rehema na Huruma” huegemea kwa yule ambaye ni mfano mdogo wa ulimwengu na tunda lake.Na Bismil-Laah inaunganisha dunia na Kiri cha Enzi cha Uungu na ni ngazi ya mtu kupanda hadi kule.

Siri ya Pili

Umoja au Upweke wa Uungu unadhihirika katika uzaanaji usio kifani wa viumbe binafsi.Ili tusiweze kuzichoshwa akili zetu kwa yote haya mara moja, Qur'an, ikiwa ni muujiza wa kudhihirisha mambo, inakariri kila mara udhahiri wa Uungu Mpweke ndani ya Uungu Mmoja. Kwa mfano, jua linajumuisha vitu kadha wa kadha katika mwanga wake. Lakini kulishika jua katika akili ya mtukwa ujumla wa mwanga wake wote kutahitaji uwezo wa kimawazo na wa kuona wa kiwango kikubwa sana. Kwa hiyo, ili jua lisisahaulike, vitu vyote vinavyong'ara hurudisha silika za jua, mwanga na joto lake, kwa uwezo wake wote, na hivyo linadhihirisha kule kuwa kwake jua. Na huku kudhihirisha silka za jua nako kunarudishwa kwa vilehizo silika, mwanga na joto la jua pamoja na mchanganyiko wa rangi uliyomo ndani yake, hujumuisha vitu ambavyo jua linavikabili.

Halikadhalika - kwa Allah ndiko kuliko mifano ya juu kuliko kokote:dosari zozote xisisababishwe na mifano yetu dhaifu -kama ambavyo Upweke wa Allah nakule kuwa Kwake Mtegemewa wa Milele vimedhihiri, pamoja na Majina yote ya Kiungu, katika kila kitu, kwenye viumbe mahususi vyenye hisia na hususani kwenye nafsi ya ukiyoo ya mwanadamu, basi ndivyo lilivyo kila moja ya Majina ya Kiungu yanayohusiana na viumbe, kupitia katika Umoja wa Uungu, kwa kujumuisha viumbe vyote. Kwa hivyo, Qur'an tena na tena inatukumbusha muhuri wa Upweke wa Uungu ndani ya Umoja wa Uungu - zisije akili zikachushwa na Umoja na mioyo ikawa haijali Kiini Kisafi na Kitakatifu.Na ni Kwa Jina la Allah, Mwingi wa Rehema na Huruma, inayoonyesha dalili tatu muhimu za muhuri wa Umoja wa Uungu.

Siri ya Tatu

Kinachosababisha ulimwengu usio mipaka huu kufurahi dhahiri ni Rehema ya Uungu.Kinachoupa ugiza ile cheche ya mwanga na maisha au uhai, bila shaka, ni Huruma ya Uungu. Pia yaelekea ni hiyo Rehema ya Uungu inayolea na kukuza viumbe vinavyohangaika katika uhitaji wake usio mwisho. Tena, ni hiyo Rehema ya Uungu ambayo wazi wazi inasababisha ulimwengu wote kumuelekea mwanadamu, kwa njkia ileile ambavyo mti pamoja na sehem,u zake zote huelekezwa kwenye matunda yake, na kuharakisha kwenda kumsaidia mwanadamu. Kinachojaza na kuangaza ile anga isiyo mipaka, na dunia ambayo ingekuwa tupu na isiyopendeza, kuifanya ifurahi, bila shaka ni hiyo Rehema ya Uungu. Na ni Rehema ya Uungu inayomteulia mwanadamu mwenye maisha ya muda mfupi umilele na cheo cha kiumbe huyo kwa anuani na upenzi wa Mmoja wa Milele kabla na baada ya milele.

Ewe mwanadamu! Kwa kuwa Rehema za Kiungu ni ukweli wenye nguvu sana, na ambao unashawishi sana, wa wastani sana, msaidizi sana, unaostahili mapenzi sana, sema:Kwa Jina la Allah, Mwingi wa Rehema na Huruma.Ung'ang'anie ukweli huu na uepushwe na ukiwa mtupu na adha ya uhitaji usiokuwa na mwisho. Jisogeze kwa Mfalme Mkuu wa Milele kabla na baada ya milele, na uwe wewe mkusudiwa, mpendwa na mpenzi wa Mfalme Mkuu huyo.

Kule kuwepo vitu vya aina nyingi ulimwenguni vilivyokusanyika kumzunguka mwanadamu kwa makusudi na kwa kuona mbele, na vinaharakisha kumkidhi mahitaji yake yote kwa mpangilio na uzuri mkamilifu kabisa - bila shaka hali hii inahitaji maelezo. Ama kila kiyu ulimwenguni kinamtambua mwanadamu mwanadamu na hivyo humkimbilia kiutii kwenda kumsaidia - ambayo haingii akilini, na haiwezekani - au kiumbe ambacho hakina nguvu kabisa kama alivyo mwanadamu kina nguvu ya mwenye nguvu kuliko wote, ufalme mkubwa, au msaada kwa mwanadamu humfikia kwa njia ya Kumtambua Mmoja Mwenye Nguvu Kabisa, nyuma ya pazia ya ulimwengu unaoonekana.Kwa maneno mengine, si kama vitu mbalimbali ulimwenguni vinamtambua mwanadamu, bali kufanya kwao hivyo ni ushahidi kuwa Mmoja Mwingiwa Kila Kitu, anaelewana naye na anamtambua.

Ewe mwanadamu! Zindukana!Ingewezekanaje yule Mmoja Mwenye Utukufu Wote, anayesababisha kila aina ya vitu vikuelekee wewe, vikikunyooshea mikono, vikitoa msaada na kusema: “Tumekuja!” wakati una shida, yawezekanaje kuwa Yeye hakufahamu, kuwa Yeye hakuoni, kuwa Yeye hana habari na wewe? Yeye hukufundisha wewe kuwa Yeye huwa anakujua wewe kupitia kwenye Rehema Yake. Basi na wewe mjue Yeye na uonyeshe kwa heshima na taadhima kuwa unamjua. Elewa barabara kinachousalimisha ulimwengu mkubwa kwa kiumbe kama wewe, mdogo, wa muda mfupi, mdhaifu kabisa, usiye nguvu na muhitaji, na akaufanya ukuhudumie wewe, ni ukweli wa Rehema ya Uungu, yenye Hekima, Uweza, Ujuzi na Nguvu.

Bila shaka, Rehema kama hiyo huhitaji shukrani yote na ya dhati, na utii mkubwa na wa kweli kabisa. Kwa hivyo sema Kwa Jina la Allah, Mwingi wa Rehema na Huruma, ambayo inadhihirisha na inafafanua shukrani hiyo ya dhati na utii wa kiaminifu. Ifanye iwe ni kukubalika kwako katika Rehema Yake, kiingiliaji kati na wakili katika Mahakam ya Mwenye Rehema Zote.

Kuwepo na udhati wa Rehema ya Uungu ni dhahiri kabisa kama lilivyo jua. Kama ambavyo nakshi za katikati za zulia la ukutani hufumwa kwa kuleta pamoja katikati nyuzi za kushoto kwenda kulia na juu kwenda chini, ndivyo zile nyuzi angavu zitokazo katika kudhihirika kwa Majina ya Uungu elfu na moja kwenye ulimwengu mkubwa, zinavyofuma lakiri ya huruma, mshono wa upole mkubwa, muundo wa uzuri ndani ya muhuri wa Rehema, kiasi kwamba hukandamizwa akilini kwa mng'aro zaidi kuliko jua.

Mwenye Neema na Rehema Zote, Anayelisalimisha jua na mwezi, elementi na madini, mimea na wanyama, kama nyuzi za kulia na juu za nakshi iliyofumwa kwa mwanga wa Majina Yake elfu na moja, kwa ajili ya huduma ya maisha, amaye anadhihirisha Huruma Yake katika kujitolea-muhanga, utamu wa kipekee wa huruma, wa umama katika mimea na wanyama; Anayesalimisha uhai wote wa viumbe vyenye uhai kwa mwanadamu na kwa hivyo anadhihirisha umuhimu wa mwanadamu, kuwa kwake mfumo mbora na mzuri kuliko vyote wa kutoka kwa Mola Mwenye Uuungu, na kwa hiyo anadhihirishamng'aro wa Rehema Yake ambao Mmoja anao, mbele ya kutokuwa Kwake na mahitaji yeyote, alifanya Rehema Yake iwe kiingilia kati kinachokubalika kwa viumbe Vyake vyenye hisia na kwa mwanadamu.

Iwapo wewe u mwanadamu kweli, sema ewe mwanadamu: Kwa Jina la Allah, Mwingi wa Rehema na Huruma. Kitafute mpaka ukipate kile kiingilia kati. Bila shaka ni ile Rehema ya Uungu inayoleta uhai, inayolea na inayodhibiti mamia na maelfu ya mimea na wanyama duniani humu, bila kusahau hata kimoja kati yao, wala kuvichangaya, bali kukikuza kila kimoja kwa wakati muafaka kabisa, kwa mpangilio mkamilifu, hekima na uzuri, na kukandamiza juu ya sura yote ya dunia hii muhuri wa Upweke wa Uungu. Kama ambavyo kuwepo kwa Rehema ya Uungu ni kweli kama kuwepo kwa viumbe duniani, ndivyo pia kila kimoja ya hivyo viumbe vilivyopo kama ushahidi wa ukweli wake kama idadi yake.

Kama muhuri wa Rehema na Upweke wa Uunguunavyokandamizwa juu ya dunia hii, pia ndivyo unavyokandamizwa juu ya sura ya nafsi ya mwanadamu. Na Mhuri wa Huruma uliokandamizwa juu yake sio kidogo kuliko ile Huruma na Rehema iliyotiwa muhurijuu ya sura ya ulimwengu mpana. Dhahiri mwanadamu ana nafsi imara iliyokaa katikati ya mfumo, mazingatio ya Majina elfu moja na moja ya Uungu.

Ewe mwanadamu! Yawaje kwamba Yule Ambaye anakupa wewe sura hiina anakandamiza juu yake muhuri wa Rehema na Lakiri ya Upweke, vipi akuwache wewe kivyako, akuone huna maana, asijali matendo yako, na hivyo kuvifanya viumbe vyote vilivyoelekezwa kwako, viwe visivyofaana bure, kuufanya mti wa kuumba uwe hauna thamani na wenye kuoza na matunda yaliyooza? Atasababisha Rehema Yake ikataliwe wakati Rehema hiyo ni dhahiri kama jua, na Hekima Yake, ambayo ni angavu kama mwanga, na kila kimoja hakiwezi kutiliwa mashaka yeyote, wala hakina dosari yeyote? Allah apishe mbali fikra kama hiyo!

Ewe mwanadamu! Jua kuwa ipo njia ya kupanda kukifikia kiti cha enzi cha Rehema ya Uungu, na njia hiyo ni: Kwa Jina la Allah, Mwingi wa Rehema Huruma.

Hebu zingatia kipimo cha umuhimu wake kwa kutazama mwanzo wa milango ya Qur'an, ambayo ni muujiza wa madhihirisho, mwanzoni mwa vitabu vyote vya maana, mwanzoni mwa matendo yote mema.Hoja ya wazi pia ya kuuelezea ukubwa wa Kwa Jina la Allah,Mwingi wa Rehema na Huruma, ukubwa ambao Anaujua Yeye, ni usemi wa Imam Shafi'i, mmoja wa wanazuoni wa msitari wa mbele sana, radhi la Allah imwendee:

“Ingawa Kwa Jina la Allah, Mwingi wa Rehema na Huruma ni aya moja tu, imefunuliwa mara 114 katika Qur'an.”

Siri ya Nne

Umoja wa Uungu unadhihirika katika uwingi usio kifani (wa viumbe ambavyo vinatofautiana kila kimoja ulimwenguni):kusema mbele yake, “Wewe tu Ndiye tunayekuabudu” haiwezi kututosha kwa sababu akili zetu hutangatanga (mbali na Ukweli). Itahitaji moyo mkubwa kama duniakumwona Yeye katika Upweke Wake nyuma ya Umoja ndani ya jumla ya vitu tofauti, kisha useme: “Wewe tu Ndiye tunayekuabudu, na Wewe tu Ndiye tunayekuomba msaada”. Kwa hivyo, ni lazima ile Lakiri ya Upweke wa Uungu iwepo katika akili zote na aina zote za viumbe kama ambavyo ipo kwenye kila kiumbe tofauti, na kuwa lazima, kila mmoja na wote, wamkumbuke Yeye katika Upweke Wake:hitaji lile hutimizwa kwaUpweke wa Uungu kuonyeshwa ndani ya Lakiri ya Rehema ya Uungu. Kisha, kila mmoja, katika kila ngazi, huwezeshwa kumgeukia Yeye Aliye Nadhifu na Mtakatifu, na huku akisema: “Wewe tu Ndiye tunayekuabudu, na Wewe tu Ndiye tunayekuomba msaada”, huongea na Yeye moja kwa moja.

Ni katika kuidhihirishahii siri pevu, kuonyesha wazi wazi hiyo Lakiri ya Rehema ya Uungu, ndipo Qur'an ambayo imejaa Hekima Zote ghafla ikaingiza taarifa maalumu kwa ujumla, ilito ndogo kuliko zote ikiwa na eneo kubwa kuliko yote la rejea, na ile maalum ikiwa na kitu cha kawaida sana, kama kwa mfano, uumbaji wa mbingu na ardhi. Ili akili iweze kuepushiwa kutangatanga na moyo uepushiwe kuzama, ili roho igunduwe moja kwa moja Lengo lake la Kweli la Kuabudu, Qur'an imeligusia somo la kuumbwa kwa mwanadamu na la kusema kwake, taarifa za kindani za vitu alivyopewa na hekima vilivyomo kwenye umbile lake, kwa mfano kila inapotaja kuumbwa kwa mbingu na ardhi.Ukweli huu umedhihirishwa kiajabukatika aya ifuatayo:

30:22Na katika ishan Zake (za kuonyesha Uweza Wake) ni kuumba mbingu na ardhi, na kuhitilafiana lugha zenu na rangi zenu.”

Katika viumbe visivyohesabika, katika kuzaliana kusiko kifani, zipo aina na daraja za Lakiri ya Umoja wa Uungu, katika, kama inavyoweza kusemwa, miduara yenye katimoja kutoka kwenye mkubwa kuliko yote mpaka mdogo kuliko yote. Lakini hata huo Umoja uwe wazi wazi namna gani, bado ni Umoja ndani ya uwingi, na hauwezi kuongelewa kikweli na watazamaji.Kwa hivyo, sharti kuwepo Lakiri ya Upweke wa Uungunyuma ya Umoja - ili utafauti wa kila kimojahauleti picha akilini ya uwingi, na ili, moja kwa moja mbele ya Yeye Aliye Nadhifu na Mtakatifu, njia ya kwenda moyoni yaweza kufunguliwa.

Tena ili kuionyesha Lakiri ya Upweke wa Uungu, kuuvutia moyo kwake, kielelezo cha kushangaza, mwanga unaoangaza sana, utamu muafaka, uzuri wa kupendeza na ukweli wenye nguvu, vimewekwa juu yake. Bila shaka ni nguvu za Rehema zinazoonyesha viumbe vyenye hisia, zinazovivutia kwake, na kuwawezesha waifikie Lakiri ya Upweke, kumtumikia Yeyekatika Upweke Wake, na hivyo kuonyesha anuani halisi ya maombi: “Wewe tu Ndiye tunayekuabudu, na Wewe tu Ndiye tunayekuomba msaada”.

Kwa hivyo, Kwa Jina la Allah, Mwingi wa Rehema na Huruma, faharisi ya Mlango wa Ufunguzi (Al-Fatiha) na mukhtasari wa Qur'an, ni ishara na mkalimani wa hii siri pevu.Kila anayeifikia ishara hii anaweza kupanda kupitia daraja za Rehema ya Uungu. Na yeyote anayemfanya huyo mkalimani kusema anaweza kugundua siri za Rehema ya Uungu na aione mianga ya Huruma na Wema.

Siri ya Tano

Ipo hadith isemayo kwamba Allah Alimuumba mwanadamu kwa umbo au mfano wa Yeye Aliye na Rehema Zote.Tafsiri ya masufi wakwezaji mno haiafikiani na misingi ya imani. Wengine wenye jazba mno miongoni mwao walidai kuwa hali ya kiroho ya mwanadamu ipo 'katika umbo la Mwenye Rehema Zote'.Wakiwa wamezama kwenye usingizi wa kubabaisha kwa kuwaza sana, huenda wanaweza kusamehewa kwa kutoa maoni ambayo ni kinyume na ukweli. Lakini wale wenye akili timamu lazima, baada ya kupima, waone yale maoni yao ambayo ni kinyume cha misingi ya imani kuwa hayakubaliki. Vinginevyo, wao pia watakuwa na makosa.

Allah Mnadhifu na Mtakatifu Ambaye huuamuru na huutawala ulimwengu wote kama vile ni kasri au nyumba, na huzigeuza nyota kwa urahisi kama vile ni punjepunje na akazisafirisha humo anganikwa hekima na uzuri, Ambaye huvituma vipunje vidogo sana kama vile ni maafisa watiifu, hana mfano wala msawa wake, wala mshiriki wala kinyume. Pia kwa muujibu wa maana ya aya:

42:11 Hakuna chochote mfano Wake, Naye ni Mwenye Kusikia, Mwenye Kuona.

Hana umbile hana mfano wala hana mwenzi aliye sawa Naye kwa namna yeyote.

Kwa upande mwingine, kwa muujibu wa maana na kwa kulinganisha kulikoashiriwa na aya:

30:27Naye Ndiye Mwenye sifa nzuri mbinguni na katika ardhi, Naye Ndiye Mwenye Nguvu, Mwenye Hekima.”

Matendo Yake na Sifa (Attriubutes), Majina Yake, yanaweza kutiwa fikirani. Yaani, mifano na malinganisho kuhusu matendo ya Allah, yanaruhusiwa. Hivyo, maana ya hadith inatutaka tuelewe:'Mwanadamu yu katika umbo ambalo kwa ujumla wake linaashiria Jina la Uungu, Mwingi wa Rehema.'

Hakika, kama tulivyoeleza hapo juu, Jina la Uungu, Mwingi wa Rehema, ladhihirika kupitia kwa Majina elfu moja na moja juu ya sura ya ulimwengu, na juu ya sura ya ardhikupitia ushahidi mwingi usio kifani wa Umola Pekee wa Allah. Kwa njia hiyo hiyo, kudhihirika kikamilifu kwa Jina, Mwingi wa Rehema, kunadhihirika, kwa mfano mdogo, katika umbile kamilifu la mwanadamu, kama ilivyo juu ya sura ya ardhi na ya ulimwengu.

Ushahidi mwingine wa uwiano sahihi katika suala hili, unaweza kupatikana katika mfano ufuatao:

Viumbe hai na mwanadamu ni machimbuko ya ushahidi (loci of evidence) wa Yeye Ambaye Lazima Yupo, uthibitisho na viyoo kwa Mwingi wa Rehema na Huruma. Hizi thibitisho ni za hakika sana, ni wazi mno na zaonekana mno kiasi kwamba, kama ambavyo mtu anaweza kusema kuhusu kiyoo kung'aa kinaporejesha mwanga wa jua - 'kiyoo kile kiko katika umbile la au kiko kama jua' - kwa maana ya kusisitiza mn'gao wa ushahidi wa mwanga wa jua katika kiyoo, ndivyo ambavyo mtu anaweza kusema, kama ilivyosemwa, 'Mwanadamu yuko katika umbile la Yeye Aliye Mwingi wa Rehema Zote' - kwa maana ya kusisitiza kwake uwazi wa ushahidi ndani yake wa Mwingi wa Rehema. Kwa hivyo, kwa muujibu wa mfano huu wa hiyo siri, wale watuwa kati zaidi miongoni mwa wale wanaoamini 'Umoja wa Kitu' walisema, 'Hapana ambaye yupo ila Yeye', kwa maana ya kuonyesha uwazi wa ushahidi na ukamilifu wa uhusiano.

Ewe Allah, Ewe Mwingi wa Rehema, Mwingi wa Huruma! Kwa njia ya 'Kwa Jina la Allah Mwingi wa Rehema na Huruma', tuhurumie kwa muujibu wa kuwa Kwako Mwingi wa Rehema, nautufungulie akilini mwetu hizo siri za 'Kwa jina la Allah, Mwingi wa rehema na huruma', kwa muujibu wa kuwa Kwako Mwingi wa Rehema. Aamin.

Siri ya Sita

Ewe mwanadamu usiyekuwa na furaha, unayehangaika katika kutojiweza kusiko kifani na kuhitaji kusikokuwa na mwisho! Elewa jinsi Rehema ya Uungu ilivyo na thamani kubwa na jinsi inavyokubalika kama mpatanishi. Ni njia ya kwenda kwa Mfalme Mtukufu Ambaye ndani ya jeshi lake zimo nyota nyingi sana na punje ndogondogo zinazofanya kazi pamoja kwa utii na uelewano mkalifu kabisa. Na Yeye, yule Mfalme Mtukufu, Mmoja, wa Milele aliye kabla na baada milele, ndiye Ategemewaye Milele - kila kitu kinamuhitaji Yeye Ambaye asilani hana mahitaji yeyote.

Yeye yu tajiri kupita kifani, kamwe hauhitaji ulimwengu au vilivyomo ndani yake. Ulimwengu wote uko chini ya madaraka Yake na uongozi Wake, nao wote ni mtii mbele ya ufalme na ukubwa Wake, unamwogopa na unasujudu mbele ya ukuu Wake. Hiyo ndiyo Rehema ya Uungu, ewe mwanadamu, na ni kwa ajili yako. Inakupandisha hadi Kwake Yeye, asiye na hitaji lolote, Mfalme wa Milele, Anayekutaka urafiki, Anayekuita wewe ni mtumishi Wake mpendwa sana.Ke bado, kama ambavyo jua liko mbali sana nawe kiasi kwamba huwezi kulifikia wala kulikaribia ingawa mwanga wake unarejeshwa (reflected) na unawezeshwa kuuona kwa njia ya kiyoo chako, kwa njia hiyo hiyo, wewe uko mbali sana mno na Mwanga wa Yeye aliye Nadhifu na Mtakatifu, wa Milele wa kabla na baada ya milele, wewe huwezi kumkaribia Yeye lakini Mwanga wa Rehema Yake unamfanya \yeye Awe karibu nawe.

Kwa hivyo, ewe mwanadamu, kila anayeigundua Rehema hii huigunduahazina ya mwanga usiozimika. Na njia ya kukupeleka kwake ni kupitia katika Sunna za Nabii mbora kuliko wote, baraka za Allah na amani zimwendee yeye, ambaye ni mfano murua kuliko yote na wakala wa Rehema, sauti Yake iliyo fasaha kuliko zote na mleta habari mahili kuliko wote, na ambaye anasifiwa katika Qur'an kuwa ndiye 'rehema kwa limwengu zote'.

Na njia ya kuifikia huu udhihirisho wa Rehema ambao ni 'rehema kwa limwengu zote' ni kutamka ombi hilo la kumtakia baraka za Allah zimwendee juu yake. Kwa yakini, nia ya ombi hili ni rehema. Ikiwa ni ombi la rehema kwa yule ambaye ni udhihirisho hai wa Rehema ya Uungu, ni njia ya kuifikia hiyo 'rehema kwa limwengu zote', kwa ajili yako mwenyewe, na kwa hivyo kumfanya awe njia kwa ajili yako ya kuipata Rehema ya Mwingi wa Rehema wa wenye rehema.

Kundi lote la Waislamu katika idadi kubwa dunia nzima hutamka ombihili kwa ajili ya huyo 'rehema kwa limwengu zote' ambayo ni sawa Rehema. Na hili ndilo onyesho la kushangaza la jinsizawadi ya Rehema ya Uungu ilivyo na thamani sana na jinsi eneo lake lilivyo pana sana.

Kwa kumalizia: Kito cha thamani kuliko vyote katika nyumba-ya-hazina ya Rehema ni Mtume Muhammad, baraka za Allah na amani ziwe juu yake, naye pia ndiye mlinda mlango wake. Ufunguo wa kwanza wa hiyo nyumba-ya-hazinaya Rehema ni 'Kwa Jina la Allah, Mwingi wa Rehema na Huruma'. Na ufunguo ulio rahisi kuliko zote ni ombi au kumsalia Mtume.

Ewe Allah! Kwa ajili ya siri za 'Kwa Jina la Allah, Mwingi wa Rehema na Huruma' mpe baraka na amani yule ambaye Ulimpeleka awe rehema kwa limwengu zote kwa muujibu wa Rehema Yako na heshima kwake, na kwa ukoo wake na Maswahaba wake.

Tupe rehema ili tuepukwe na kuhitajia rehema ya yeyote, miongoni mwa viumbe wako, baki Yako Wewe. Aamin.

Utukufu uwe Wako Wewe! Hatuna ujuzi wowote isipokuwa ule uliotufundisha Wewe.

Hakika Wewe Ndiwe Mjuzi wa Vyote, Mwenye Hekima Zote.


İKİNCİ SÖZ

NENO LA PILI

Njia ya Kuelekea Katika Ridhaa

Ukitaka kuelewa jinsi ya kufaidi, kwa njia ya imani, kuridhika na kubarikiwa kukubwa kabisa, na jinsi ya kuzowea kufanikiwa na urahisi, basi isikilize hadithi yenye mafunzo ifuatayo.

Watu wawili kwa pamoja walifunga safari ya kikazi na ya kufurahi. Mmoja wao aliyekuwa na kiburi, anayejifikiria mwenyewe tu, akaelekea upande mmoja; na mwingine ambaye ni humhudumia Allah akaelekea upande mwingine.

Kwa kuwa yule anayejifikiria mwenyewe ana majivuno na anayetazamia kutokewa na mabaya tu, aliishia kwenye nchi aliyoidhani ni mbaya kuliko zote kwa sababu ya kutazamia kwake mabaya tu. Kule akajikuta kila pahala kazungukwa na watu mafukara na wa hovyo ambao wanateswa na waonezi na maisha yao kuharibika. Kila anapokwenda huona mandhari hiyo hiyo. Kila mtu katika nchi ile ana madhila yayo hayo. Kisha anaamua ayasahau matukio yote yale kwa kuwa mlevi. Basi kila mmoja anaonekana kama mgeni au adui kwake. Anapata maono ya kutisha ya wafu na watoto mayatima. Roho yake inatumbukia katika maumivu.

Yule msafiri mwingine, kinyume cha huyu, ambaye ni humhudumia Allah, mwenye tabia nzuri na akili ya wastani, anakwenda katika nchi ambayo, kwa maoni yake, ni nzuri sana. Mtu huyu mzuri anaona tamasha la watu wote. Katika kila kona kuna shangwe na furaha, na nyumba ya kumkumbuka Allah inafurika karibu ya kupasuka. Pia anaona sherehe za furaha za kumaliza wajibu zilizochanganyika na vilio vya kutajiana salamu njema na shukrani. Na pia anasikia mlio wa ngoma na bendi ya kuandikisha maaskari ukiwa na miito ya 'Allah Ndiye Mkuu Kupita wote' na “Hakuna mungu ila Allah'. Kinyume na yule msafiri mwingine, ambaye anaugua machungu yake yeye mwenyewe na ya watu wote, huyu msafiri mwenye hali ya furaha huwa anafurahia furaha yake mwenyewe na ile ya watu wote. Pia anafaidi biashara ya faraja na anatoa shukrani kwa Allah.

Anapokutana na yule msafiri mwingine, anaelewa hali yake na anamwambia, 'Umekuwa mwendawazimu. Vitu vyote vibaya na ubaya unaouona unatoka katika dunia yako ya ndani. Kwa sababu hiyo wewe unadhani kicheko ni kilio, na kumaliza wajibu nikufukuzwa na kunyang'anywa. Zindukana, safisha moyo wako ili hili pazia ovu lifunuliwe machoni kwako na ili uone ukweli. Kwani nchi hii ni ya sheria, ya utajiri na iliyostaarabika, inayomilikiwa na mfalme mwenye nguvu na huruma na haki. Wa hiyo mambo hayawezi kuwa kama unavyoyaona au kufikiri wewe.'Isha yule msafiri mwingine anazindukana na anjuta sana: 'Ndio, nimepotewa akili kwa sababu ya hivyo nilivyokunywa. Ahsante. Namwomba Allah Aridhike nawe kwa kuniokoa mimi kutoka kwenye hali hii mbaya.'

Ewe roho yangu! Ujue kwamba yule aliyewahi kuwa mtu wa kiburi anawakilisha kafiri (asiyeamini) au mtenda dhambi asiyejali. Dunia hii kwake yeye ina maana ya kilio kwa ujumla. Viumbe wote hai waonekana kuwa ni mayatima wanaolia kwa sababu ya machungu ya kutengwa na uozo. Wanadamu na wanyama wanaonekana ni viumbe wapweke, wasiostaarabika walioteketezwa kwa vifo. Vitu vikubwa kama milima na bahari vyaonekana katika maono yake kama mzoga mwovu usio roho. Maono yake yanayotokana na kutoamini kwake na kuelekezwa vibaya kunazaa wasiwasi katika akili yake unaomtesa yeye.

Lakini yule mtu mwingine ni mwenye kuamini. Anaamini juu ya Allah na anamkiri Yeye. Kwa jinsi anavyoona yeye, dunia hii ni pahala ambapo watu wanamtukuza Yeye, aina ya uwanja wa kufanzia mazoezi kwa watu na wanyama, ni aina ya jengo la kufanyia mtihani kwa watu na majini. Kila aina ya wanyama na wanadamu wanafurahia kuwaliza wajibu wao - yaani wale wanaomaliza wajibu wao wa maisha husafiri na furaha ya kiroho mpaka kwenye dunia nyingine ya milele. Hii ni rahisi sana kuelewa - dunia yahitaji kizazi kipya cha kuijaza na kufanyia kazi humo. Aina nyingiza wanyama na wanadamu wameingiaduniani kufanya shughuli zao maalumu. Viumbe vyote hai ni kama askari au hata maafisa wanaofurahia shughuli waliochaguliwa. Na sauti zinazosikika ni sauti za kusifu kwao na kutukuza, wanapoanza, au za furaha wanapofanya kazi, au za kutoa shukrani wanapomaliza. Kwa maoni ya mtu anayeamini, vitu vyote ni vitumishi vitii, au maafisa marafiki, kitabu kipendwacho cha Bwana Mwingi wa Ukarimu kulikowote na Mmiliki mwenye Huruma zote, Kweli nyingi zaidi nzuri na kuu na za furaha kama hizi zinatokana na imani yake.

Hii ni kwa kuwa imani huzaa mbegu ya kitu ambacho kwa kweli ni mti wa Tuba wa peponi. Ambapo kutoamini kuna mbegu ya mti wa Zukkum wa Motoni.

Usalama na hali njema hupatika katika uislamu na katika imani tu. Kwa hivyo sharti tuwe tukioa shukrani kwa Allah, kwa kusema: 'Sifa zote ziwe za Allah kwa dini ya Islam na imani kamilifu.'


ÜÇÜNCÜ SÖZ

NENO LA TATU

Kuchagua Njia Sahihi

Kwa Jina la Allah, Mwingi wa Rehema na Huruma

2:21Enyi watu! Mwabuduni Mola wenu……

Ukiwa unataka kuelewa utamu na faida ambayo huja na sala au maombi, na hasara kubwa na mbomoko unakuja na dhambi nakuteketea kunakokuja na kutotekeleza amri za Allah, basi sikiliza hadithi hii fupi ya kufundisha ifuatayo, na ujaribu kuielewa.

Hapo kale, askari wawili waliamuriwa waende katika mji wa mbali. Wakatembea pamoja hadi walipofika njia-panda. Mtu mwenye busara aliyesimama pale akwaambia:

'Barabara iendayo kulia haina hatari na wasafiti tisa kati ya kumi wapitao barabara ile hufaulu na hawapati tatizo. Lakini barabara iendayo kushoto haileti faida yeyote na wasafiri tisa kati ya kumi wanaopitia kule hupata hasara kubwa. Barabara zote ni sawa kwa urefu. Lakini kuna tofauti hii moja - msafiri katika barabara ya kushoto, ambao haina kanuni na haina anayeisimamia, husafiri bila vifaa wala silaha. Kwa hivyo anaonekana kuwa anastarehe sana na hali yake ni rahisi. Kwa yule askari mwingine mambo ni kinyume, barabara anayoipitia iko chini ya kanuni za kijeshi. Sharti achukue gunia zima la vyakula vyenye lishe nzuri, vyenye uzito wa takribani kilo nne na silaha kubwa ya kijeshi yenye uzito mkubwa ambayo itamshinda adui yeyote kwa urahisi.

Baada ya kusikiliza ushauri wa yule mtu mwenye busara, mmoja wa wale maaskari wawili, yule mwenye bahati, akaelekea barabara ya kulia. Akanyanyua na kubeba mgongoni mzigo wake mzito (ingawa unabebeka); lakini moyo wake na roho yake vinaepuka yale madeni makubwa na woga. \yule mtu mwingine, asiye na bahati, anajiondoa jeshini, anakataa kuwa chini ya kanuni na anaelekea barabara ya kushoto. Mwili wake hauna ule uzito mkubwa wa mizigo, lakini moyo wake na roho yake vimejaa hatari na wasiwasi. Saa zote ana woga na milele ana mahitaji. Hatimaye anafika mjini. Kule anahesabiwa kuwa ni muasi na mkimbizi.

Yule askari anayeridhia kanuni za kijeshi, anayebakia na gunia lake na silaha na anayeelekea katika barabara ya kulia, anasafiri kwa amani, bila wajibu wowote na bila kumwogopa mtu yeyote. Naye pia hatimae anafika mjini; lakini anahesabika kule kuwa ni askari mwaminifu ambaye katekeleza wajibu wake kikamilifu.

Sasa, ewe roho yangu isiyo nidhamu yenye tamaa za kimwili, zingatia: mmoja wa wale askari anawakilisha mtumishi mtiifu wa Allah, wakati yule mwingine anawakilisha wale waasi na wanaofuata matakwa yao wenyewe. Ile barabara ni mshipi-wa-maisha unaotoka katika dunia ya roho nyingi, ikipitia katika dunia hii na kaburini na kuendelea hadi kwenye Maisha-baada-ya-kifo. Ule uzito mkubwa (lakini unaobebeka), na silaha ni wajibu wa kuabudu na ucha-Mungu. Sala zaelekea ni kazi ngumu, lakini kwa hakika zinampa mtu amani na faraja zisizoweza kuelezeka kwa maneno. Anayesali hutamka ndani ya sala zake Ash-hadu an laa ilaaha illal-Allah, yaani,

'Ninashuhudia kuwa hapana mungu ila Allah, Ambaye Ndiye Muumba na Mpaji-Vyote. Kila kitu, kiwe cha shari au cha kheri ni zawadi ya Allah. Yeye ni Mwingi wa Hekima zote; kamwe Hafanyi vitu visivyokuwa na maana; na ni Mwingi wa Huruma zote; Rehema Yake na Ukarimu ni mwingi sana. Kwa kuwa ana imani, yule askari anayeamini anaona katika kila tukio mlango uelekeao kwenye utajiri wa Rehema ya Uungu, na huugonga mlango huo kwa sala zake. Anatambua kwamba kila kitu ulimwenguni kiko kwa ajili ya Rabb wake, Mola wake na Muendelezaji wake. Hukimbilia Kwake Yeye.

Huku akimuamini kabisa Allah na akiwa kajisalimisha kikamilifu, hujilinda dhidi ya maovu yote ya dunia. Imani yake humpa kujiamini kikamilifu.

Kama ilivyo kwa kila tendo, chanzo cha huko kujiamini ni imani na kujitolea kitiifu kumpenda Allah; na kamailivyo kwa kila tendo baya, chanzo cha woga ni kupotoshwa. Hata kama dunia italipuka kama bomu, haitomtisha mtumishi mzuri wa Allah ambaye ana moyo ambao umeangazwa kikweli. Anaweza hata kuyatazama matukio hayo kwa heshima kama ni ajabu ya Pawa ya Anayetegemewa-Milele - wakati mtu anayetumia akili zake (rationalist) na mwanafalsafa maarufu lakini asiyekuwa na imani anaweza kutetemeka akikiona kimwondo (comet) angani, huku akiogopa kuwa kisije kikaiangukia dunia.(Hivi ndivyo watu wengine huko Marekani walivyohisi hivi karibuni walipokiona kile kimwondo cha 'Halley's comet').

Mwanadamu ana matakwa yasiyokwisha, lakini uwezo wake wa kuyakidhi ni mdogo mno. Yuko chini ya hatari ya madhila kadhaa, wakati nguvu zake binafsi zinaishia pale anapoweza kupafikia, mahitaji na matakwa yake, mateso na hudhuni zake, ni mapana kama dhana zake.

Sasa mtu yeyote ambaye sio kipofu kabisa wa kuuona ukweli, ataelewa kuwa ni faida kubwa, furaha kubwa na riziki kubwa sana kwa kiumbe fukara, kisichojiweza na dhaifu kama mwanadamu kujisalimisha kwa Allah, kumwabudu, kumwamini, na kumtegemea Yeye. Kama kila mmoja atakavyokubali, barabara salama ni bora kuliko barabara ya hatari, hata kama upo uwezekano mdogo sana wa kupita salama. Njia ya imani tunayojaribu kuieleza ni njia salama na inayompelekea mtu kwenye raha isiyokwisha na kwa takribanuhakika kamili. Hata hivyo njia ya wasioamini na waasi, kama walivyokubaliana wataalamu wengi sana na watu wenye ufahamu (insight) na uchunguzi, na hata ukakubaliwa na waasi wenyewe, haina faida na ina takriban uhakika kamilifu wa hasara isiyo mwisho.

Kwa ujumla, twaweza kusema hivi:Kama ilivyo raha ya dunia nyingine, furaha ya dunia hii pia inategemea kuwa umejisalimisha kwa Allah na kuwamtumishi Wake Yeye mtiifu. Hivyo sharti tumtukuze Allah bila kuacha, kwa kusema: 'Sifa ziwe kwa Allah kwa utii na fanaka katika NjiaYake'; na tumshukuru Yeye kuwa sisi tu Waislamu.


DÖRDÜNCÜ SÖZ

NENO LA NNE

Thamani ya Sala Zilizoamriwa

Kwa Jina la Allah, Mwingi wa Rehema na Huruma

Sala Zilizoamriwa ni Nguzo ya Dini

Iwapo unataka kuelewa kwa uhakika wa kuwa mbili kujumlisha mbili ni nne jinsi sala zilizoamriwa (salat) zilivyo na thamani kubwa na muhimu, na kwa jitihada ndogo tu inayokufanya upate zawadi ya kusali, na jinsi ilivyo ujinga na hatari kwa mtu kutosali, basi sikiliza kwa makini hadithi hii ifuatayo:

Hapo kale mfalme maarufu aliwatuma watumishi wake wawili kwenda katika shamba zuri, akimpa kila mmoja sarafu 24 za dhahabu. Hilo shamba lilikuwa na umbali wa miezi miwili. Akawapa maagizo yafuatayo:

'Tumiaeni fedha hizi kwa tikiti na mahitaji mengine ya safari na ya baada ya kuwasili.

Iko stesheni moja iliyoko umbali wa siku moja ambako treni, gari na ngede huwepo, Na ambazo mnaweza kutumia yeyote kulingana na mtaji wenu.'

Wale watu wawili wakatoka baada ya kuyapata maagizo haya. Mmoja ana bahati sana kiasi kwamba alitumia sehemu ndogo tu ya fedha zake kabla ya kufika pale stesheni.

Alitumia fedha zake uzuri hadi bwana wake akampenda.Hivyo mali zake zikaongezeka Mara elfu moja. Yule mwengine kwa kuwa alikuwa hana bahati na ni mjinga, alitumia sarafu zake 23 kati ya zile 24 katika kamali na mambo kama hayo kabla hajafika pale stesheni. Akabakiwa na sarafu moja tu. Rafiki yake akamwambia:

'Tumia sarafu hii kununulia tikiti, usipofanya hivyo, itakulazimu wewe uende kwa miguu na utaabike na njaa. Bwana wetu ni mkarimu, huenda atakuonea huruma na kukusamehe. Wanaweza kukuruhusu upande ndege, na hivyo tukaweza kufika shambani kwetu kwa siku moja. Vinginevyo utalazimika kwenda kwa miguu na uvumilie kwa miezi miwili ya njaa wakati ukilivuka jangwa.'

Iwapo yule mtu asiyekuwa na bahati asipomsikiliza rafiki yake na atumie ile sarafu muhimu kununulia tikiti, ikiwa badala ya hivyo atachagua kuitumia kwenye madhambi kwa kufaidi maraha, hata mtu mjinga kuliko wote atakubali kuwa mtu yule amesimama katika hasara na ujinga mkubwa sana.

Sasa basi, ewe mwanadamu usiyesali, na ewe roho yangu isiyo mwelekeo wa Kusali, sikiliza maelezo yake!

Huyo mfalme maarufu ni Mola wetu, Muumba wetu. Wale watu wawili, mmoja ni mcha-Mungu anayesali sala zake kwa ari sana. Mwingine yule asiyejali, anawakilisha watu wasiopenda kusali. Zile sarafu 24 za dhahabu ni saa 24 za kila siku moja. Shamba ni Mbinguni na stesheni iliyoko jirani ni kaburi. Safari yaanzia kaburini kwenda hadi kwenye maisha ya milele. Watu huenda safari hiyo ndefu kwa nyakati tofauti, kufuatana na matendo yao na tabia zao. Wengi kati ya wale wacha-Mungu kikweli, hupitisha maisha ya miaka 1000 kwa siku moja kama radi, wengine saaa hamsini kila saa kwa spidi ya kudhani: Qur'an inarejea au inakariri ukweli huu katika aya zake mbili.

Hiyo tikiti ni salat, yaani sala iliyoamriwa. Saa moja tu inatosheleza kusali sala za siku moja. Iwapo utatumia saa 23 za kila siku ya maisha yako katika dunia hii, na huihifadhi hiyo saa moja tu iliyobakia kwa ajili ya sala muhimu ambazo ndizo muhimu kwa hiyo dunia nyingine, hiyo itaonyesha ujinga wako, na inakuweka katika hali ya hasara kubwa. Unaweza kuwa na shauku ya kulipa nusu ya fedha zako kwenye bahati nasibu ambako wapowatu 1000 wanacheza, ingawa uwezekano wa wewe kushinda ni moja ya elfu moja.Ambapo ukisali, uwezekano wa kushinda ni 99%. Sasa usipotumia Moja ya sarafu zako kuipata fursa hii, kuchuma haziza isiyokwisha, mtu yeyote ajionaye ana akili timamu ataacha kuelewa jinsi tabia yako hiyo ilivyokuwa mbali sana na utumizi wa akili yako?

Isitoshe katika kusali kuna faraja kwa roho na akili. Wala sio vigumu kwa mwili.

Tena, ukiwa na nia njema, matendo yote na tabia zote za yule anayesali huwa kama ibada. Kwa njia hii, maisha yake mafupi hutumika kwa ajili ya maisha ya milele huko kwenye dunia nyingine. Na maisha yake ya kupita hupata ile hali ya kudumu.


BEŞİNCİ SÖZ

NENO LA TANO

Mafunzo Sahihi kwa Muumini

Kwa Jina la Allah, Mwingi wa Rehema na Huruma

16:128 Innal-Lwaaha ma'al-ladhiynat-taqaw wal-ladhiyna hum-muhsinuwn (Kwa hakika Allah yu pamoja na wale wanaomcha (Yeye), na wale wafanyao mema (kama vile wanamuona Yeye).”

Kuelewa kuwa kazi tulizopewa za kusali sala zilizoamriwa na za kuepuka madhambi makuu ni kweli, na kuwa kazi zote mbili zimeelekezwa moja kwa moja katikahulka ya wanadamu, soma hadithi ya mafumbo ifuatayo:

Wakati wa vita kulikuwepo maaskari wawili kwenye kundi la jeshi, mmoja amefunzwa barabara na mwenye moyo mwema, na Mwingine ni askari mpya na ni mtumwa kwa nafsi yake. Wa kwanza huhudhuria mazoezi na hukazana dhidi ya adui. Hana hofu juu ya vyakula na masrufu kwa sababu ana hakika kuwa ni kazi ya serekali kutoa vifaa na vyakula, na akitokea kupaja ugonjwa au majeraha itampa matibabu kamili. Anajua kuwa kazi yake kuu ni kwanza kujifunza kisha kupigana kwa aniaba ya nchi; pia hushiriki katika kugawa vyakula na hufanya kazi kidogo jikoni kama kuosha mabakuli ya kulia.

Akiulizwa anachofanya, hujibu: 'Ninafanya baadhi ya kazi za nchi (kazi za nchi)'.

Hasemi anafanya kazi ili aweze kuishi.

Mwingine, askari asiyekuwa na uzoefu na anayejifikiria mwenyewe, hahudhurii mazoezi ya mafunzo ya mara kwa mara wala kupigana. Hujieleza yeye mwenyewe kama ifuatavyo:'Hiyo hainihusu mimi, hiyo ni ya serekali.'.Kwa sababu ya msimamo huu, yeye hujali maisha yake tu, hutoroka kutoka kwenye uwanja wa vita na badala yake huenda sokoni.

Siku moja yule askari mwingine ambaye haupendi mwelekeo huu, alimshauri hivi:'Ndugu yangu, kazi yako kuu ni kujifunza kuhusu vita na upigane kwa niaba ya nchi. Ndio maana umepewa nafasi hii. Lazima umtegemee mfalme. Hakuachi uwe na shida ya chakula. Kutoa vyakula na masrufu ni jukumu lake sio lako. Wa vyovyote wewe huna uwezo wa kujipatia vyakula nyakati zote muhala momote. Na sasa tumo katika hali ya vita: wewe unaweza kushitakiwa kuwa u mtoro au muasi na ukabiliwe na adhabu.

'Ni kweli yaelekea kuna kazi mbili, moja ni jukumu la mfalme na nyingine letu. Mfalme mara kwa mara hutoa mahitaji ya mafunzo na vita. Azi yetu ni kufunzwa na kupigana.'

Hebu fikiria jinsi ilivyo hatari ile hali ya askari yule asiyejali iwapo hatozingatia hayo anayoambiwa na rafiki yake!

Ewe roho yangu kaidi! Ule uwanja mkali wa vita unawakilisha hekaheka za maisha ya dunia hii. Jeshi lililogawanywa katika makundi ni picha ya watu wa mataifa yote, na lile kundi maalum la kivita linawakilisha jumuiya ya Kiislamu. Wale maaskari wawili, mmoja ni mcha-Mungu wa Kiislamu ambaye anajua kile anachoagizwa akifanye na anajitahidi dhidi ya nafsi yake na dhidi ya Shetani ili asitende madhambi. Yule askari mwingine ni mtenda dhambi asiye bahati ambaye kamwe hajali kufanya wajibu wake kama mtumishi, kama alivyopangiwa na Allah, lakini hutenda madhambi mengi sana, na tena anajali mno vyakula na masrufu mpaka anamshutumu Muendelezaji. Mafunzo yanawakilisha sala za kila siku na wajibu mwingine anaotazamiwa awajibike kwao kila mtumishi muumini wa Allah. Vita inawakilisha mwenendo mzima wa roho kupata uokovu wa milele.

kwa njia ya kupigana dhidi ya matamanio ya kimwili (carnal passions), yawe ni matamanio ya kuzuka yenyewe au yanayoshawishiwa na Shetani. Kazi mbili zilizotajwa hapo zinaeleweka kiurahisi: ya kwanza, kuumba na kuendeleza maisha ni jukumu la Muumba peke Yake. Ya pili ni jukumu letu - kuomba au kutoa shida kwa Muumba na Muendelezaji, na kumtegemea Yeye tu kikamilifu.

Ni Yeye tu Anayetoa maisha au uhai ambayo ni muujiza wa kierevu kuliko yote wasanaa ya Yeye Anayetegemewa Milele, na ajabu ya Hekima ya Mola, Anaendeleza maisha kwa vyakula. Je, unahitaji kushawishiwa?

Wanyama dhaifu na rahisi kuliko wotekama samaki na minyoo ya matunda ndio ambao hulishwa vizuri kuliko wote. Pia wale viumbe wasiojiweza na wenye hatari ya kushambuliwa kuliko wote, kwa mfano watoto wachanga, au wanyama waliotoka kuzaliwa, hupata vyakula bora kuliko vyote.

Kupata chakula kinachohitajika sio suala la kutumia nguvu au matashi (hiari); kinyumwe cha hivyo, ni suala la kuhitaji na kutaabika kwa ukosefu au uhaba.Ili kuelewa jinsi hii iwezavyo kuwa, linganisha jinsi miti inavyolishwa na jinsi wanyama wanavyolishwa, linganisha samaki na mbweha, watoto wachanga na majitu wakatili, na haya yatosheleza kukushawishi.

Mtu yeyote ambaye huacha sala zake za kila siku kwa ajili ya maisha yake ya kawaida, huyo aweza kilinganishwa na askari katika hadithi hiyo ya mafumbo: anadharau mazoezi yake, anatoroka kutoka katika uwanja wa vita kwa sababu ya kuhofu kutopata chakula na anakwenda kuzurura sokoni.

Kinyume cha hivi, mtu kutafuta rizikikutoka ardhini (jiko la Rehema ya Yeye Aliye Mkarimu na Mpaji wa vyote - baada ya kutekeleza sala, na kuepuka kuwa mzigo au tatizo kwa wengine, ni ubora na utu halisi (fine and manly). Hii pia ni aina ya ibada.

Isitoshe, hulka na mwanadamu na roho yake vyaonyesha dhahiri kuwa ameumbwa ili kumwabudu Allah. Yeye (mwanadamu) yu mdogo kuliko hata mbayuwayu mdogo kulingana na nguvu zake za kimwili tu na ushindaniunaotarajiwa kwa maisha ya dunia hii. Lakini kwa muujibu wa ujuzi na uelewaji wake wa mahitaji yake, kusali au kuomba na kuabudu - ambavyo ni lazima kwa maisha yake ya kiroho na maisha ya Baada ya Kifo - yeye ni mfalme na kamanda wa viumbe vyote hai.

Kadiri unavyoiandaa dunia hii,ewe roho yangu, lengo lakona kazi kwa ajili yake, wewe unaweza kuwa askari tu ndani yake, usiye na udhibiti zaidiwa mambo yako kama alivyo nao mbayuwayu. Ambapo ukielekea kwenye Maisha ya Baada ya Kifo na uihesabu dunia hii kuwa ni shamba la kupandwa tu, maandaaji ya dunia ijayo, na utende itakikanavyo, utakuwa mfalme wa ufalme wa wanyama na mtumishi muwezana muombaji wa Allah, na mgeni mheshimiwa Wake katika dunia hii.

Sasa una chaguzi mbili.Unaweza kuchagua yeyote kati ya ke.Kwa hivyo omba mwongozo na fanaka kwa njia Yake kutoka kwa Mwenye Huruma kuliko wenye huruma wote.


ALTINCI SÖZ

NENO LA SITA

Mapatano Makuu

Kwa Jina la Allah, Mwingi wa Rehema na Huruma

“9:111 Innal-Lwaaha shtaraa minal mu-uminiyna anfusahum wa amwaalahum bi anna lahumul jannah. “Allah Amenunua kwa Waislamu nafsi zao na mali zao (watoe mali zao na nafsi zao katika kupigania dini) ili na Yeye Awape Pepo).”

Ikiwa unataka kuelewa faida ya mapatano, kuelewa heshima ya cheo, apatayo anayeuza roho au nafsi na mali yake kwa Allah, na kuwa mtumwa Wake na askari Wake, hebu isikilize hadithi ifuatayo ya mafunzo:

Hapo zamani mfalme aliwakabidhi watu wake wawili shamba (estate) kwa kila mmoja, pamoja na karakana zote muhimu, mashine, farasi, silaha na vifaa vingine. Lakini wakati ule ulikuwa wa vita, ambapo vitu havikubakia vilivyo, bali sharti viportee au vibadilike. Mfalme, katika rehemayake alimtuma afisa wake mkuu kabisa kwa hao watu wawili, na kwa njia ya amri ya hurumaaliwaarifu ifuatavyo:

'Niuzieni mali mlioishika kwa niaba au dhamana, ili niwahifadhie mimi. Isiharibike bure. Vita itakapokwisha, nitawarejeshea ikiwa katika hali njema zaidi kuliko kwanza. Ni mali yenu ya dhamana nami nitawalipa bei kubwa.

Mashine na vifaa vyote vitatumika kwa jina langu kwenye meza yangu. Bei zake na ada za kuvitumia zitaongezwa zote, huenda mara elfu. Nitawapa ninyi wenyewe faida yake. Ninyi mu dhaifu na mafukara. Hamuwezi kugharimia kazi kubwa kama hizi. Kwa hivyo niacheni mie nigharimie mahitaji na vifaa vyote, na niwape ninyi mapato na faida zote. Ninyi mtavitumia mpaka silaha zitakaponyang'anywa. Zifikirieni faida hizi tano za maafikiano haya.'

Na msiponiuzia mali hizo, kama muonavyo, hakuna anayeweza kuhifadhi alicho nacho. Ninyi pia mtapoteza vyote mlivyonavyo sasa. Vitatoweka bure, na mtakosa bei kubwa ninayowapa. Vifaa tatavyenye thamani kubwa kabisa, mizani mizuri, vilivyo tayari kutumika, vyote vitapoteza thamani yao kwa vile hakuna vyumavyuma vinavyofaa kufanyia kazi vifaa hivyo. Pia mtakuwa na shida ya kuviangaliana kuvihifadhi vyombo hivyo, kisha mtaadhibiwa kwa kuvunja dhamana yenu .

Kuuza mali zenu kwangu ni kuwa askari wangu na mutende kwa jina langu. Mbali na Kuwa askari wapya au askari wa kawaida tu, mtakuwa maafisa waheshimiwa wa mfalme mtukufu.'

Baada ya hao watu wawili kusikiliza hiyo amri njema, mmoja wa wale wawili aliyekuwa na busara akasema:

“Kwa vyovyote vile nina heshima na furaha kuuza. Ninatoa shukurani mara elfu moja.”

Yule mwingine alikuwa na kiburi, mchoyo na aliye mfisadi, nafsi yake ilikuwa inajivuna kama ya Farao. Kama mabaye alikuwa wa kukaa milele kwenye shamba lile, alipuuza mitetemeko ya ardhi na misukosuko ya dunia. Akajibu:

“Hapana! Ni nani Mfalme? Sintouza mali yangu wala kupunguza maraha (confort) yangu.”

Baada ya muda mfupi tu, yule mmoja alifikia cheo kikubwa sana kiasi kwamba Kila mtu akawa anamwonea wivu. Alipendwa na mfalme, akaishi ndani ya kasri ya mfalme kwa furaha. Yule mwingine, kinyume chake, alishuka hadhi chini sana mpaka kila mmoja akawa anamwonea huruma na kusema: “Alistahili hivi.” Kwa sababu ya makosa yake, akapoteza furaha yake, pamoja na mali yake, na akawa anateseka na Adhabu na uchungu kwa ajili hiyo.

Sasa! Ewe roho, uliyejaa matamanio! Itazame sura ya ukweli kwa njia Ya darubini ya hii hadithi ya mafunzo. mfalme kwenye hadithi ndiye Mfalme wa Milele, wa kabla na baada ya milele, Molawako, na Muumbaji wako.

Mashamba na nyumba, alana mizani ni raslimali unayoiita ni yako maishani mwako - vikiwemo mwili wako, roho yako na moyo wako, na hisia zako za nje na ndani kama jicho, ulimi, akili, na uwaziaji . Afisa mbora zaidi kuliko wote katika hadithi hii ya kufunza ni Mjumbe Mbora wa Allah, na amri ya hurumaniQur'an yenye Hekima, ambayo inaainisha biashara (transaction) tunayoiongelea katika aya ifuatayo:

“9:111 Allah Amenunua kwa Waislamu nafsi zao na mali zao (watoe mali zao na nafsi zao katika kupigania dini) ili na Yeye Awape Pepo).”

[Innal-Lwaaha shtaraa minal mu-uminiyna anfusahum wa amwaalahum bi anna lahumul jannah.]

Ule uwanja wa vita uliojaa ni sura ya dunia yenye mawimbiambayo hubadilika, huyeyuka, na hugeuka, na kumfanya mwanadamu atafakari.

Na mwanadamu huuliza: Kwa kuwa kila kitu kitatoka mikononi mwetu, kiteketee na kupotea, hakuna njia ya kukigeuza kiwa kitu cha kudumu milele?

Tutawezaje kukihifadhi? “Wakati anafikiria hayo, ghafla mtu huyo husikia sauti ya mbinguni ya Qur'an ikisema hivi:” Hakika ipo njia nzuri na rahisi ambayo inatoa faida tano.

“Njia gani hiyo?”

“Kuuza dhamana hiyo kwa Mwenyewe halisi Mwenye Yake. Hizo faida tano katika biashara hiyo ni hizi zifuatazo:

Faida ya kwanza: Mali ya mpito hugeuka kuwa ya kudumu. Haya maisha ya kufifia, akipewa Yeye wa Milele na Ajihuishae Mwenyewe wa Utukufu na ukavitumia kwa ajili Yake vitabadilika na kuwa vya kudumu milele.

Huzaa matunda na kudumu daima. Nyakati za maisha ya sasa ya mtu, bila shaka, zitapotea na zitaoza kama zinavyooza mbegu na viini vyake. Lakini maua ya furaha yatafunguka na kuchanua katika milki ya Umilele, na kila moja litatoa pia hali ya kung'aa na ya kutia moyo huko kwenye Milki ya Kati .

Faida ya pili:Pepo hutolewa kama zawadi.

Faida ya tatu:Thamani ya kila kiungo na kila hisisa huongezwa mara elfu moja.

Kwa mfano, akilini kipawa, chombo. Iwapo huiuzi kwa Mwenye Enzi Yote, lakini ukaitumia kwa ajili ya nafsi yako, itakuwa ni chombo cha mkosi, kibayana cha kudhuru, ambacho kitailemea nafsi yako dhaifukwa hudhuni za maisha yaliyopita na hofu za kutisha za maisha yajayo; itashukahadi kwenye daraja la chombo cha nuksi kiharibifu. Hii ndiyo maana mtenda madhambi daima huangukia kulewa, au anasa zingine za kipuuzi, ili kuepuka maudhi na majeraha ya akili yake.Lakini ukiiuza akili yako kwa Mmilikaji wake halisi, na uitumie kwa ajili yake Yeye, itakuwa kama ufunguo wa siri wa kufungua hazina isiyo kifani ya Hurumana ambayo makabati yake yamejaa busara ambazo viumbe huwa nazo. Ukiwa kama ufunguo, pia hukukweza wewe hadi kwenye daraja la muongozimuadilifu na mcha-Mungu anayestahili furaha ya milele.

Jicho ni moja ya hisia, dirisha ambalo roho hutazamia nje kuiona dunia.

Ukiwa hutoliuza kwa Mwenye Enzi Yote, bali ukalitumia kwa ajili ya nafsi yako kwa kukodolea macho vitu vyenye uzuri wa kupita na wa muda, litateremka daraja hadi kuwakama kuhadiwa matamanio ya kimwili. Lakini ukiliuza hilo jicho kwa Mtengenezaji Anayeona Kila Kitu, na ukalitumia kwa ajili Yakena chini ya masharti aliyoamuru Yeye, basi jicho lako litapanda daraja hadi kuwa msomaji wa Kitabu Kikuu cha Ulimwengu, shahidi wa miujiza ya Mola wa viumbe wote, nyuki aliyebarikiwa anayefyonza maua ya Rehema katika bustani la dunia hii.

Kuonja ni hisia nyingine. Iwapo hutoiuza kwa Muumbaji wako Mwenye Hekima, na badili yake ukutumie kwa ajili ya nafsi yako na kwa ajili ya ulimi au Tumbo, mlinzi katika karakana yake. Lakini iwapo utakuuza kwa Mpaji Mtukufu, basi hisia za kuonjaulizopewa ulimi itapanda daraja hadi kufikia mnyapara stadi katika hazina ya Huruma ya Kiungu, mkaguzi mwenye shukraniwa majiko ya Uweza Unaotegemewa Milele .

Ewe akili, hebu jihadhari! Fikiria jinsi chombo cha uharibifu kilivyo, na jinsi ufunguo wa kufungua kila kitu ulivyo. Ewe jicho! Ona tofauti baina ya kuhadi maovu na mnyapara msomi wa Maktaba ya Kiungu! Ewe ulimi!

Onja vizuri tofauti baina ya mwangalia mlango wa zizi au karakana na mdhamini wa hazina ya Rehema ya Allah!

Ukilinganisha ala na vipawa na viungo vyote hivi, utaelewa kwamba mwenye kuamini huipata hali ya kustahili kuingiaPeponi, na asiyeaminihuipata hali ya kuingia Motoni. Sababu ya kila mmoja wao kuipata hali hiyo ni kuwa, yule anayeamini, kwa sababu ya imani yake, hutumia dhamana ya Muumbaji wake kwa ajili Yake na chini ya amri Alizoamuru Yeye Mwenyewe; ambapo asiyeamini, huisaliti dhamana na huitumia hiyo kwa ajili ya nafsi yake ya kimwili.

Faida ya nne: Mwanadamu hana msaada na amekabiliwa na mikosi mingi. Ni fukara, na mahitaji yake ni mengi sana. Hajiwezi kwa lolote mwenyewe na mzigo wa maisha ni mzito sana. Asipomtegemea Yeye Mwenye Uweza Wote wa Utukufu, na aiweke imani yake juu Yake na ajisalimishe Kwake kwa dhati kabisa, dhamira yake daima itatatizika. Hujiona yanamsibu mateso ya bure, maumivu na majuto, na vyote hivyo humharibia kuelewa kwake, na kumgeuza awe kama mnyama mwitu .

Faida ya tano: Wale ambao wanaweza kuifunua asili ya kweli ya mambo, na waliopata uzoefu wa ukweli, wote wanakubali kwamba, zawadi tukufu ya kumuabudu na kumtukuza kote Allah kunakofanywa na viungo vyako, hisia zako na vipawa vyako, vyote utapewe wewe mwenyewe katika wakati wa shida kubwa zaidi kuliko zote, katika umbo la matunda ya Peponi.

Ukiwa hutaki biashara hii pamoja na faida zake tano, baki ya kunyimewa hizo faida, utapata hasara tano.

Hasara ya kwanza:Mali na vizazi uvipendavyo sana, ile nafsi na matamanio Unayoyapenda, na ujana na maisha ambayo unayapa mapenzi ya kijinga, vyote vitatoweka na badala yake machungu na madhambi ubaki umefungiwa shingoni mwako.

Hasara ya pili: Utapata adhabu ya kuisaliti dhamana, kwa kuwa, kwa kule kutumia kwako ala muhimu kwa ajili ya mambo yasiyo maana, utakuwa umeikosea nafsi yako wewe mwenyewe.

Hasara ya tatu: Kwa kuvidhalilisha vipawa vyote adhimu vya mwanadamu hadi kufikia daraja la chini zaidi kuliko la wanyama, utakuwa umeitukana na umeikhalifu Hekima ya Allah.

Hasara ya nne: Katika ufukara wako na kutoweza kwako kujisaidia, utakuwa Umejitwika mzigo mzito wa maisha katika mabega yako dhaifu, na daima Utakuwa ukinung'unika kwa ajili ya mambo ya mpito na utengano.

Hasara ya tano: Wewe utageuza vipawa vyema vya Yeye Mwenye Huruma, kama akili, moyo, jicho, ulimi, ambavyo ulipewa wewe ili uandae misingi ya maishaya milele na ya kubarikiwa ya huko Akhera au ya Baadaye, ili viwe na umbo baya, linalofaa kufungua malango ya Motoni yaliyo mbele yako.

Na fikia kuuza. Kwa nini watuwengi hawalikubali hili? Ni jambo gumu sana kulifanya - yaani kuuza?La, hata sivyo! Si vigumu hata kidogo. Viwango vya yanayoruhusiwa ni vipana, na vinatosheleza kabisa matakwa ya mwanadamu: hakuna haja ya kuvamia yaliyokatazwa. Kazi zilizoamrishwa na Allah ni nyepesi na chache. Kuwa mtumwa na askari wa Allah ni heshima kubwa mno kiasi kwamba haielezeki.

Kazi ya kila mtu ni kutendana kuanza kufanya kila kitu kwa Jina la Allah, Kama askari: kupokea na kutoa kwa niaba ya Allah, kutenda mambo kwa muujibu wa idhini na sheria Yake. Pindi mtu katenda dhambi, basi sharti aombe msamaha

Wake kwa kusema hivi: “Ewe Mola! Tusamehe madhambi yetu na utukubali sisi kama watumwa wako; ukabidhi imani Yako kwetu hadi wakati wa malipo utakapowadia. Aamin!” na umuombe Yeye.


YEDİNCİ SÖZ

NENOLASABA

Mlango Unaoelekea Kwenye Furaha ya Mwanadamu

Kumwamini Muumba Mwenye Enzi Zote na kuamini maisha ya Baadae, yote ni sawa kwa umuhimu, kwa kuwa ni kupitia imani hiyo ndiyo siri ya ulimwenguimedhihirishwa, na mlango wa furaha ya mwanadamu umefunguliwa. Kumtegemea Muumba katika ustahamilivu, kuomba kutoka kwa Mpaji kwa shukrani, na kutaka ukimbizi Kwake -hizi ni dawa muhimu kwa maradhi ya wanadamu. Kuitii Qur’an, kuzingatia sheria zake, kudumisha sala na kujizuia kutenda madhambimakubwa (Kaba’ir) hutengeneza nyaraka na pasipoti ya safari ya milele, mwanga wa kaburini na mafao yamaisha yajayo. Ukiwa unataka kuuelewa ukweli wa hili, sikiliza hadithi ifuatayo iliyojaa maana.

Hapo zamani palikuwepo askari katikati ya uwanja wa vita, ambaye alijikuta yumo katika hali ya kutisha. Alijeruhiwa upande wake wa kulia na kushoto - nyuma yake kulikuweko simba aliyekuwa tayari kumrarua, na mbele yake rafiki zake walikuwa wananyongwakwenye vitanzi. Na mbele yake ilikuweko barabaraya kwenda uhamishoni.

Askari huyo alikuwa na hudhuni kubwa na alikuwa ametatizika, wakati mtu mmoja mcha-Mungu na mwenye busara alipomtokezea upanda wake wa kulia, na akamwambia: “Usikate tamaa. Nitakupa hirizi mbili, maneno muhimu. Ukiyatumia, simba aliyeko nyuma yako atatulizana na mtii kama farasi, na vitabzi vitakuwa kama pembea ya wewe kustarehea. Pia nitakupa dawa mbili. Ukizitumia kwenye vidonda vyako, vitapona na kutoa harufu nzuri ya waridi. Nitakupa pia tikiti itakayokuruhusu wewe kusafiri umbali wa miaka katika siku moja. Ukiwa una shaka yeyote, basi zijaribu uone ukweli ninaosema.”

Baada ya hivi, ghafla mtu mmoja shetani akatokea upande wa ksuhoto na akasema: “Habu tufurahi, tusikilize muziki, tule na tunywe hivi vitu vitamu.”

Kisha akamwuuliza askari: “Maneno gani hayo unayosema yasiyoeleweka?”

“Ni dua takatifu”, akajibu huyo askari.

“Yaachilie mbali mambo hayo tata, na tusiharibu furaha yetu..

Ni kitu gani hicho mikononi mwako?

“Dawa.”

“Itupilie mbali. Wewe huna maradhi yeyote. Hilo karatasi gani lenye lakiri tano juu yake?”

“Ni tikiti, na kadi ya chakula.”

“Zichane! Unawezaje kufikiria kwenda safari katika siku nzuri hivi ya vuli (spring)?”

Kwa njia hii yule mtu shetani hujaribu kumlaghai na kumpotosha yule askari.

Na hatimayeaskariatashawishikakumfuata, kwa kuwa yeye ni mwanadamu, na wanadamu huweza kughilibiwa.

Kisha ghafla kuliani kwake, askari anasikia sauti kama ya radi ikisema hivi:

“Amka!Usighilibiwe. Liambile hilo shetani kuwa: ‘Ukiwa unaweza kumwuua simbanyuma yangu, basi fanya hivyo. Iwapo unaweza kuondosha vitanzi mbele yangu, basi fanyahilo. Iwapo unaweza kuyaponya madonda yangu basi yaponye. Ikiwa unaweza kupanga iuli nisiwe na haja ya kutoka hapa, basi fanya hivyo. Tukiona haya yote yanafanyika, basi tunaweza kufurahi.Ikiwa huwezi, basi nyamaza kimya, ewe mtu mjinga na muongo.!’

Na turejee kwenye ukweli.

Hujiona sisi wenyewe humu duniani kama yule askari. Simba ni wakati wetu uliochaguliwa wa kifo chetu. Kitanzi kinawakilisha utengano na marafiki zetu, mmoja mmoja, siku baada ya siku. Majeraha mawili ni: kutojiweka kwa lolote kwa milele kunakoudhi, na ufakara wa kuhudhunisha usio kifani. Safari ndefu ni ya kutokakwenye dunia ya roho kwenda hadi kwenye maisha ya kiini cha mtoto ndani ya tumbo la uzazi la mama, kisha hadi kwenye maisha ya ujana, uzeeni, kisha kuzikwa kaburini na maisha ya kaburini mpaka siku ya Ufufuo, na kupita kwenye daraja la Swiraatw ili kuanza maisha ya Baadae. Ama kuhusu zile hirizi mbili, ni imani juu ya Allah na imani juu ya maisha ya Baadae.

Kwa hivyo yaelewe maneno haya: “Imani juu ya Muumba Mwenye Nguvu Zote na imani juu ya maisha ya Baadae”. Hirizi hii adhimu hutupatia amani yaakilini mwetu, na Rehema ya Allah; na yule simba kwa kuwa hawezi kufanya lolote bila idhini Yake anakuwa mtii kama farasi. Kwa sababu hii, wale wacha-Mungu na wasomi, wale ambao wanakielewa kweli kifo hawaogopi kufa - kinyume chake wanapenda kufa kabla hata ya wakati waliopangiwa wafe.

Mpito wa wakati (passage of time), unaoingiliwa na utengano na marafiki zetu (kwa sababu ya vifo, vilivyowakilisha kwenye hadithi hii na vitanzi), kwa kuamini juu ya maisha ya Baadae, kwa hakika huwa ndio njia ya kuona nakshi zenye kujaa rangi na matendo ya ajabu ya Allahyanayojadidishwakila mara, miujiza ya Uweza Wake, na uthihirisho wa Huruma Zake. Kwa kuwa “viyoo” vinavyorudishazile rangi za jua ni tofauti na hubadilishwa, matokeo yanayoonekana huwa mazuri zaidi.

Ama kuhusu zile dawa, mojapo ni ustahamilivu na utegemezi kwa AllahAmbaye Ndiye Mmiliki waamri ya:

36:82 Hakika amri Yake Anapotaka chochote (kile kitokee) ni kukiambia tu:

'Kuwa', basi mara huwa. [Innamaa amruhuw idhaa araada shay-an an yaquwlalahuw kun fa yakuwn].”

Kwani hata katika hali ya kutisha kuliko zote na mbele ya afa au msiba mkubwa kuliko yote, yeye husema:

2:156 Ambao uwapatapo msiba husema: 'Hakika sisi ni wa Allah, na Kwake

Yeye tutarejea (Atatupa jazaa Yake). [Al-ladhiyna ilaa aswaababathum-Muswiybatun, qaaluw innaa lil-Laahiwa innaa ilayhi raaji'uwn.].” na humtegemea Mola wake Mwenye Huruma zaidi kuliko wote kwa utulivu.

Hii ndio maana wacha-Mungu wanaridhika na kutambua kwao kutoweza kujisaidiambele ya Allah, na huweka matumaini yao yote kwenye uamuzi wa Allah.

Hakika kuna raha katika kumwogopa Allah. Ikiwa mtoto wa mwaka mmoja angeulizwa ni kitu gani kinachopendeza kuliko vyote, angesema: ‘kulindwa katika kumbatizi zuri la mama yangu, huku nikiwa najua udhaifu wangu na kutoweza kujisaidia – badala ya kuadhibiwakama nilivyotazamia.’ Hata hivyo, jumla ya huruma walizo nazoakina mama wote duniani ni chembe ndogo tu ya Huruma ya Allah. Kwa sababu hii, watu wenye ukamilifu hufurahia sana kuwa na hali ya kutoweza kujisaidia na kumwogopa Allah, na huacha vyote vilivyomo katika uwezo wao wenyewe na kufuata ukimbizi kwa Allah. Wanaufanya woga na kule kutoweza kujisaidia kuwa upatanishimbele ya Allah.

Dawa nyingine ni kumwomba Allah kwa kumtolea shukrani na ridhaa, na kutegemea Rehema ya Mpaji wa Vyote, Mkarimu. Ni juu yetu kuomba, na juu ya Allah kutoa. Anawezaje Mpaji wa Vyote Mkarimu, Ambaye kaitandika sura yote ya ardhi kama meza kwa ajili yao na akayafanya majira ya vuli kwa ajili ya maua ya kuweka juu ya meza; vipi wageni wa Huyo wanaweza kuuhesabu ufukara wao wenyewe na kutoweza kujisaidia mbele ya Allah kuwa ni mzigo usiobebeka? Hawawezi! Kwao wao ufukara na mahitaji huwa ni shauku hivyo hujaribu kuongeza ufukara - ndio maana watu wenye ukamilifu hujivunia ufukara: (Lakini hii isieleweke vibaya: kutambua ufukara wake mtu katika maudhui haya humaanisha ufukara wake mbele ya Allah, haimaanishi kuwa mhitaji na ombaomba kwa watu wenzio). Kuhusu pasi ya kuendea Milele, ni sala tano za kila siku, kutekeleza wajibumwingine, na kuepuka dhambi kuu. Kama ilivyokubaliwa na watu watambuzi na wasomi, njia pekee ya kupata mwanga na mafao na chombo kichukuzi kwa safari ndefu kwendea Milele ni kuzishika amri za Qur’an na kujizuia na makatazo yake. Kuwa na sayansi na falsafa na ufundi na busara peke yake havina maana sana kwani vitu hivi huangaza yu barabara hadi kufikia kaburini.

Ni muhimu kiasi gani, na rahisi, na nyepesi kazi ya kusimamisha sala tano na kujinyima dhambi kuu saba. Ukiwa na akili, na ni ile isiyoharibika, basi unastahili kujua jinsi yalivyo muhimu na makubwa matokeo ya kusimamisha sala na kuepuka dhambi. Ukishaelewa, utamgeukia yule aliyepotea, na kwa yule anayekuelekeza wewe upotee na utende dhambi, na useme:

“Endapo unaweza kufutilia mbali kifo, fukuzilia mbali hali ya kutoweza kujisaidia na ufukara, na ufunge mlango wa kwenda kaburini - kisha tuonyeshe ili nasi tuone. Vinginevyo nyamaza na uniache niisikilize Qur’an inavyoelezea ulimwengu. Tujazwe na nuru yake. Tutende mambo kwa muujibu wa mwongozo wake. Kwani Qur’an ni ukweli kwa vile inakuja kutoka kwa Muumba - na inasema ukweli, ikisambaza nuru yake kila pahala.

Ewe Allah, iangaze mioyo yetu kwa nuru ya imani na Qur’an. Ewe Allah, ututajirishe na ufukana kuhusiana na Wewe. Usitufirisi kwa kukupuuza Wewe.

Tumejitolea nguvu na uwezo wetu kwa ajili Yako, na tumetaka ukimbizi kwenye Uweza Wako na Nguvu, kwa hivyotufanye tuwe miongoni mwa wale wanaoweka imani yao Kwako na usituache peke yetu. Tuhifadhi sisi na Hifadhi Yako. Tupe Rehema sisi na waumini wote, wanaume na wanawake. Mpe Baraka na amani bwana wetu Muhammad, mtumishi Wako na Nabii Wako, mteule wako na rafiki Yako mpenzi - uzuri wa Milki Yako, wa msitari wa mbele kuliko yote wa uumbaji Wako na lengola mapenzi Yako na jua la uongozi Wako; ulimi wa ushahidi Wako, udhihirisho wa Huruma Zako, nuru ya uumbaji Wako, mbora kuliko wote miongoni mwa viumbe Wako, taa ya Upweke Wakomiongoni mwa uwingi wa viumbe Vyako, mfumbuzi wa siri ya uumbaji Wako, mtangazaji wa Milki ya UmolaWako, mhubiri wa kinachokupendeza Wewe, mbainishaji wa Hazina ya Majina Yako, msimamizi wa watumishi Wako, mfafanuzi wa ishara (signs) Zako, kiyoo cha Uzuriwa Umola Wako, mduara na kompasi ya kukusahidilia Wewe na kutufanya Kwako sisi tuwe mashahidi; KipenziChako na Mjumbe Wako ambaye ulimleta awe rehema kwa limwegu zote – na juu ya familia yake na Masahaba zake, na juu ya ndugu zake miongoni mwa manabii na wajumbe, na juu ya malaika Wako walioletwa karibu, na juu yawatumishi Wako waadilifu (righteous). Aamin.


SEKİZİNCİ SÖZ

NENO LA NANE

Umuhimu wa Dini

Kwa Jina la Allah Mwingi wa Rehema na Huruma

2:255 Allah hakuna mungu ila Yeye, Mwenye Uhai wa Maisha (Ever -Living), Aendelezae kila uhai na Yeye Ajiendeleza Mwenyewe (Self Subsistent). [Allwaahu laa ilaaha illaa huwa, al-hayyul-qayyuwm]”

3:19 Bila shaka dini (ya haki) mbele ya Allah ni Uislamu. [Innad-diyna ‘indal-Lwaahil Islaam]”

Ili kuielewa dunia na roho ya mwanadamu ndani yake, kuelewa hali (nature) na thamani ya dini kwa mwanadamu, kuelewa jinsi gani, kungekuwa hakuna hiyo Dini ya kweli, dunia ingalikuwa shimo la giza kuliko yote, na asiyeamini angekuwa kiumbe asiye bahati kuliko wote, kumaizikwa nini na nini kinachofungua ishara ya siri ya ulimwengu huu na kinaikomboa roho ya mwanadamu kutoka katika giza, ni imani katika Kuwepo na Umoja wa Allah, na utegemezi Kwake - soma hadithi hii ya mafunzo:

Hapo kale, kulikuweko ndugu wawili waliofunga safari ndefu kwa pamoja.

Mmoja alikuwa ni mwenye kujipa kila alitakalona mwerevu. Mwingine ana nidhamu ya binafsi na ana hekima. Baada ya muda wanaifikia njia-panda katika barabara yao wanakomkuta mzee mwenye hekima. Wakamuuliza wapite njia gani. Akawaambia njia ya kulia inahitaji kutii sheria inayotawala ile barabara, lakini huu mzigo wa kutii huleta usalama fulani na furaha; wakati njia ya kushoto inaahidi uhuru inaowakilisha na pia hatari fulani na hudhuni. Akasema, “Sasa uchaguzi ni wenu.”

Alivyosikia hivi, yule ndugu aliye na nidhamu safi, akimuamini na kumtegemea Allah, akaenda kulia na akasema yeye anakubali kuitegemea sharia na mpangilio mzuri. Ndugu mwingine akaelekea kushoto kwa sababu tu ya uhuru. Kwa nje akaonekana karidhika lakini kwa hakika kwa ndani hakuhisi utulivu. Akafika katika jangwa. Ghafla akasikia sauti ya kutisha ya nyama la mwitu (beast) anayetaka kumshambulia. Akakimbia hadi akafika kwenye kisima kilichokauka chenye kina cha mita 60, akajitumbukiza humo. Alipotumbukia nusu ya kina, akakutana na mti ulioota kwenye kuta za kisima hicho. Akaning’inia katika huo mti ili kujiokoa asitumbukie zaidi.

Huo mti ulikuwa na mizizi miwili. Panya wawili, mmoja mweupe na mmoja mweusi walikuwa wakiitafuna hiyo mizizi. Yule mtu akitazama juu anaona lile nyama la mwitu bado linamngojea kule juu ya kisima.Akitazama chini anaona lipo jidudela kutisha limekaribia miguu yake, domo lake kubwa likiwa wazi kumpokea. Kwa kuwa alikuwa na wasaa wa kutazama uzuri, huyo mtu alichunguza kwa makini kuta za kisima akaona zote zimefunikwa na wadudu wafanyao kazi. Akautazama mti ule tena. Akaona kuwa mti huo ulikuwa mtini, na kwa miujiza yake ulikuwa na matundaaina mbali mbali, kama jozi na makomamanga Pale aliponing’inia kisimani, hakuelewa kuwa yote yale yalikuwa yakitokea yana maana au umuhimu wa namna yeyote, kwamba mandhari na matukio hayo ndani yake hayawezi kuwa yametokea kwa bahati tu. Kwamba lazima yawepo, ziwepo siri fulani za matukio haya yote, kwamba nyuma ya mandhari na mtukio haya yote sharti asimame mpangaji na mtendaji wa yote - lakini hakuna hata moja ya haya yanayompitia akilini mwake kwa sababu kukosa kutafakari .

Sasa ingawa mtu huyu kindani alifadhaishwa na hali hii, na roho yakena moyo wake ukawa unalalamika, nafsi yake yenye kuamrisha maovu inajidai kahuna kitu cha kulalamikia, kwa hivyo hajali kulia kwa moyo wake na roho yake.Huyo mtu anajifanya yuko bustanini, akifurahi tu, akaanza kula matunda ya kila aina bure - lakini baadhi yao ikatokezea kuwa yana sumu na yana madhara kwake kuyala hivi.

Katika Hadith Qudsi (usemi wa Mtume, ambao maneno yake ni ya Mtume, lakini maana yake ni ya Allah). Allah Anasema hivi:

Nitamtendamtumishi Wangu kwa muujibu wa yeye anavyonifikiria Mimi.”

Huyu mtu mjinga aliyetumbukia kisimani analiona kila tukio lililomfika yeye kama tukio tu, kama halina uzito wala maana yeyote zaidi ya hivo - na kwake yeye, ndivyo ilivyo.

Hafi lakini haishi vizuri pia. Anang’ang’ania tu katika machungu ya kuwekwa juu juu.

Sasa hebu tumfuatilie yule ndugu mwingine. Yeye ni ana busara zaidi kati yao wawili, kwa sababu yeye ana nidhamu zana, na hana wasiwasi. Kila saa hufikiria mazuri, anazingatia sheria, na anajihisi mwenyewe ana usalama na yu huru ndani ya hiyo sheria.

Kila anapokuwa safarini, huingia bustanini na hukuta, baki ya maua mazuri na matunda ya kuvutia, vitu vibaya na vilivyoharibika mle, anaweza kugeuza akili yake kwenye vile vilivyokuwa vizuri na safi. Yule ndugu yake hawezi na wala hafanzi hivyo; amejihusisha na maovu na hviyo hawezi kufarijika katika bustani kama hilo. Yule ndugu mwenye hekima huishi kwa muujibu wa usemi: “Wewe tazama upande mzuri wa kila jambo”, na kwa hivyo huwa na furaha kwa kila jambo. Humo njiani, naye pia alilikuta jangwa, kama mwenziwe alivyolikuta, na nyama la mwitu linamtokea.Yeye pia anaogopa lakini sio kama yule ndugu yake, kwa sababu ana hakika kuwa hilo nyama la mwitu lazima liwe limetumwa na mkuu fulani. Huyu mtu mwenye nidhamu naye pia anajitumbukiza kwenye kilichopo hapo, na afikapo nusu njia anakamata matawi ya mti; naye pia anawaona panya wawili wanaoitafuna mizizi miwili ya huomti. Akitazama chini aliliona lile dude , na kule juu lile dude bado linamngojea. Kama yule ndugu yake, anaona kuwa haya mambo ni ya ajabu. Lakini kwa kuwa ana nidhamu na mwenye hekima, anaona kuwa mamboi yote haya mageni yamepangwa na nguvu fulani na ni ishara. Anahisi kuwa hayuko peke yake, na kuwa anaangaliwa na kutahiniwa na nguvu fulani. Anaelewa kuwa anaongozwa kwa njia fulani na huo ni mtihani na una madhumuni fulani.

Anamfikiria huyo aliyepanga matukio yote haya na anauliza: “Ni nani Huyu Ambaye Anataka mimi nimjue Yeye?’ Katika kujihoji hvi mtu huyo bado ana subira na nidhamu zake kamili, kwa hiyo hii kujihoji kunazusha ari yake ya kumpenda Huyo mmiliki wa hiyo ishara. Upendo huo pia unamfanya awe na hamu ya kuelewa hiyo ishara na maana ya hayo matukio, na matakwa ya kuzipata sifa njemaambazo zitampendeza huyo mmiliki wa ishara.

Anaona kwamba ule mti anaouning’inia ni mtini lakina aina ambayo inazaa takribani kila namna ya matunda. Haoni woga tena; anaelewa kuwa mti huu unakuwa kama orodha ya matunda ambayo yanamilikiwa na Mwenyewe Ambaye haonekani, ambayo Huyo Mmiliki kaandaa kwa wageni wake kule bustanini. Vinginevyo mti mmoja hauwezi kuzaa aina nyingi hivyo za matunda kama unavyozaa mti huu.

Huanza kuomba kwa dhati na matokeo yake, hufunuliwa (inspired) ufunguo wa siri.

Kisha husema:

“Ewe Mmiliki wa mandhari hii na matukio haya yote, mimi wote niko mikononi mwako. Naomba ukimbizi Kwako na niko tayari kukufanyia lolote. Nataka idhini Yako na nina hamu ya kukujua Wewe.”

Kufuatia sala hii, ukuta wa kisima ghafla bila kutazamia unapasuka, na mlango unafungukia kwenye bustani nzuri ajabu. Hakika lile domo la lile jidude limegeuka kuwa mlango, na vyote jidude na nyama la mwitu yanakuwa ni watumishi wawili wanaomualika yeye aingie. Lile nyama la mwitu hugeuka hasa kuwa farasi wa yeye kumpanda.

Na kwa hivyo ewe roho vivu, na ewe rafiki yangu ninayekuwazia kichwani! Hebu sasa tulinganishe misimamo ya hawa ndugu wawili, ili tupate kuona kuwa zuri huleta zuri, na ovu huleta ovu:

Yule msafiri aliyekwenda kushoto, njia ya kujiamini mwenyewena uhuru wa kujitakia , yu akaribia kumezwa na jidude, saa zote ana wasiwasi. Ana upweke na hujihisi kuwa ni mfungwa anayekabili mashambulizi ya manyama ya mwitu. Tena, huongezea zaidi katika hudhuni hizi kwa kula matunda ambayo yaelekea kuwa matamu lakini yana sumu, ambayo yameletwa kuwa kamasampuli tu, hayakukusudiwa yaliwe kwa ajili yake yenyewe bali kwa ajili ya kuwashawishi walaji kuyatafuta yale yaliyo halisi na wawe wateja wake. Huyu asiye na bahati hugeuza siku yake kuwa giza; yeye mwenyewe anajionea kwa kubadilisha hali yake kuwa ni kama ya motoni, kwa hivyo hastahili kuhurumiwa, wala hana haki ya kulalamika kwa yeyote.

Kinyume cha hivyo, yule msafiri aliyekwenda kulia, yumo katika bustani akiwa na watumishi waliomzunguka. Analichunguza hata tukio la kigeni na zurikwa woga, na anajiona kuwa yeye ni mgeni mheshimika, akifurahia watumishi wazuri wa Mwenyeji wake Mkarimu. Hayali yale matunda yaliyoko katika mtini ule. Bali huyatazama, na akielewa uhakika wake, huahirisha raha ya kuyala na anafaidi ile fikra ya kuyala baadae.

Huyo mwingine ni kama mtu anayeikataa hali yake ya kupendelewa katika bustani ya kiangaziakizungukwa na marafiki, na badala yake, kwa kujifanya aleweshwa na vilevi vichafu, anajifikiria mwenyewe yuko miongoni mwa manyama ya mwitu wakati wa kipupwe, na analalamika kwa sababu hiyo.Anajihini nafsi yeye mwenyewena anawatukana marafiki zake, kwa hivyo hastahili rehema. Yule ndugu aliyekwenda kulia, njia ambayo inayokubali kwa kuamini kila alichopewa na anatii sharia, anaona na kuukubali ukweliwote ambao kwake yeye ni mzuri. Kwa kufanya hivi anamheshimu yule aliye na ukweli, na ndio maana ndugu huyu anastahili rehema. Kwa njia hii tunaweza kuelewa angalau kidogo, maana ya amri ya Qur’an:

4:79 Wema uliokufikia umetoka kwa Allah, na ubaya uliokufikia unatoka nafsini mwako. [Maa aswaabaka min hasanatin fa minal-Lwaahi wa maa aswaabakamin sayyiatin fa min-nafsika].”

Tukianza kufikiri juu ya tofauti baina ya ndugu hawa wawili tunaona kwamba nafsi ya ndani ya mmoja wao iliandaa hali kama ya motoni kwa ajili yake, inayotokana na msimamo wake kuhusu ukweli, ambapo kuhusu yule ndugu mwingine, uzuri aliozaliwa nao, nia chanya, na hali asilia njema, vilimpeleka katika hali ya furaha na ya kupendelewa sana. Sasa, naiambia nafsi yangu ya ndani na nafsi ya ndani ya kila aliyesoma mpaka hapa:Ikiwa unataka kuwa kama yule ndugu mwenye bahati zaidi fuata mwongozo wa Qur’an. Taarifa ya hadithi hii inaweza kuelezewa kwa kirefu, lakini kiini chake kwa ufupi ni hiki:

Mmoja wa hao ndugu ni muumini ambaye ana moyo mzuri, na yule mwingine ni asiyeamini na mwenye kukufuru. Kuhusu zile njia mbili ile ya kulia ndio njia ya Qur’an na imani ambapo ile nyingine ni njia ya kutoamini na ya kuasi. Bustani lililo njiani ni jamii ya wanadamu na ustaarabu ambayo ina yote mawili ndani yake - uzuri na ubaya, usafi na uchafu. Mtu mwenye akili ni yule atendaye mambo kwa kufuata kanuni:

“Chukua yaliyo dhahiri na mazuri, na yawache yaliyotibukana yaliyo na wasiwasi”,

na anaendelea na safari yake na utulivu moyoni mwake.

Jangwa katika hadithi hii ni ardhi, na nyama la mwitulinalojitokeza bila kutazamiwa ni kifo. Kisima ni maisha ya mwanadamu, na kina cha mita sitini ni wastani wa umri wetu wa miaka sitini. Mti mle ndani kisimani ni maisha yenyewe, na wale panya wawili waliokuwa wakiitafuna mizizi yake miwili ni mchana na usiku. Lile jidude mle ndani kisimani ni mlango wa kaburi, mlango wa Maisha baada ya Kifo na kwa muumini, huwa ndio mlango wa kuingilia Bustanini. Wale wadudu kwenye ukuta wa kisima ni matatizo ambayo huwakabili watu humu duniani. Hata hivyo hayo matatizo ni maonyo ya taratibu ya Allah kwa muumin, kumzuia asitelezee kwenye usingizi wa kutojali. Na matunda juu ya mti, kama tulivyodokezea, ni mafao ya dunia hii ambayo yameletwa kama sampuli kutoka kwenye baraka za Maisha baada ya Kifo, yanayowaalika wateja kuelekea kwenye matunda ya Peponi.

(Kuna mti mmoja tu kisimani, lakini una matunda mbalimbali. Hii yaonyesha Lakiri ya Uungu Ambayo uzuri wake pekee ni “kuumba kila kitu kutoka katika kitu kimoja” na “kubadilisha kila kitu kuwa kitu kimoja”, kutengeneza mimea na matunda mbali mbalikutoka katika udongo mmoja tu; kuumba viumbe vyote hai kwa tone moja tu la maji, kuvilisha na kuviendeleza vyote sawa sawavyote vilivyo hai kwa kutumia aina mbali mbali za vyakula.)

Turejee kwenye hadithi, ishara inaonyesha radhi ya siri ya Allah katika kuumba; hii ishara hufunguliwa kwa imani, na pale ufunguo wake ni:

“Ewe Allah, hakuna mungu ila Allah; Allah hakuna mungu ila Yeye, Mwenye Uhai wa Maisha,Aendelezae kila uhai na Yeye Ajiendeleza Mwenyewe”

Kwa mmoja wa wale ndugu, domo la lile jidude hugeuka likawa mlango wa kuingilia Bustanini. Hii ni alama kuwa, wakati kwa yule ndugu mwingine, kama ilivyo kwa wasioamini wote, kaburi ni mlango wa kuendea pahala pa matatizo, tumbo la jidude, kwa wanaoamini ni mlango wa kuendea katika Bustani la Milele ambalo ndio baraka ya Allah kwa wafuasi watii wa Qur’an.

Lile nyama la mwitu hugeuka kuwa mtumishi mtiifu, farasi mwenye nidhamu aliyefunzwa. Hii ina maana kuwa, kwa wasioamini, kifo ni kutengwa kuchungu kutoka kwa wapendwa, aina ya kifungo bada ya kuiacha dunia inayoonekana kama ndio pepo.

Kwa upande mwingine, kwa wale wanaoamini, ni njia ya kuungana na marafiki na washirika wao ambao wamekwishakwenda kwenye Maisha baada ya Kifo, ni sawa kama kwenda kwenye makazi yao ya milele ya furaha. Kwao wao ni mualiko rasmi wa wao kwenda katika Mabustani ya Milele kutoka jela ya duniani; wakati wa kupokea mshahara ambao utatolewa kwa ukarimu wa Yeye Mwenye Huruma na Rehema nyingi kuliko zote kwa ajili ya kazi Alizotendewa Yeye, na aina ya kustahafu kutoka katika mzigo wa maisha Kwa ujumla, yule anayechagua maisha ya mpito kama lengo lake, anajiingiza katika moto ingawa anaishi katika ile anayiita ni pepo duniani. Kinyume cha hivi, yule anayelenga katika maisha ya milele atapata amani na furaha katika dunia zote mbili. Juu ya matatizo yote, bado anamshukuru Allah na atakamilisha maisha yake ya dunia kwa ustahamilivu ambayo, kama atavyokujaelewa vizuri, ni chumba cha kupumzikiatu kinachoelekea mbinguni.

Ewe Allah, tufanye tuwe miongoni mwa watu wenye furaha, uokovu, Qur’an, na imani! Aamin.Ewe Allah, mpe amani na baraka bwana wetu Muhammad, na wape familia yake na Maswahaba, zipe idadi zote za herufi zote zilizomo katika maneno ya Qur’an, yanayorudishwa kwa idhini ya Yeye Mwenye Huruma kuliko wote kwenye mawimbi ya sauti ya kila neno linalosomwa na wasomaji wa Qur’an, tokea mwanzo ilipofunuliwa mpaka mwisho wa muda, na tupe Rehema sisi na wazazi wetu, na wape Rehema waumini wote wa kiume na wa kike, kwa idadi ya maneno hayo kwa njia ya Rehema Zako, Ewe Mwingi wa Rehema kuliko wenye wingi wa rehema. Aamin. Na sifa zote zimwendee Allah, Mola wa limwengu zote.


DOKUZUNCU SÖZ

NENO LA TISA

Maana ya Nyakati Mbalimbali za Sala

Kwa Jina la Allah Mwingi wa Rehema na Huruma

“30:17 Basi Mtukuzeni Allah mnapoingia katika nyakati za usiku (isha)na mnapoingia katika nyakati za asibuhi (alfajiri).18: Na sifa zote njema ni Zake Yeye Allah mbinguni na ardhi, na mtukuzeni wakati wa alasiri na mnapoingia katika wakati wa adhuhuri. [17: Fasubhaanal-Lwaahi hiyna tumsuwna wa hiyna tuswbihuwn. 18: Wa lahul hamdu fis-samaawaati wal-ardhwi wa ‘ashiyyanw-wa hiyna tudhwhiruwn.]”

Unaniuliza mimi, ewe Mwislamu mwenzangu, sababu ya kugawanya hizi sala za kila siku katika vipindi maalum vitano. Nitaongelea moja tu ya sababu nyingi.

Kila wakati wa sala sio tu ni kifunguzi cha pahala pa kugeukia, lakini pia ni kiyoo cha utoaji nguvu za Kiungu na mafao ya Kiungu ya dunia nzima katika utoaji huo. Tunaamriwa kusimamisha sala zilizoamriwa katika nyakati hizi maalum ili kumpa ibada na utukufu zaidikwa Yeye Mwenye Nguvu zote zenye Utukufu na kumpa Yeye shukrani zaidi kwa mafao ambayo yamekusanywa baina ya nyakati mbili zozote, ambayo ndio maana ya sala zilizoamriwa. Ili kuelewa kiasi maana hii ngumu, tuna hoja tano za kuzingatia.

Hoja ya Kwanza

Kila sala maalum inasimama kwa ajili ya kumsifu na kumtukuza Allah na kumshukuru Yeye. Yaani ni kumtukuza Yeye kwa kutamka “Subhaan-Allwaah (Utukufu uwe kwa Allah)”, kwa maneno na matendo, kwa kuutambua Ufalme Wake (His Majesty). Ni kumkweza na kumkuza Yeye kwa kutamka “Allwaahu akbar (Allah ni Mkuu kuliko wote)”, kwa maneno na matendo, kwa kuutambua Ukamilifu Wake; na ya tatu ni kwa kutamka “Al-hamdu li Llaah (Sifa zote ziwe kwa Allah)” kwa moyo, ulimi, na mwili, kutoa shukrani Kwake kwa kuitambua Hisani. Kwa sababu hii tunahitimisha kuwa utukuzo, ukwezo, na kusifia , na kutoa shukrani ndio moyo wa sala. Ni kwa sababu hiyo haya yote matatu yapo katika kila sehemu za sala, katika maneno na matendo yote. Tena, baada ya kila sala, ibarahizi tatu takatifu hukaririwa mara 33 kila moja, ili kuthibitisha na kukamilisha malengo ya sala, maana ya sala hutamkwa moja baada ya nyingine kwa haya matamko mafupi.

Hoja ya Pili

Maana ya kuabudu ni hii:

Mwanadamu, mtumishi wa Allah, akitambua dosari zake, udhaifu na ufukara mbele ya Uungu, husujudu kwa upenzi na mshangao mbele ya Ukamilifu wa Yeye Mola, Nguvu Zake za Uungu, ambazo kwayo kila kiumbe hutegemea, na Huruma Yakeya Uungu. Kwa maneno mengine, kwa vile Ufalme wa Yeye Mola unahitajia kuabudiwa na kutiiwa, pia Yeye Mtakatifu unatuhitajiasie wanadamu tutambue dosari zetuna tuombe msamaha Wake, tutangaze kuwa Yeye hana dosari yeyote na katakasika na uamuzi mpotofu wa watu wasiotambua na la muhimu zaidi kushindwa kwa viumbe Vyake.

Ukamilifu wa Nguvu Zake huhitaji kuwa mtumishi, kwa kutambua udhaifu wake na kutoweza kujisaidia miongoni mwa viumbe vyote, hutamka:”Allah ni Mkuu kuliko wote”, kwa kumuabudu na kushangaa mbele ya utukufu wa kazi za Yeye nayetegemewa Milele, na huku akiinama kwa udhalili mkubwa, huomba ukimbizi Kwakena huiweka imani yake Kwake.

Na hazina isiyo kifani ya Huruma ya Mola huhitajia mtumishi atangaze mahitaji yake na yale ya viumbe wengine kwa kusali na kuomba msaada Wake, na hutangaza baraka Zake kwa njia ya kumsifu na kumshukuru, kwa kutamka “Al-hamdu li-Laah”. Kwa ufupi, maneno na matendo ya sala zilizoamriwa yana maana zote, na kwa hivyo ziliamriwa na zikapangwa na Allah.

Hoja ya Tatu

Wanadamu ni mfano mdogo wa ulimwengu wote; kwa njia hiyo hiyo Sura ya kwanza ya Qur'an, Al-Faatiha, ni mfano mdogo uliong'arishwa wa Kitabu chote;na sala ni fahirisi ing'aayo, inayohusisha njia zote za ibada, na ramani takatifu, inayodokezea aina mbali mbali za kuabudu kwa kabila zote za viumbe hai.

Hoja ya Nne

Mgawanyo unaofuatiliana wa mchana na usiku, miaka na awamu za maisha ya kila mtu humu duniani, ni, twaweza kusema, saa kubwa sana ambayo sehemu zake zinafanya kazi kama magurudumu na nyenzo za saa ambayo, kila vinapotembea, huhesabu sekunde, dakika na saa.

Kwa mfano:

Wakati wa Fajr (asubuhi sana) uliochaguliwa uwe wa sala a asubuhi, mpaka mawio ya jua, unaweza kufananishwa na kuzaliwa kwa majira yamasika, au wakati ambao mbegu ya kiume hupata ukimbizi katika tumbo la uzazi litakaloilinda, au kwa siku ya kwanza kati ya zile siku sita mfululizo ambapo dunia na anga ziliumbwa, na inakumbusha jinsi Allah Anavyotumia Nguvu Yake na Anavyotenda katika nyakati hizo na matukio hayo.

Wakati wa Dhuhr (mara baada ya saa sita mchana), waweza kufananishwa na kukamilika kwa balehe, au katikati ya kiangazi, au wakati wa kuumbwa mwanadamu katika maisha wa dunia. Hii pia inaonyesha udhihirisho wa huruma wa Allah na wingi wa baraka katika matukio hayo na vipindi hivyo.

Wakati wa 'Aswr (alasiri) inafanana na majira ya masika, na uzee, na wakati wa Nabii wa Mwisho, ulioitwa ni Wakati wa Furaha. Inakumbusha akilini matendo ya Uungu na mafao ya Mwenye Huruma Zote ndani yake.

Wakati wa Maghrib (machweo ya jua) inakumbusha kule kwisha kwa viumbe vingi mwishoni mwa majira ya masika na kifo cha mwanadamu. Kwa hivyo unatutahadharisha mapema sisi juu ya kuteketezwa kwa dunia mwanzoni mwa Ufufuo, na pia hutufundisha jinsi ya kuelewa udhihirisho wa Ufalme wa Allah na kwa njia hii hutuamsha sisi kutoka kwenye usingizi mzito wa kupuuza.

Wakati wa 'Isha (usiku), unakumbusha dunia ya giza na jinsi inavyovifunika kwa pazia vitu vyote vya mchana kwa sanda yake nyeusi, na majira ya kipupwe yanavyofunika ardhi iliyokufa kwa mashuka yake ya kaburini meupe. Hukumbusha pia kazi zilizobaki za wafu kusahauliwa kabisa, na hutuonyesha sisi kwisha kabisa kwa dunia ambako hakuepukiki ambayo ni pahala pa majaribio. Kwa hivyo wakati wa 'Isha hutangaza matendo ya kutisha ya Yeye Mwenye Nguvu ya Ushindi wa Ufalme.

Wakati wa usiku, kwa kukumbuka yote mawili majira ya kipupwe na kaburi, na Dunia ya Katikati, humkumbusha mtu kwa kiasi gani roho ya mwanadamu inatarajia Rehema ya Yeye Mwingi wa Rehema zote.

Sala ya Tahajjud, wakati wa baadae wa sehemu ya ndani ya usiku, hutukumbusha jinsi itakavyokuwa mwanga muhimu sana katika giza zito la kaburi. Kwa njia hii, kwa kukumbuka mafao yasiyo kifani ya Mpaji wa Kweli Aliyompa mwanadamu katika mlolongo wa matukio yote haya ya kipekee, huionyesha jinsi ambavyo Yeye Anastahili sana kusifiwa na kushukuriwa.

Asubuhi inayofuata ni wakati ambao unaashiria ile asubuhi inayofuatia Ufufuo; kama ambavyo ni muhimu, ni ya maana, na ya hakika, asubuhi hiyo hufuatia baada ya usiku, na majira ya vuli huja baada ya kipupwe, basi ndivyo asubuhi ya Ufufuo au vuli inayofuatia Maisha ya Katikati ni hakika kabisa kuwa itakuja.

Sasa tunaelewa kwamba kila wakati uliochaguliwa kwa ajili ya sala tano za kila siku, ni mwanzo wa pahala muhimu pa kugeukia, na ni kumbukumbu ya mageuzi makubwa zaidi au muhala mwa kugeukia katika maisha ya ulimwengu. Kwa njia ya utoaji wa kutisha wa kila siku wa Nguvu za Yeye Ategemewaye Milele, nyakati za sala zinakumbusha miujiza ya Nguvu za Uungu na zawadi za Rehema za Uungu katika kila mwaka, kila kizazi, na kila muhula.

Kwa hivyo sala zilizoamriwa ambazo ni wajabu wa kiasli na msingi wa ibada na deni lisilohojika la mwanadamu, ni muafaka kabisa na zinafaa kwa nyakati hizi.

Hoja ya Tano

Mwanadamu ameumbwa akiwa dhaifu sana, ke bado kila kitu kinamhusisha, kinamuathiri na kinamfadhaisha yeye. Pia hana kabisa nguvu, juu ya kuwa maafa na maadui wanaomkabili ni wengi mno. Tena yu fukara sana na ana mahitaji kem kem. Isitoshe yu mvivu na hajiwezi, na bado mzigo wake wa maisha ni mzito sana. Akiwa ni mwanadamu, ameungana na dunia iliyobaki, ke bado utowekaji wa vitu anavyovipenda na ambavyoanavijua, na machungu ambayo huweza kusababishwa na haya, hurudiarudia kumtesa. Mwisho, akili yake na hisia zake humhimiza kuwa na malengo ya utukufu na humuelekeza kwenye faida za milele, lakini hawezi, hana subira, asiye nguvu, na ana kiwango kifupi cha maisha.

Kwa hiyo inaweza kueleweka waziwazi jinsi ambavyo ilivyo muhimu kwa roho ikiwa katika hali kama hii, wakati wa Fajr - asubuhi mapoema - kuwakilisha maombi, kwa njia ya sala na dua, mbele ya Makao Makuuya Mwenye Nguvu Zote za Ufalme, Mwenye Huruma Zote za Hisani, kuomba fanaka na msaada kutoka Kwake, na jinsi alivyo muhimu kama wa kumwegemea ili aweze kuhimili na kuvumilia matatizo na mizigo inayoweza kumkabili wakati wa mchana.

Dhuhr (adhuhuri)ni kipindi cha wakati ambapo siku iko kileleni kwake (at its zenith), na inaanza kwenda mbele kukamilisha mzunguko wake na watu hupaa mapumziko ya muda kutoka katika shughuli na mambo mengine, na wakati roho yahitaji kusimama kutoka kwenye kutojali na kutohisi kunakosababishwa na kazi ngumu, na mafao ya Uungu yanaonekana kikamilifu.

Ni vigumu, basi, kumwita mtu ni mwanadamu kikweli ambaye hatambui jinsi ni ilivyo vizuri, muhimu, inapendeza kusimamisha sala ya adhuhuri, ili mwanadamu, aliye kwenye mapumziko kutoka kwenye mishinikizo ya maisha ya kila siku na kutoka kwenye kutojali, asimame kidhalili mbele ya Mtoaji Halisi wa baraka, atoe shukrani zake na husali ili apate msaada Wake. Pia huinama ili kuonesha kutojiweza kwake mbele ya Utukufu Wake na Nguvu Zake, na husujudu kutangaza kushangaa kwake, upenzi na udhalili mbele Ukamilifu Wake wa Milele na Hisani zisizo kifani .

Ama kwa wakati wa 'Aswr, alasiri, unafanana na unakumbusha wakati wa kusikitisha wa majira ya masika na hatua za minung'uniko za uzee, na kipindi cha kuhudhunisha cha mwisho wa wakati. Ni wakati ambapo kazi za siku zinakamilishwa, na mafao ya Uungu ya siku ile yanapokewa, kama afya, usalama, na huduma nzuri kwa ajili ya Allah, vimekusanyika kuunda jumla kubwa. Pia ni wakati ambao huwa tunaona jua linafifia chini upeoni kuthibitisha kuwa kila kitu sio cha kudumu: leo kipo kesho kimetoweka. Sasa mwanadamu ambaye anapenda umilele na ambaye kaumbwa kwa ajili hiyo, na anaonyesha heshima kwa mafao anayopewa, lakini ambaye ana hudhuni kwa sababu ya mitengano maalumu, husimama, akachukua udhu, na baada ya hivyo akasali sala iliyoamriwa. Kwa hivyo, yeyote ambaye ni mwanadamu kikwelikweli, anaweza kuelewa jinsi ilivyowajibu wake muhimu, jinsi ilivyo huduma muafaka, jinsi ilivyokuwa ni njia bora ya kulipa deni la shukrani, hakika, jinsi ilivyokuwa raha nzuri kusimamisha sala ya alasiri. Kwani kwa kuomba dua mbele ya Makao Makuu ya Milele ya Mtegemewa wa Milele Muendelezaji na Anayejiendeleza Mwenyewe, kwa kuomba ukimbizi kwenye Rehema zisizo kifani, na kwa kutoa shukrani kwa mafao Yake yasiyohesabika,kwa kuinama kidhalili mbele ya Nguvu na Utukufu wa Mwenye Umola, na kwa kusujudu katika udhalili wa hali ya juu kabisa mbele ya Mwenye Uungu wa Milele, huwa na amani ya akilina hupata faraja ya kweli na wepesi wa roho.

Wakati wa jioni hutukumbusha mwanzo wa majira ya kipupwe na wa kwa-heri za hudhuni za viumbe dhaifu vya majira ya kiangazi na masika; inakumbusha pia kutengana kwa kusikitisha kwa mwanadamu na wapendwa wake kwa njia ya vifo. Tena inakumbusha wakati wa taa ya jua la ardhi, hapa pahala pa majaribio, itazimishwa na wakazi wa dunia hii watahama kwenda katika dunia nyingine, kufuatia kubomoka kunakosababishwa na mitetemeko ya mwisho ya ardhi. Pia ni onyo kali kwa wale wanaoenzi wapendwa wa kupita wa muda, na kila mmoja wao akijua kuwa siku moja atakufa.

Wakati wa sala ya jioni, roho ya mwanadamu, ambayo kwa asili yake hupenda sana Uzuri wa Milele,hugeukia Kwake Yeye wa Milele, Ambaye huumba na kuunda matukio yote haya. Ambaye anaziongoza sayari za anga. Ni wakati ambao roho ya mwanadamu hukataa kutegemea kitu chochote chenye mwisho, na hulia Allwaahu akbar! - maana yake Allah ndiye Mkubwa kuliko wote. Kisha mbele Yake, hutamka Alhamdu li-Llaah, sifa zote zimwendee Allah, mwanadamu humsifia Yeye kwa kutambua kuwa Ukamilifu Wake usio dosari, Uzuri usio kifani, Hisani, na Rehema isiyo kiwango. Baadaye, kwa kutamka:

“1:5 Wewe tu Ndiye tunayekuabudu, na Wewe tu Ndiye tunayekuomba msaada.”

Humuabudu na kutaka msaada kwa Mola Asiye na msaidizi, Mwenye Uungu usio mshirika, na Ufalme wa bila kuchangia. Kisha mwanadamu huinama mbele ya Ukuu Usio kipimo, Uweza usio kikomo, na Heshima na Utukufu Mkamilifu, hivyo anaonyesha, pamoja na viumbe vyote, udhaifu na kutoweza kujisaidia kwake, na udhalili na ufukara, na husema:”Utukufu uwe kwa Mola wangu, Mwenye Nguvu”.Baada ya hivi, husujudu mbele Yake kwa kutambua Uzuri usiokufa na Hisani ya Asili Yake, Sifa Zake takatifu zisizobadilika, na Ukamilifu Wake wa siku zote, mwanadamu hutamka kwa kumtenganisha na wote isipokuwa Yeye, mapenzi yake na utumishi wake kwa kushangaa na kujidhalilisha, humpata Yeye Mwingi wa Uzuri wa Kudumu, Mwenye Huruma zote wa Milele, na kwa kutamka:

Utukufu uwe kwa Mola wangu, Aliyetukuzwa kuliko wote

humtangazaMola wake Aliyekwezwa kuliko wote, kuwa katakasika na upungufu na dosari yeyote.

Baada ya hivyo, mwanadamu hukaakinyenyekevu na kwa hiari yake, na hutoa kwa hiari yake mwenyewe, sifa na tukuzo kwa Yeye wa Milele, Mwenye Nguvu zote na Mwenye Ufalme wote kwa ajili ya viumbe wote, na humuomba Allah kumpelekea amani na baraka kwa Mjumbe Wake Mtakatifu. Kwa kufanya hivyo, hujadidisha utii wake kwa Mjumbe wa Allah na kutangaza utii wake kwa amri zake, hujadidisha na kuimarisha imani yake, na, kwa kuzingatia amri hiyo ya busara katika kasri hili la ulimwengu, huwa anashahidilia Upweke wa Muumba na Ujumbe wa Muhammad, ambaye ndiye mtangazaji wa Ufalme wa Umola wa Allah, mtangazaji wa mambo ambayo yampendeza Yeye, na mfafanuzi wa ishara na aya za Kitabu cha Ulimwengu.

Basi vipi mtu anaweza kuwa mwanadamu kweli asiyetambua jinsi sala ya jioni ilivyo wajibu muruwa, jinsi lilivyo tendo la raha la huduma, jinsi ilivyo aina nzuri ya ibada, jinsi lilivyokuwa jambo muhimu, jinsi yalivyo mazungumzo muruwa na Muumba na ilivho furaha ya kudumu katika nyumba hii ya wageni ya muda.

Wakati wa ‘Isha (usiku), ukiwa ndio wakati ambao mabaki ya mwisho ya siku upeoni hupotea, na usiku hufunika ardhi, hutukumbusha utumiaji imara wa Umola wa Allah Akiwa ni Mbadilishaji wa Usiku na Mchana, na wa shughuli za Uungu za Mwenye Hekima zote wa Kikamilifu Akiwa ni Anayelishinda Jua na Mwezi, Anayeonekana katika kugeuza ukurasa mweupe wa mchana kuwa ukurasa mweusi wa usiku, na katika kubadilisha vizuri maandishi yenye rangi ya kiangazi yawe ukurasa tasa mweupe wa kipupwe. Wakati huu wa siku pia unatukumbusha pia matendo ya Allah kama Muumbaji wa Maisha na Vifo katika kuhamishia kikamilifu kazi zawafu kwenye dunia nyingine utakapowadia wakati wake. Ni wakati unaokumbusha utumiaji kwa kifalme na udhihirishaji wa kihisani wa Allah kama Muumbaji wa Mbingu na Ardhi katika kuiteketeza kabisa hii dunia finyu, dhalili na ambayo hufa kwa ngurumo na misukosuko, na katikakukunjuka kwa Dunia ya Maisha Baada ya Kifo hii pana, ya milele na ya kifalme. Pia inaonya kuwa ni Yeye tu Anayeweza kirahisi kabisa kugeuza mchana kuwa usiku, kipupwe kuwa kiangazi, na hii dunia kuwa dunia nyingine, Ndiye anayeweza kuwa Mmiliki na Mkuu wa Kweli wa ulimwengu, Ambaye ndiye pekee anayestahili kuabudiwa na kupendwa kwa dhati.

Kwa hivyo, ujapo usiku, roho ya mwanadamu ambayo ni dhaifu mno isiyoweza kujisaidia, na ni fukara mno inayohitaji mengi, na imetupwa huko na huko kwa sababu mbali mbali na inabingirika mbele kwenye mustaqbali usiojulikana, husimamisha sala ya 'Isha. Kufanya kwake hivyo kuna maana ifuatayo:

“Kama Ibrahim, mwanadamu husema:

“6:76 Na usiku ulipomwingilia (Ibrahim wakati kakaa na makafiri), akaona akaiona nyota, alinena: 'Hii ni Mola wangu'. Ilipotua (ilipopotea hiyo nyota) alisema: 'Sipendiwale wanaopotea (hawawepo ila wakati makhsusi tu).

[Falammaa janna 'alayhil-laylu ra-aa kaukaban, qaala, haadha Rabbiy, fa lammaa afala qaala laa uhibbul-aafiliyn.]”, na kupitia sala zake huomba ukimbizi katika Makao Makuu ya Mwenye Kuishi maisha yote, na Anayeabudiwa wakati wote, Yeye Anayependa wa Milele.

Kutoka kwenye maisha ya mpito tu katika dunia hii ya giza, ya muda mfupi, Hubembeleza kwa Yeye Atayebaki, wa Milele, na kwa muda wa mazungumzo yasiyokwisha, sekunde chache za maisha yasiyoishia kifo, huomba apokee mafao ya Mwingi wa Rehema na Huruma zote, na mwangaza wa uongozi Wake, ambao utaitupia dunia yake mwangaza na ung'arishe mustaqbali, na Ayapoze machungu yatokanayo na kuisha kwa viumbe vyote na marafiki.

Kwa ufupi tu, mwanadamu huisahau dunia, ambayo imemuacha usiku ule, na ashitakie machungu yake ya moyoni katika Makao Makuu ya Rehema huku akilia machozi. Kabla usingizi haujaja, ambao unafanana na kifo, na kwa kuwa lolote laweza kutokea, hutekeleza wajibu wake wa kila siku wa “mwisho” wa kuabudu. Ili apate kufunda uzuri rekodi ya matendo yake ya siku ile, husimama akasali. Yaani, huinuka kwenda mbele ya Mpendwa wa Milele Anayeabudiwa badala ya wale wenye maisha ya kifo ambao amewapenda siku nzima, mbele ya Yeye Mwenye Nguvu zote na Mkarimu sana badala ya viumbe wasiojiweza wenyewe ambao amekuwa akiwaomba siku nzima, mbele ya Mlinzi Mwenye Huruma kwa matarajio ya kuokolewa kutoka kwenye maovu ya viumbe viumizavyo ambavyo amukuwa akitetemeka mbele yao siku nzima.

Huanza na Faatiha, mlango wa ufunguzi wa Qur'an, yaani badala ya kuwavika kilemba cha ukoka na kuwa na deni kwa viumbe vyenyekasoro na vihitaji, ambayo sio sahihi, yeye husifia sifa za Mola wa limwengu zote, Mkamilifuna Ajitoshelezaye Yeye Mwenyewe, Mwenye Huruma na Mkarimu sana. Kisha huendelea kwa kusema:

“1:5 Wewe tu Ndiye tunayekuabudu,

Yaani, juu ya kuwa kwake mpweke na hana maana, kupitia kwenye uhusiano baina ya mwanadamu na Mmiliki wa Siku ya Hukumu, Ambaye Ndiye Mfalme wa Milele, hufukia daraja la kuwa mgeni apendezae na afisa muhimu katika ulimwengu. Kwa njia ya kutamka:

“1:5 Wewe tu Ndiye tunayekuabudu, na Wewe tu Ndiye tunayekuomba msaada.”

Huwakilisha Kwake, kwa niaba ya viumbe vyote, ibada yao na hubembeleza msaada Wake kwaajili ya mkusanyiko wote wa viumbe wote. Kisha, kwa kusema:

“1:6 Tuongoze Njia iliyonyooka.”,

huomba aongozwe kwenye Njia Nyoofu ambayo inaleta furaha ya milele na ndio njia inayong'aa.

Sasa ni zamu ya kusema:”Allah ni Mkuu Kuliko wote”, na kuinama huku Ukifikiria Ukuu wa Yeye Mfalme, Ambaye, kama ile mimea na wanyama wanaolala, majua yaliyofichika na nyota za makaburi ni kama maaskari Ambao wapo chini ya amri Yake, na taa na watumishi katika nyumba hii ya wageni ya duniani. Hufukiri sasa juu ya sijida kubwa ya viumbe vyote:Wakati ikitolewa amri ya “Kuwa! Na ikawa.”, aina zote za viumbe vya kikla umri na kipindi – hata ardhi na ulimwengu – kama jeshi lenye nidhamu kweli la askari watiifu, kila mmoja kapumzishwa kazi yake, yaani kapelekwa kwenye Dunia ya vile ambavyo Havionekani, kwa njia ya kusujudu kwa kifo kwa mpangilio mkalifu, kila kimoja kinatamka: “Allah ni Mkuu kuliko wote”, na anainama kwa ajili ya kusujudu, na wanapoinuliwa ili waishi mnamo vuli, katika ufufuo, sauti ya tarumbeta inayotoa maisha kutoka kwenye amri ya 'Kuwa! Na inakuwa', huamka wote na wakuwa tayari kumtumikia Mola wao. Mwanadamu asiye na maana pia, huku akiwafuata, hutamka: “Allah ni Mkuu Kuliko wote” mbele ya Mwenye Rehema zote za Ukamilifu, Mwenye Huruma zote za Hisani, katika upenzi ulioshikwa na mshangao na udhalili uliotiwa umilele na kujidhalilisha binafsi kwenye heshima, na huinama na kusujudu, yaani hufanikiwa Kupaa kwa aina fulani. Na bila shaka sasa utakuwa umezingatia jinsi ulivyo mzuri, muafaka, wenye kuingia akilini, wa kutukuzwa na kupendeza ule wajibu, huduma, na tendo la ibada, na jinsi kusimamisha sala ya 'Isha kulivyokuwa ni jambo muhimu na la maana sana.

Kwa hivyo, kwa kuwa kila moja ya hizo mara tano ni ishara ya mageuzi makubwa, ishara ya shughuli nyingi za Mola, na sehemu ndogo tu ya mafao ya Kilimwengu ya Kiungu, sala zilizoamriwa, ambazo ni wajibu na deni, Na zimeamriwa kama zilivyotajwa kwa hekima kamilifu.

Utukufu uwe Kwako. Hatuna ujuzi ila ule uliotufunza Wewe. Hakika Wewe Ndiwe Mjuzi wa vyote, Mwenye Hekima zote.

Ewe Allah! Mpe baraka na amani yule ambaye ulimtuma aje awe mwalimu kwa watumishi Wako kuwafunza elimu ya kukujua Wewe na kukuabudu Wewe, na kuwafahamisha hazina za majina Yako, mfafanuzi wa ishara au aya za Kitabu Chako cha Ulimwengu, na kiyoo, kupitia kwenye ibada yake, kwenda kwenye Hisani Yako Wewe Mola, na juu ya familia yake na Maswahaba, na utupe Rehema sisi sote na waumini wote wa kiume na wa kike. Aamin. Kwa ajili ya Huruma Zako Ewe Mwenye Huruma kuliko wote wenye kuonea huruma!


Hiç yorum yok:

Yorum Gönder